Simanjiro kuwa na Hospitali ya Wilaya

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Zaidi ya miaka 20, Wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara, haikuwa na Hospitali ya Wilaya.

Hii iliwapa shida wananchi na kuiomba Serikali kupunguza makali ya maisha yao kwa kuwasogezea Huduma hiyo karibu

Huduma ya afya mbali na kutolewa kwenye vituo vya Afya na Zahanati, wananchi hao wanalazimika kwenda Kilimanjaro na Arusha kusaka huduma hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula alisema, Serikali iliwapa bill 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambao unaendelea

Alisema hatua ya ujenzi iliyofikiwa ni njema kwani ifikapo tar 30 June 2019 hospitali hiyo itakuwa imekamilika..
IMG_0489.JPG
 
Zaidi ya miaka 20, Wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara, haikuwa na Hospitali ya Wilaya.

Hii iliwapa shida wananchi na kuiomba Serikali kupunguza makali ya maisha yao kwa kuwasogezea Huduma hiyo karibu

Huduma ya afya mbali na kutolewa kwenye vituo vya Afya na Zahanati, wananchi hao wanalazimika kwenda Kilimanjaro na Arusha kusaka huduma hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula alisema, Serikali iliwapa bill 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambao unaendelea

Alisema hatua ya ujenzi iliyofikiwa ni njema kwani ifikapo tar 30 June 2019 hospitali hiyo itakuwa imekamilika..View attachment 1117882
Kila la kheri wanasimanjiro!!
 
Inajengwa Wapi? Mirerani au Olekosment ? Wilaya Simanjiro jiografia yake inachanganya, hasa mpaka wake na Wilaya ya Moshi (vijijini), Mwanga na Arumeru. Miinuko milima inafanya baadhi ya maeneo kama vijiji vya Msitu Wa Tembo, Magadini, Kiruani na Majengo kuonekana kama yapo wilaya ya Moshi (vijini), ni vijiji viliuvyoko Moshi chini (TPC). Miundombinu kama barabara katika wilaya hii ni shida. Kiujumla Mkoa Manyara nao Mipaka yake na mikoa jirani ni utata mtupu kama ilivyo mkoa wa Pwani na mikoa jirani nayo. Inabidi huduma zingine zitaendelea kupatikana mikoa jirani kuliko kufika makao makuu ya wilaya/ mkoa
 
Wilaya Ya Simanjiro ndiyo wilaya isiyo na barabara zenye hadhi ya kitafa walau kiwango cha changarawe. Kama ilivyo ngumu kuyafikia makao makuu ya mkoa wake wa Manyara yaliyoko mjini Babati nako kufika makao makuu ya wilaya (olekosment) ni shughuli pevu kutokana na kutokuwepo kwa barabara za kueleweka hasa ukitokea mjini Moshi ukafika TPC. Kuanzia Msitu wa Tembo kuelekea wilayani ni shughuli pevu hasa wakati wa masika. Bora maeneo mengine yaingizwe mkoa wa Kilimanjaro na Arusha. Wananchi wanapata taabu sana kwenda makao makuu ya wilaya na mkoa kutokana na ukosefu wa barabara za kueleweka ikichangiwa na jiografia. Maeneo yaliyoko mashariki mwa miinuko (milima) ya simanjiro yawe mkoa wa Kilimanjaro maana ndiko huduma nyingi wanakopatia huko. Kutoka Kata ya Msitu kwenda Babati inashangaza sana. Inabidi uingie mkoa wa Kilimanjaro uelekee mkoa wa Arusha kisha uingie tena mkoa wa Manyara (babati). Haijulikani walizingatia nini kuugawa mkoa wa Arusha na kuanzisha mkoa wa Manyara na kisha wilaya ya Simanjiro.
 
Back
Top Bottom