Simba na Yanga Vs CCM na Chadema

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Najua wengi watajiuliza kwa nini nisiandike Simba Vs Yanga au CCM Vs Chadema. Nimeandika Simba na Yanga Vs CCM na Chadema kwa makusudi kabisa kujaribu kuoanisha mahusiano ya fani hizi mbili tofauti za siasa na mpira wa miguu kama zinashabihiana.

Wakati nikiwa shule ya msingi mara nyingi kulikuwa na makundi mawili ya mpira kundi la Yanga na kundi la Simba. Vivyo hivyo mitaani kulikuwa na makundi hayo hayo. Maofisini hadi kwenye vijiwe vya kahawa utayakuta hayo makundi. Hadi leo hii ingawa ligi kuu ina timu 12 lakini zinazoongelewa zaidi ni Simba na yanga.

Kuna mwaka fulani (siukumbuki) timu moja kati ya hizo mbili zilizojulikana kama watani wa jadi ilitaka kushuka daraja lakini juhudi za ziada zilifanyika hadi ikabakishwa daraja la kwanza, kisa, sababu mbalimbali zilitolewa, ligi itapooza, mapato yatapungua, kiwango kitashuka utadhani kilikuwa juu nk.

Tanzania bara kuna takribani ya vyama 20 vilivyosajiliwa lakini ukweli usiopingika kwenye miaka ya hivi karibuni ukiondoa CUF iliyo na nguvu Zanzibar ni vyama vya CCM na Chadema ndivyo vinavyotawala midomoni mwa watu iwe mitaani maofisini vyuoni na hata hapa JF.

Hali hii ya DOMINANCE katika siasa ukiachilia mbali mpira wa miguu; je ni kweli kuwa inasaidia kukuza demokrasia au ndiyo inadidimiza. Watu wengi kuzungumzia vyama viwili tu ni dalili ya kuongezeka kwa upeo wa uelewa katika masuala ya siasa au ndio unazidi kupungua kwa kujifunga kwenye mawazo ya wachache na kuacha nje mawazo ya walio wengi.

Naomba tujadili wazo hili la CCM na Chadema ku dominate siasa za Tanzania tukirejea mfano wa timu za Simba na Yanga ku dominate mchezo wa mpira wa miguu kama zinasaidia kuongeza au kudumaza kiwango cha Demokrasia nchini.
 
ccmchademageneralelecti.jpg
 
Back
Top Bottom