brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,386
Klabu ya Simba Sc yenye makao yake makuu mtaa
wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es salaam
inatarajiwa kufanya maandamano ya amani siku ya
jumanne.
Katika barua iliyoandikwa na Rais wa klabu hiyo
Evans Aveva kwenda kwa Kamishina wa Kanda
Maalum wa jeshi la Polisi mkoa wa Dar es
salaam, Simba watafanya maandamano hayo
kuanzia saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 7
mchana.
Maandamano hayo yataanzia makao makuu ya
klabu ya Simba kuelekea ofisi ya Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Mchezo yakiwa na
ujumbe wa uonevu wanaofanyiwa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Klabu ya Simba imekua na malalamiko mengi
TFF na yamekua hayasikilizwi kwa kipindi kirefu,
lakini pia tumepata taarifa za kuitwa Kamati ya
Maadili msemaji wetu wakiwa na lengo la
kumziba na kumfunga mdomo asiweze kuseme
uonevu huo.