"SIMBA KUBADILISHA JINA NA KUWA "Dar es salaam United Fc"

yohana charles

Senior Member
Mar 21, 2013
134
10
Kufuatia mchakato unaoendelea wa kufanyia marekebisho katiba ya Simba,miongoni mwa mambo yanayosemekana yatafanyiwa marekebisho ni jina la klabu ya Simba sc kuwa Dar es salaam United...je wewe kama mdau wa michezo hususan Simba unaonaje na unasemaje kwa hili?
 
Hivi hawa viongozi wanataka kutuharibia klabu kwa mambo yasiyo na maana!-hawajui kuwa brand-ndo kila kitu kwa timu?!-ni sawa na ni ukweli kuwa uko nyuma timu hii-iliwahi kuitwa Sunderland-lakini hiyo haiwezi kuwa na muda huu.Brand"Simba"ni kubwa mno-itawachukua karne kutake the lead!
 
Hapa hatujadili michezo hebu peleka jukwaa la michezo na burudani.

Kufuatia mchakato unaoendelea wa kufanyia marekebisho katiba ya Simba,miongoni mwa mambo yanayosemekana yatafanyiwa marekebisho ni jina la klabu ya Simba sc kuwa Dar es salaam United...je wewe kama mdau wa michezo hususan Simba unaonaje na unasemaje kwa hili?
 
Watani zangu wanataka kuaribu Brand ya Jina Simba.......haya...
 
Hiyo itakuwa klabu nyingine sio Simba S.C niliyokua nikiifaham. Pamoja na kwamba ilishapitia majina mengine huko nyuma.

Lengo ni nini kupata sapoti yu wana Dar es Salaam kama ilivyo kwa Mbeya City aU?!
 
Kufuatia mchakato unaoendelea wa kufanyia marekebisho katiba ya Simba,miongoni mwa mambo yanayosemekana yatafanyiwa marekebisho ni jina la klabu ya Simba sc kuwa Dar es salaam United...je wewe kama mdau wa michezo hususan Simba unaonaje na unasemaje kwa hili?

...naona jinamizi la kibaguzi linaanza kuwanyemelea! Baadaye itaitwa Kariakoo Unite FC, na baada ya muda itabadilishwa na kuitwa "Barabara / Mtaa wa Msimbazi FC"

"nawashauri wanachama wa SIMBA wa mikoani tafuteni au anzisheni nanyi timu zenu, wanaDAR ES SALAAM wanataka kujimilikisha timu ya SIMBA, nyie wa mikoani hamna chenu, baada ya katiba mpya"
 
Jina zuri ni Msimbazi United. Nitaakikisha ili jina la Msimbazi United linapitishwa. Jina la Simba sio zuri wanachama wenzangu wa Simba SC
 
Wakibadilisha jina itakuwa ndo mwisho wa kushabikia hii timu, itabidi nihamie hata Simiyu United sijui itaanzishwa au nitajitahidi nianzishe hata mwenyewe.
 
Upuuzi tu it doesnt make sense kubadilisha jina kunaisaida vipi simba kimaendeleo na kupata mafanikio??
 
...naona jinamizi la kibaguzi linaanza kuwanyemelea! Baadaye itaitwa Kariakoo Unite FC, na baada ya muda itabadilishwa na kuitwa "Barabara / Mtaa wa Msimbazi FC"

"nawashauri wanachama wa SIMBA wa mikoani tafuteni au anzisheni nanyi timu zenu, wanaDAR ES SALAAM wanataka kujimilikisha timu ya SIMBA, nyie wa mikoani hamna chenu, baada ya katiba mpya"
Kama huko mkoani kwako kuna timu iko ligi kuu ni ujinga kushabikia Simba au Yanga.
 
Back
Top Bottom