Simba SC 4-1 Ruvu Shooting | NBC Premier League | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara NBC Premier League kupigwa leo Mei 8, 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC anamkaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Takwimu na kila kizuri kinaegemea zaidi upande wa Simba SC kwenye mchezo huu lakini kiuhalisia chochote kinaweza kutokea This is Football.

Ni Vita vya Kocha Pablo Franco kwa System ya 4-2-3-1 na Charles Mkwasa dhidi ya System ya 4-3-3 ni Vita vya kwanza kwenye Flanks kisha kulishinda eneo la Kiungo, unategemea kuwaona Simba SC wakitawala eneo la Kiungo, unategemea kuwaona Ruvu Shooting wakisubiri matendo ya pili (Turn Over)

Ruvu Shooting amezuia vizuri kwenye mechi zao tano za mwisho wamepata cleansheet mbili na mechi nyingine mbili kati ya hizo hawajaruhusu zaidi ya goli moja, ni mchezo mmoja tu waliruhusu goli moja, ambapo ni takwimu nzuri kwa daraja ambalo Ruvu Shooting walipo.

Ni mechi ambayo Simba SC anaitaka ili kurejesha Confidence kwani hawajapata ushindi katika mechi tatu za mwisho kwenye Ligi zote ametoa sare, tutegemee kuwaona Simba muda mwingi wakiingia katika zone ya Ruvu Shooting ili kuifungua safu yao ya ulinzi.

Je ni kipi Ruvu Shooting watakifanya dhidi ya Quality ya mpinzani na kucheza dhidi ya presha ya Simba kwa dakika zote tishini, umakini katika kuzuia, ni ngumu kucheza bila ya kufanya kosa hata moja, ni suala la muda kutupa majibu sahihi ndani ya dakika 90.

Kocha msaidizi wa Simba SC Suleiman Matola, amesema kiufundi mechi haitakuwa rahisi, mechi itakuwa ngumu, lakini wamejiandaa kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi.

Naye Kocha msaidizi wa Ruvu Shooting Rajabu Mohamed, amesema kuwa Mechi itakuwa ngumu dhidi ya Timu Kubwa, Kongwe, lakini wamejipanga kujaribu kushinda mchezo huo.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku.. Usikose Ukaambiwa

Kulipewa Mwana..Kulitaka Mwana

..... Ghazwat....


Naaam mpira umeanza uwanja wa Mkapa

Ni Vita vya dakika 90 za jasho na damu

Simba SC 0-0 Ruvu Shooting

02' Simba wanapata Free Kick, inapigwa kulee lakini golikipa Makaka anasafiri na kupangua mpira ule na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

07' Ruvu wapo nyuma mapema tu, Nadhani wanasoma mchezo kuona gani watapenya ngome ya Simba

12' Jaribio kwa Simba kupitia kwa Sakho na Kagere linashindwa kuzaa bao, huku Chanongo akijibu mapigo upande wa Ruvu Shooting

15' Abrahaman Mussa yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha

20' Pamoja kumiliki mpira eneo la kati lakini, bado mambo ni magumu upande wa Simba

23' Mkude yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kuumia, huku Abdulswamadu akionyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya.

24' Kona kuelekea Ruvu, inapigwa kulee Wooooooo, Wawa anapiga shutii lakini linatoka nje ya lango

Ametoka Mkude na nafasi yake anaingia Bwalya upande wa Simba SC | Simba SC 0-0 Ruvu Shooting

30' Henock anamvisha kanzu maridadi mchezaji wa Ruvu, huku Gadiel akikosa nafasi ya kutengeneza bao.

Oyaaa, Peter Banda anashindwa kuweka mpira kambani baada ya jitihada zake kuzimwa na golikipa Makaka

35' Ruvu wanakosa nafasi nzuri ya kupiga shuti lango la Simba, Wawa na Henock wapo nyuma kwa ulinzi mkali.

