Majigambo na ukimya nadhani inatokana mienendo ya usajili mpaka sasa. Ukimya wa Yanga unatokana na mashabiki kuwa na hofu ya kusambaratika timu iliyokuwa tayari inaonesha dira. Tayari benchi la ufundi limeshameguka bado wachezaji muhimu haijulikani hatima yake. Na ukijumlisha kuwa mashabiki walikuwa wameshazoshwa kujiamini kupitia Nabi sasa haijulikani nini kitajili mbeleni. Nyuso za mashabiki wa Yanga zitarudi baada ya kuangalia mechi kadhaa zitakazochezwa ili kujua uwezo wa benchi jipya.
Azam, wanachokifanya sio kigeni, walishafanya hivyo misimu kadhaa nyuma kuleta vyuma lakini ubingwa ni kupokezana kwa timu za Kariakoo, labda wabadiilike hivi sasa.
Simba ndio pekee ambao wanaweza kuwa na matumaini makubwa nyusoni mwao tofauti na Azam kwasababu Simba wanaimarisha kikosi chao. Kikosi cha Simba cha msimu uliopita ilikuwa ni kikosi bora cha wachezaji wanaonza ila mapungufu yalikuwa ni machache sana. Ndio timu iliyokuwa na Ukuta bora + safu bora ya ushambuliaji kwa Tanzania kwa msimu uliopita. Kiungo ndio ilikuwa sehemu kubwa yenye mapungufu. Kwa kuziba hayo mapungufu wanajawa na matumaini ya kufanya vizuri kwa kuzingatia kuwa kocha ni yule yule wa msimu uliopita.