Simba msisikilize kelele za majirani zetu

Betterhalf

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
2,879
2,554
Habari za jioni wanajamvi.
Awali ya yote nimshukuru Muumba kwa kuniwezesha kuiona Jumapili ya leo, na nikaweza kudiriki kuishika kalamu.
Ligi kuu ya VPL imeshika kasi sana kipindi hichi ambapo mzunguko wa 20 unaendelea kwenye viwanja mbalimbali.
Kama ilivyo ada kwa watani wa jadi, kila mmoja amekuwa akimuombea adui yake apate matokeo mabovu.
Hali hii imechochea furaha isiyo kifani kwa mashabiki wa Yanga kufuatia Chama Kubwa "SIMBA SC" kutoka sare mbili na timu za Mwadui na Stand Utd.
Kwa tathmini ya haraka, SIMBA imepoteza pointi NNE kwa mechi NNE dhidi ya timu hizo na imevuna pointi NANE kutokana na michezo ya mzunguko wa kwanza na wa pili dhidi ya timu hizo.
Kwa mwenye ufahamu mkubwa wa mpira kama MZEE Akilimali, bado ataipongeza SIMBA kwa matokeo hayo, lakini kwa wenye ushabiki "mahaba niue", wataendelea kuichachafya na kuikashifu SIMBA.
Rai yangu kwa viongozi, benchi la ufundi,wanachama,wachezaji,mashabiki na wapenzi wa SIMBA SC ni kuwa watulivu na wenye kuangalia yaliyopo mbele yetu kwa kuwa kuna kila dalili ya kulibeba kombe la VPL msimu huu.
Karata zichangwe vizuri kwa kuzipa uzito sawa mechi zote.
Pia, viongozi na msemaji wa timu kuweka akiba ya maneno wakati huu hasa yale yanayohusu siri na mikakati ya ndani inayopangwa na benchi la ufundi katika kuziendea mechi zilizobaki.
Vilevile, kila mtu kwa nafasi yake, atekeleze majukumu yake ili kuiletea SIMBA SC heshima yake hasa wakati huu.
Aidha, porojo na siasa za majirani zetu " noisy neighbours", tusizijibu kwa fujo bali kwa mikakati ya siri kabisa pasipo kupigizana nao kelele.
Zitapigwa propaganda nyingi lakini uelekeo wetu uwe ni wa kuwakimbia kimya kimya.Naiona safari ya ubingwa wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.
Mwisho, nawatakia maandalizi mema kuelekea mchezo wa kimataifa wa CAF Confederation Cup dhidi ya Al-Masry hapo siku ya Jumatano.Ni imani yangu kwamba kila kitu kitaenda vizuri INSHAALLAH.MUNGU ni mwema kwetu na tutafanikiwa kuiwakilisha vyema Tanzania.
MUNGU IBARIKI SIMBA SC, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Alamsiki.
04/03/2018
1748HRS
 
Mzee Akilimali hapendwi kwa ajili ya kuwa mkweli.Sasa hivi anazungumzia kiwango na uwezo wa Youthe Rostand.
 
Kipindi kama hiki Yanga huwa hana masihara! Mjiandae tu kisaikolojia kwani ubingwa mmeshaukosa!
 
vp mbona mlianza kushangilia ubingwa halafu mara mnaanza kutetemeka tena watani?
Hakuna kutetemeka mkuu.Game tano za raundi ya kwanza tulivuna pointi 11 na magoli 14; raundi ya pili game tano tumevuna pointi 11 na magoli 14.
Tofauti ipo kwenye magoli tuliyoruhusu; raundi ya kwanza magoli 3 na raundi ya pili magoli 5.
Bado tuna nguvu mkuu.
 
Back
Top Bottom