Simba mfano wa kuigwa msimu huu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba mfano wa kuigwa msimu huu.

Discussion in 'Sports' started by Kijamani, Nov 16, 2009.

 1. K

  Kijamani Senior Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jana wadau wa soka walishuhudia timu ya Simba ya Dar es Salaam ikimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara ya vodacom kwa ushindi wa asilimia mia moja.Simba ambayo imejikita kileleni mwa msimamo kwa kujikusanyia pointi 33 katika michezo 11 imeonyesha dalili za mafanikio tangu mwanzoni mwa msimu.
  Mafanikio ya Simba yamechagizwa mambo mbalimbali ikiwemo usajili wa wachezaji wenye tija katika timu.Tumeshudia rais wa TFF akitoa sifa kemkem kwa wachezaji wa simba kigeni wa Simba ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye timu sambamba na wenyeji.
  Hii imekuwa tofauti na timu nyingine ambazo zimejaza wachezaji wa kigeni ambao wameshindwa kuzisaidia timu zao.Hakuna budi kwa timu nyingine kuiga mfano mzuri ambao Simba imeuonyesha msimu huu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Simba ndo nini vile...?

  Usinambie wamekula watu huko Tarangire!

  Kinachoniuma mimi habari za POOL haziwekwi hapa...Simba ..simba....Mtibwa...sijui na manininini huko!..aaaaaarrrrghhhhhh!
   
 3. K

  Kijamani Senior Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sikulaumu ndivyo uelewa wako unavyokutuma.Jiandikishe chama cha pool duniani.Soka ndio mchezo unaopendwa na watu wa kada zote duniani tofauti na pool inayopendwa kwa asilimia kubwa na walevi
   
 4. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kijamani

  Umesahau kazi ya Kocha Phiri. Ninyi ndiyo huwa mnawapa wachezaji kichwa mnamsahau kumpatia kocha big up! Wachezaji bila kocha wapi na wapi!.

  Upande mwingine wa shilingi, tunaipongeza timu ya Simba kwa Mshikamano uliozaa matunda mazuri.

  Unayetaka habari za pool anza kuziweka wewe mwenyewe usisubiri watu wengine waziweke hali haujui wanafikiria nini na hobbies zao ni zipi!! Unazungumzia POOL ipi!!!!!!
   
Loading...