Simba inaweza kutolewa klabu bingwa leo, Historia ina tabia ya kujirudia.

Mr Alpha

Senior Member
Jul 31, 2018
195
522
Kama umefuatilia mechi za simba karibuni utagundua timu imekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa siku moja barabarani wiki gereji

Timu haina kikosi aggressive chenye uchu wa mabao na muunganiko wa ushindi, timu imekuwa ikipata matokeo ya papatu papatu kulingana na siku

Simba kocha wanae mzuri shida kubwa ipo kwenye wachezaji, ina wachezaji wa kiwango cha chini mno hususan eneo la ushambuliaji likiongozwa na mchoyo na mbinafsi namba moja Saido Ntibazonkiza akisaidiwa na mzee wa makamo Clatous Chama (huyu ameisha kiwango amebaki jina tu japo kolokwinyo wengi hawataki kuamini kabisa)

Leo sitashangaa Jwaneng Galaxy wakipeleka kilio kizito mitaa ya Msimbazi, Jwaneng nao ni kama simba hivyo hii mechi ya leo ni kama mechi dhidi ya pwagu na pwaguzi lolote laweza kutokea leo

Tuwaombee kwakweli
 
Back
Top Bottom