Simba kwenye kombe la mapinduzi

Simba kwenye kombe la mapinduzi

photo mee

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
608
Reaction score
93
Tunaombeni matokeo wadau mchezo unaochezwa usiku huu kati ya wekundu wa msimbazi simba na kmkm hapo uwanja wa amani
 
Tunaombeni matokeo wadau mchezo unaochezwa usiku huu kati ya wekundu wa msimbazi simba na kmkm hapo uwanja wa amani

Ni kweli unaandika habari hii hapa au makusudi tu kwamba unajua jukwaa la siasa lakini unaleta fujo ?
 
Simba 2 Chuoni 0
Magoli yamefungwa na Singano Messi.
 
Tunaombeni matokeo wadau mchezo unaochezwa usiku huu kati ya wekundu wa msimbazi simba na kmkm hapo uwanja wa amani

kwa habari na picha nenda Bin Zuberi, tukileta hapa watu wanapata presha
 
Wekundu wa Msimbazi Simba wametinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Chuoni ya Zanzibar kwa mabao 2-0.



Mrundi Amissi Tambwe na kinda Ramadhani Singano ‘Messi' ndiyo waliofanya ‘mauaji' hayo usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.


Simba chini ya Kocha Zravko Logarusic na msaidizi wake Selemani Matola ilionyesha soka la kuvutia na kuwapa wakati mgumu Chuoni.
Pamoja na kuonyesha juhudi lakini wakati fulani, Chuoni walilazimika kuutafuta kwa tochi ili kupambana na makali ya Simba ambao walionekana wako sawa.

TAMBWE, MESSI WAIZAMISHA CHUONI, SIMBA YATINGA NUSU FAINALI MAPINDUZI - SALEH JEMBE
 
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
MABAO mawili ya Ramadhani Yahya Singano ‘Messi' usiku huu yameipeleka Simba SC Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2014 baada ya kuilaza Chuoni ya Unguja 2-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Messi baada ya kufunga bao la kwanza akiruka sarakasi kushangilia na chini ni baada ya kufunga bao la pili

Kwa ushindi huo, Simba SC itamenyana na URA ya Uganda katika Nusu Fainali ya pili keshokutwa Uwanja wa Amaan, Saa 2:00 usiku, baada ya Azam na KCC zitakazomenyana Saa 10:00 jioni.
Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 47 kwa shuti kali baada ya kukutana na krosi ya Issa Rashid ‘Baba Ubaya' kutoka wingi ya kushoto.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Simba wakishangilia bao lao la pili leo Uwanja wa Amaan[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Bao la pili, Messi alifunga dakika ya 59 baada ya kupiga mpira kutokea pembeni kulia na kuwachanganya mabeki wa Chuoni kisha kuzama nyavuni.
Pamoja na kufunga mabao hayo mawili, Messi alicheza kwa kiwango cha juu hii leo na haikushangaza alipotajwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya mchezo huo na kuzawadiwa king'amuzi cha Azam TV.
Chuoni walicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kuibana kabisa Simba SC kupata bao, hali iliyoashiria mchezo huo ungekuwa mgumu zaidi kipindi cha pili.
Lakini mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mcroatia wa Simba Zdravko Logarusic mwanzoni tu mwa kipindi cha pili, kuwatoa viungo wa kati Jonas Mkude aliyekuwa anacheza chini na Ramadhani Chombo ‘Redondo' juu na kuwaingiza Amri Kiemba na Ally Badru, yalibadilisha taswira nzima ya mchezo.
Tangu hapo, Simba SC ilianza kucheza kandanda ya kuwapa raha mashabiki wake kwa kushambulia kwa kasi na haikushangaza ilipopata mabao mawili ndani ya dakika 14 za kipindi cha pili.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Nassor Masoud ‘Chollo' dk66, Issa Rashid ‘Baba Ubaya', Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude/Amri Kiemba dk46, Haruon Chanongo, Ramadhani Chombo ‘Redondo'/Ali Badru dk46, Awadh Juma, Ramadhani Singano ‘Messi'Said Ndemla dk70, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk74.
Chuoni; Ahmed Suleiman, Hussein Rashid/Ramadhani Hamad dk49, Mwinyi Mngwali, Ahmed Salum, Saleh Mohammed, Adam Othman, Shaaban Msafiri, Hamad Makame/Yussuf Mohamed, Amour Kitipwa/Abdulkadir Ibrahim, Ame Amour na Ibrahim Jeba.

SIMBA RAHAAAA, MESSI UTAMUUUU…WAPEMBA MDEBWEDO KWA MNYAMA, WALALA 2-0 AMAAN - BIN ZUBEIRY
 
Safi sana Simba kwa ushindi huu mnono lakini Wavimba macho wamenuna kama nini ni kama ule wimbo unaosema "Narudi kazi haooo wamenuna haoo,narudi kazi haooo wamenuna haoo':first:😛oa
 
another clean sheet. Beki ya Simba iko vizuri sana.
 
Huenda pia safu ya washambulizi kwa timu zote ni butu kama ilivyo ya Simba ambayo jana tu ndiyo imeona lango kati ya mechi nne sasa, so tusibweteke
 
wapange za bongo na uganda ili fainali wachze wabongo na waganda ndio muzuka zaidi..
 
Back
Top Bottom