Simba kujenga ghorofa 12 Msimbazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba kujenga ghorofa 12 Msimbazi

Discussion in 'Sports' started by mdau wetu, Oct 18, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam iko katika mikakati ya kuimarisha vitega uchumi wake, ikiwamo kujenga jengo la ghorofa 12 makao yake makuu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuacha kutembeza bakuli.
  Katika kuelekea mipango hiyo, tayari wamezungumza na benki mbili tofauti zenye nia ya kupanga kwenye jengo hilo ambapo wanatarajia kuziweka hadharani hapo baadaye.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema klabu hiyo kwa sasa ina mikakati mingi ya kujiweka vizuri kiuchumi, ili kuondokana na ukata, pamoja na kuishi katika jengo ambalo haliendani na hadhi ya klabu hiyo kubwa hapa nchini.
  “Katika kufanikisha maendeleo mbalimbali ya klabu, nimeamua kuunda kamati mbalimbali ili klabu kuwa na manufaa na mimi kupunguza majukumu, kwa kuwa sasa nitakuwa na majukumu mawili tu la uwanja pamoja na mikakati ya maendeleo ya klabu,” alisema Rage.
  Alizitaja kamati hizo kuwa ni ya Fedha, Mashindano, Ufundi, Usajili pamoja na Kamati ya Nidhamu.
  Aliwataja wanaounda Kamati ya Fedha ambayo inaongozwa na Geodfrey Nyange ‘Kaburu’, ni Adam Mgoi, Makamu Mwenyekiti; huku wajumbe wakiwa Saidi Pamba, Kifiri, Zitto Kabwe, Juma Pinto, Abdul Mteketa na Murtaza Mangungu; huku Kamati ya Mashindano ikiwa na Joseph Itang’are (Mwenyekiti), Azim Dewji (Makamu Mwenyekiti), Jerry Ambe, Swedy Mkwabi, Hassan Hassanol, Mohamed Nassoro, Amosi Makala, Richard Ndasa na Suleiman Zakazaka (Wajumbe).
  Kamati ya Ufundi ni Ibrahim Masoud (Mwenyekiti), Evans Aveva (Makamu Mwenyekiti), Dan Manembe, Khalid Abeid, Musley Rwekha, Mulamu Ng’hambi, Saidi Tuli, Rodney Chidua na Patrick Rweyemamu (Wajumbe), wakati Kamati ya Usajili wako Zacharia Hans Poppe (Mwenyekiti), Kasimu Dewji (Makamu Mwenyekiti), Francis Waya, Crecensius Magori, Salim Abdallah, Collins Frisch na Gerald Lukumay (Wajumbe).
  Rage aliitaja Kamati ya Nidhamu kuwa ni Mwenyekiti, Peter Swai, huku Makamu Mwenyekiti akiwa Jamal Rwambow na wajumbe wakiwa Charles Kenyera, Evody Mmanda na Chaulembo.
  Wakati huohuo, Rage alisema kuhusu suala la mchezaji wao Kelvin Yondani ambaye anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu, walimpa barua mbili na hakujibu hata moja, hivyo uongozi pamoja na kamati ya ufundi umemtaka aje azungumze nasi kama anataka kuvunja mkataba na wako tayari.
  Alisema kuliko kitendo cha kuongea na vyombo vya habari ni bora aende kuzungumza na uongozi na wao watamruhusu kama atahitaji kuondoka, kuliko kukaa kimya bila ya sababu.
  Aliongeza kuwa kutokana na kosa la Yondani, wangeamua kuchukua hatua kwa kufuata kanuni za FIFA na za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingemwia vigumu mchezaji huyo, kwani mchezaji akiwa na kosa la utovu wa nidhamu, anastahili kufukuzwa na haruhusiwi kwenda kujiunga na klabu yoyote mpaka uongozi wa timu husika aliyokuwa anaichezea ukubaliane na hilo.
   
 2. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Waache longo longo, wawekeze kwenye uwanja kwanza. hi za kujenga uwanja mwaka unaisha sasa hatujui hata kiwanja kipo wapi
   
 3. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi bado hizi clubs (Simba, Yanga) zinapata watu wa kuwongopea? NI wazuri sana kujenga vitega uchumi na kucheza mpira kwenye vyombo vya habari. Rage asiite waaandishi wa habari ila aende chamazi apewe semina elekezi kwenye mambo haya. Ushamuona Bakhresa MAELEZo? unakutana na mambo yake tu. KWA UFUPI HIZO NI POROJO. MUULIZEN RAGE UWANJA WA SHOPPING MALLS UNAZINDULIWA LINI?
   
 4. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  hivi nuyu ndo yule rage wa FAT ?
   
 5. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  aliahidi siku mia moja, kukamilisha jengo la simba na kuhamia.leo hii miakamiwili hata rangi bado kukamilika.poleni sn wadanganyika
   
Loading...