39' Almanusura Simba SC wapate bao, Shuti kali la Kagere linambabatiza beki wa Ruvu

40' Kibu Goooooooooooooaaal gooal

Kibu Denis anaipatia Simba SC bao kwa kwanza baada ya kutokea piga nikupige lango la Ruvu Shooting

Simba SC 1-0 Ruvu Shooting

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko

Kwake Banda, anapiga Krosi kwake Sakhooo, anakosaaaaaa

Haya kwao Ruvu wanakwenda mbele kuleee, lakini wanakosa vile vile, wanao Simba sasa kuleee Bandaaa looo, Mobby anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari ile..!

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele ya bao moja kwa bila dhidi ya Ruvu.

HT: Simba SC 1-0 Ruvu Shooting

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa na hakuna mabadiliko kwa pande zote mbili.

Ruvu wanapata Free Kick, Abrahaman Mussa anapiga lakini anababatiza ukuta wa Simba SC.. mpira unaokolewa

49' Jaffar anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari lango lake, baada ya mpira wa Kibu anashindwa kutuliza eneo hilo.

52' Mobby na Kibu wapo chini baada ya kugongana wakiwania mpira Krosi uliopigwa na Gadiel

56' Bwalya aliiweka kwenye Presha lango la Ruvu baada ya shuti kali kutoka mida chache ya lango na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

58' Almanusura Ruvu wapate bao kama si uimara wa golikipa Manula kudaka mpira ule

60' Kagereeee goooooo laaaaaa ni Offside, kibendera kipo juuu kuashiria kuwa mfungaji alikuwa ameotea

Buswita anapiga Tikitaka na mpira unatoka nje, alipata pasi safi kutoka kwa Chilambo

67' Bwalya Goooooooooooooaaal gooal

Rally Bwalya anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi murua kutoka kwa Sakho

Simba SC 2-0 Ruvu Shooting

Ameingia Bocco akichukua nafasi ya Kagere upande wa Simba SC

Ruvu wamepoa kipindi hiki cha pili, Simba wanaliandama lango lao, Almanusura Bocco aifungie Simba SC bao.

74' Ally Kombo anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Gadiel

Mabadiliko ametoka Abrahaman Mussa ameingia Said na Ametoka Buswita na ameingia Joseph upande wa Ruvu

79' Mhilu ameingia kuchukua nafasi ya Banda, huku Mwenda akichukua nafasi ya Kapombe pia Mzamiru ametoka na ameingia Kennedy upande wa Simba SC

Bocco Goooooooooooooaaal gooal

John Bocco anaipatia Simba SC bao la tatu akipokea pasi murua kutoka kwa Mhilu

Goooooooooooooaaal gooal

Haruna Chanongo anaipatia Ruvu Shooting bao la kwanza kwa shuti kali

Simba SC 3-1 Ruvu Shooting

Sasa funga nikufunge mpira ni mkali sasa na upo eneo la Ruvu Shooting

Free Kick kuelekea Ruvu Shooting..Inapigwa kulee Goooooooooooooaaal gooal

Henock anaipatia Simba SC bao la nne kwa kichwa | SIMBA SC 4-1 RUVU

Mpira ni mkali Simba wanataka kuongeza bao huku Ruvu wakiwa wanataka kusawazisha, lakini Umiliki wa Simba

Kwake Bocco inapigwa kulee Mhilu anarukaaaa njeee, mpira wa kichwa unatoka nje ya lango, ilikuwa hatari sana..!

99+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo Uwanja wa Benjamin Mkapa

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi mnono wa mabao manne moja dhidi ya Ruvu Shooting

FT: Simba SC 4-1 Ruvu Shooting

........ Ghazwat....
 
Bado mechi ngapi hii ligi iishe, hamu sasa hivi ni kuona Simba SC itawasajili wakina nani, wala sio hizi game tena.

Game yangu iliyobaki ni moja tu; Simba SC vs Dar Young Africans, Semi Final ya Azam Federation.
 
Mechi iliyopita Kolo alimuotea Ruvu baada ya wachezaji wake wengi kuwa depo, leo sioni namna ya Kolo kukwepa kipondo
 
Back
Top Bottom