Simba imepewa ndege au imelipiwa nauli?

Simba imepewa ndege au imelipiwa nauli?

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Kuna huu upotoshaji unaoendelea mitandaoni kuhusiana na uamuzi wa Serikali ya Rais Samia kuipa tafu klabu ya Simba katika mechi yake ya pili dhidi ya Stellenbosch huko Durban, South Africa.

Yamezuka maneno kutoka pande fulani zikisema Simba imepewa ndege halafu badala ya kubeba mashabiki wake wanaoipambania kila siku wamebeba watu wengine wasio na mchango wa kila siku katika timu.

Kwanza ninavyojua mimi, Simba haijapewa ndege bali imelipiwa nauli katika shirika la Air Tanzania ikiwa katika safari zake za kawaida kwenda South Africa. Siyo kila aliyekuwa kwenye ile ndege iliyoipeleka timu amelipiwa na Simba au serikali.

Kuhusu hao waandishi wa habari walioambatana na timu, wanaweza kuwa wamekwenda kwa pesa za taasisi zao au wanaweza pia kuwa wamelipiwa na Simba au na mfuko huo huo wa Serikali.

Hapo sioni ubaya wowote maana kuambatana na waandishi wa habari ni jambo muhimu sana katika safari hizi. Iwe ni serikali, taasisi zao za habari au Simba yoyote ambaye amechangia kuwapelewa waandishi wa habari nadhani sio jambo la kushangaza.

Nakumbuka vizuri uto wakati wanashiriki mashindano haya hatua hizi za mwisho, walikuwa wanabeba kila mwandishi wa habari. Inashangaza kwamba huku huku South Africa waliwaleta hao hao waandishi halafu leo wao wenyewe wanawaonea gere na kuwasambazia fitna.

Nimalizie kwa kusema Simba ilipewa ofa ya ndege toka hatua ya robo fainali ila mpaka leo haijaitumia. Kuna sababu mbalimbali ambazo zimechangia hilo kutofanyika mpaka sasa.

Nilisema juzi juzi Simba tuachane kubishana na hawa mashabiki wa vitimu vidogo vidogo ambao timu zao zimefeli msimu huu. Roho zinawauma kwa haya ambayo Simba inafanikisha na hawataacha kusambaza fitna na uzushi ili mashabiki wasahau mazuri ambayo timu yao inayapata.
 
Simba akipewa ndege ndo watoto watapata madawati

Acha tujadili vitu vya msingi, sio kila saa mamipira

No reform no election'
 
Simba akipewa ndege ndo watoto watapata madawati

Acha tujadili vitu vya msingi, sio kila saa mamipira

No reform no election'
Haujalazimishwa uchangie. Unataka tujadili reform kwenye jukwaa la michezo?
 
Ikipewa uto unapiga kimya, ikipewa Simba unang'aka
Hata Yanga akipewa pesa na Rais naona ni ujinga na siasa nyepesi na unafiki

Yanga na Simba hazina shida ya huo msaada, Kuna hospital wamama wanakufa wanajifungia Kwa kukosa vida halafu hizo pesa walizopewa Simba zingeleta Suluhu
 
Hata Yanga akipewa pesa na Rais naona ni ujinga na siasa nyepesi na unafiki

Yanga na Simba hazina shida ya huo msaada, Kuna hospital wamama wanakufa wanajifungia Kwa kukosa vida halafu hizo pesa walizopewa Simba zingeleta Suluhu
Cha msingi uwe unatoa malalamiko hayo pale uto inapopewa misaada hiyo ili tusikuone mnafki
 
Sasa hivi huwezi kusikia zile kelele za Yanga kupendelewa! Na hiyo ndege na malazi wangepewa Yanga, mpaka muda huu kuna watu wangekuwa wamechafukwa kweli kweli.
 
Simba kwenye fainali ya CAF miaka ile walijisafirisha wenyewe kwenda Abijan, Ivory Coast na kurudi kwa gharama zao.

Uto omba omba wao waliomba ndege, kwa kuonewa huruma wakapewa ndege yetu wakasafiri nayo, ikawasibiri siku mbili ipo tu Airport Algeria na kuwarudisha Dar.
 
Simba kwenye fainali ya CAF miaka ile ya walijisafirisha wenyewe kwenda Abijan, Ivory Coast na kurudi kwa gharama zao.

Uto omba omba wao waliomba ndege, kwa kuonewa huruma wakapewa ndege yetu wakasafiri nayo, ikawasibiri siku mbili ipo tu Airport Algeria na kuwarudisha Dar.
Hiko kitu nikikumbuka mpaka leo kinanishangaza sana. Mashabiki wa uto walisafirishwa siku kadhaa kabla ya mechi wakalipiwa usafiri, chakula na malazi kwa kipindi chote na ndege ilikaa inawasubiri na wakashindwa kurudi na kombe.

Viongozi wa Simba hilo wamelikataa kwa kuwa halina tija. Ndiyo maana unaona wanachukua sapoti ya usafiri na malazi kwa wachezaji na ikibidi saaana mashabiki wawili watatu ambao kusema kweli ni kama kulipa fadhila tu kwao kwa jinsi wanavyojitoa ila uwepo wao uwanjani hauleti tofauti yoyote.

Simba imeshinda mechi mbili msimu huu mashindano haya haya ya CAF bila kuwepo mshabiki hata mmoja uwanjani.
 
Back
Top Bottom