Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 303
- 1,158
Zamani ilikuwa ni vigumu kwa Simba kumtema au kumweka mapumzikoni mchezaji tegemeo hata kama hana nidhamu, ilikuwa ikiogopa kuwaudhi wanachama na mashabiki wake kwa sasa hivi mambo hayo hamna.
Kwa namna Morrison alivyokuwa na mchango kwenye timu huku bado tuna safari ya kuusaka ubingwa na bado tuna kombe la ASFC, na bado wachezaji kibao majeruhi lakini uongozi umeona Morrison harekebishiki nidhamu yake, umeona Simba ni kubwa kuliko yeye.
Simba imemuonya vya kutosha Morrison na tukio la juzi la kumjeruhi shabiki wa Yanga ndio limewakera sana viongozi na kuamua kumweka kando, hata kama ni mchezaji mzuri kiasi gani.
Sidhani kama Yanga wanaweza kumuadhibu mchezaji muhimu kipindi hiki na kumwambia apumzike kama walivyofanya Simba.
Kila la heri Morrison.