Simba SC 2 - 1 Yanga SC: Shiza Kichuya aibuka shujaa wa Simba

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,185
103,688
Ndugu wanajukwaa kama mnavyofahamu ile siku mahsusi ya mechi kali kati ya derby wa Tanzania Simba SC na Yanga SC ni leo. Timu hizi licha ya kuwa ni watani wa jadi na zenye mashabiki wengi kuliko timu derby zozote Africa mashariki, zinachuana vikali kutafuta ubingwa zikitofautiana kwa alama moja

Mechi itapigwa katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10 jioni. Mechi hii itarushwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV. TBC1 nayo itarusha moja kwa moja matangazo ya Radio. Jamiiforums nayo haitakuwa nyuma itakuletea moja kwa moja kutoka uwanja wa Taifa

Hatujafanikiwa kupata jina la mgeni rasmi wa mechi hii, lakini habari zilizotufikia ni kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowasa, Mwenyekiti Mh.Mbowe, Waziri wa Ndani Mh.Mwigulu Nchemba, Major wa Ubungo Mh.Jacob, Mrembo wa Tanzania 2006 Mh.Wema Sepetu, watakuwepo uwanjani

Mkuu wenu nitawaletea moja kwa moja mechi hii hapa hapa JF, usiondoke




Goli la kwanza la Simba



Goli la pili la Simba



Updates

DK 1. Mpira umeanza

DK 3: Yanga wanapata penati baada ya Chirwa kuangushwa na mlinzi wa Simba eneo la Penati.

DK 4: Mathew Akrama anamlamba kadi ya njano Lufunga kwa kumuangusha Chirwa

DK 5 - GOOOAAL: Simon Msuva anawaandikia Yanga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati.

DK 10: Simba wanaonesha kumiliki mpira, Yanga wanakuwa makini.

DK 13: Mavugo anapokea pasi nzuri lakini anakuwa butu na kupoteza mpira ule muhimu langoni mwa Yanga, Dida anaudaka.

DK 15: Mchezo sasa upo balanced huku mipango ya Simba ikiwa haijakaa vizuri, wanashindwa kujiamini.

DK 16: Juma Luizio anaotea.

DK 17: Simba wanafanya mashambulizi lakini Dida anawahi na kudaka, Yondani yupo chini baada ya kugongwa katika purukushani hiyo.

DK 19: Kamusoko anapiga krosi murua kutokea kulia, Chirwa anaunganisha kwa kichwa na Agyei anadaka.

DK 20: Yanga wanafanya shambulizi lakini Niyonzima anapiga shuti la kitoto Agyei anaudaka.

DK 22: Kotei anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni kwa Msuva

DK 23: Krosi safi ya Juma Abdul, Zimbwe anaokoa na kuwa kona ya kwanza

DK 23: Niyonzima anachonga kona nzuri hapa lakini Agyei anaruka na kupangua

DK 25: Kamusoko anapokea pasi murua kutoka kwa Chirwa, anapiga shuti lakini mpira haujai vizuri mguu hivyo kuwa dhaifu, Agyei anaudaka.

DK 26 - Sub: Simba wanafanya mabadiliko ya mapema, Anaingia Ndemla na kutoka Luizio.

DK 28: Zuru anapoteza pasi muhimu sana ambayo ingewapa Yanga goli la pili muhimu

DK 29: Nafasi nzuri zaidi kwa Simba, Mavugo akiwa amebaki yeye peke yake na kipa Dida, anapiga mpira wa kichwa dhaifu na unatoka nje.

DK 32: Mavugo anawachambua kama karanga mabeki wa Yanga, Yondani anazuia shuti la Mavugo na Munishi anaudaka.

DK 34: Munishi analeta mbwembwe baada ya kudaka mpira baada ya kukaa na mpira mkononi kwa zaidi ya muda unaoruhusiwa. Simba wanapiga mpira wa adhabu ndogo ndani ya eneo la 18.

DK 35: Said Mdemla anapiga shuti linapaa aka mnazi.

DK 37: Yanga wanafanya shambulizi lakini Agyei anauwahi mpira. Ndemla anapiga shuti maridadi lakini linatoka nje ya lango la goli.

DK 40: Mo Ibrahim anaachia shuti kali sana lakini Munishi anaupoza mpira kwanza na kuudaka.

DK 41: Simba wanaonekana kuzinduka wakati huu wa kuelekea mapumziko. Wanapiga moja mbili lakini Dida anaudaka mpira.

