Lecheminduroi2
JF-Expert Member
- Jan 7, 2025
- 265
- 668
Hao ni wachawi tu mkuu, ile game kama kuna aliyehongwa basi ni kocha ambaye aliyemuanzisha Manula kutoka majeruhi baadala ya Lakred ambaye ndio alikuwa anafanya vizuri kwa wakati huo. Manula kafanyika kafara ya uongozi mbovu usiowajibika kipindi hicho, kumbuka walimuandama na Chama pia pamoja na Baleke, timu ilivyokuwa inastruggle kupata matokeo wakakubali yaishe kwa Chama na kweli angalau alifufua kidogo tukaanza pata matokeo.Unajua mengi wapi mnafiki tu na roho mbaya kama kawaida ya wabongo, mtu ungekuwa unajua mengi si ungeweka evidence hapa? Kitendo tu cha kuuanzisha huu uzi ni kumsagia kunguni kwa kuonesha alishiriki kweli kwenye rushwa sasa malizia uzi wako kwa kuweka ushahidi sio kuchafua tu mchezaji ili future yake ilipotee mazima. Kupangwa kwa Manula kwenye ile derby ilikuwa ni surprise kwa kila mmoja na pengine hata Yanga hawakutaraji kama angedaka yeye kwasababu Ayoub ndiye aliyekuwa na match fitness na muendelezo mzuri wa kiwango, hivyo kama kufikiria kuhongwa lazima angehongwa ambaye ana asilimia kubwa kucheza mechi tofauti na Manula ambaye hakuwahi kucheza mechi kwa kipindi kirefu sana kutokana na majeraha. Mashabiki wa bongo mnaendeshwa sana na propaganda
Manula anaonewa kwasababu ni mtanzania ila ingekuwa mchezaji wa kigeni sasa hivi Simba ingekuwa kimeumana kule CAS.