DK 42: Kamusoko anapiga shuti tena lakini mpira haujai mguu, mpira unatoka nje na kuwa goal kick

DK 42: Kamusoko yuko chini baada ya kugongana na Muzamiru

DK 44: Mo Ibrahim analazwa chini karibu na eneo la boksi, anajirusha hadi kwenye 18, wachezaji wa Simba wanadai penati ila refa anasema ni kwenye ukingo wa boksi.

DK 45: Hajibu anapiga mpira wa adhabu, inakuwa goli kick.

DK 45+1: Kamusoko anaonekana hali yake haijatengamaa, analala chini na refa anaita huduma ya kwanza na kumtoa nje ya uwanja

DK 45+3 - Sub: Kamusoko anatoka, anaingia Said Juma Makapu

DK 45+4: Mpira ni mapumzikooooooooo

DK 46: Mpambano wa mahasimu unarejea tena kipindi cha Pili huku Yanga wakiwa kifua mbele kwa bao moja la Msuva.

DK 46: Simba wanafanya mashambulizi ya mfululizo mara mbili lakini umakini wa Munishi anaweza kuokoa hatari zote.

DK 48: Simba wanafanya mashambulizi karibu kabisa na lango la Yanga, Mavugo anamfanyia madhambi mchezaji wa Yanga.

DK 50 -SUB: Anatoka Lufunga anaingia Shiza Kichuya.

DK 52: Mavugo anachezewa madhambi, refa anampa kadi ya njano Vincent wa Yanga

Dk 53: Banda analazimika kufanya kazi ya ziada na kuwa kona
KADI Dk 52, Vicent analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Mavugo

Dk 53: Msuva anageuka vizuri kwenye boksi la Simba na kuachia mkwaju mkali kabisa, GOAL KICK

DK 55- RED CARD: Boukungu anamuangusha Chirwa akiwa amebaki peke yake nje ya eneo la hatari, anatolewa nje kwa kadi nyekundu

DK 56: Anapiga faulu nzuri lakini Agyei anauona mpira na kuudaka.

DK 57: Simba wanafanya shambuli na kupata kona, Kichuya anaenda kuchonga kona.

DK 57- SUB: Simba wanamtoa Mo Ibrahim na nafasi yake inachukuliwa na Jonas Mkude

DK 63: Yanga wanafanya shambulizi lakini Agyei anatokea na kuondosha hatari

DK 64: Hajibu anapiga shuti kimo cha sungura na Munishi anaudaka kwa umaridadi

DK 66- GOOOOAAL: Mavugo anaisawazishia Simba kwa goal la kichwa kwa pasi Murua ya Shiza Kichuya.

DK 68: Simba pamoja na kuwa pungufu wanaonesha kurudi mchezoni na sasa mchezo ni vuta nikuvute.

DK 70- SUB: Anaingia Deus Kaseke kuchukua nafasi ya Hamis Tambwe, Tambwe leo katiwa kibindoni hafurukuti.

DK 72: Yanga wanakwenda vizuri na krosi ya MSuva inazuliwa na Kichuya na kuwa kona

Simba wanaonesha kupambana huku Yanga wakiwa hawajui walifanyalo, Yanga wanapoteza mipira muhimu ambayo ingeweza kuleta madhara.

DK 77: Haruna Niyonzima anaoneshwa kadi ya njano kwa kucheza ndivyo sivyo

DK 78- SUB: Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Mahadhi na kutoka Zuru

DK 81- GOOOOOAL: Shiza Kichuya akitokea upande wa kulia anaingia vizuri na katikati na kumtungua Munishi goal la kiwango, Munishi hakuwa na ujanja wowote wa kuufikia mpira ule.

DK 83: Defence ya Yanga inaonesha kuchoka kabisa, haina tena maelewano.

DK 85: Mavugo anawachambua kama karanga mabeki wa Yanga wasiopungua watatu, anapiga shuti kali sana na linagonga nguzo ya goli.

DK 90: Zinaongezwa dakika 4 za lala salama, Yanga wanaonesha kuchanganyikiwa. Wachezaji wa Simba Kichuya na Mavugo wanajiangusha ili kupoteza muda.

DK 90+1: Hatari langoni mwa Simba lakini inakuwa goal kick, Agyei anachelewesha mpira Msuva anaukimbilia na kumtengea kipa.

DK 90+4: Mpiraaa umekwishaaaaaa, Simba wanaondoka kidedea na point tatu.
 
16230137_1302913043098337_1250248293917655040_n.jpg
16230782_1025550360882757_8797161704560525312_n.jpg
 
Back
Top Bottom