Silinde ajifunze ''busara'' za Lijualikali

Silinde ajifunze ''busara'' za Lijualikali

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
24,390
Reaction score
40,287
Wasaalam JF, kwanza niweke wazi mimi ni mmoja ya shabiki wakutupwa wa siasa za Mhe.Silinde. Naonaga ni mstaarabu sana, ana maturity, hakurupuki, sio ''mropokaji'' bila data, hana jazba, anachangia kistaarabu na hana siasa za visasi ndio maana niliona anafaa sana kuwa Mwenyekiti huko mbeleni. Yes, alifaa sana yupo "composed" mno hivyo sina chuki wala ''bias'' na huyu mwamba.

Anyway, kumekuwa na kelele nyingi humu JF kuonyesha Mhe. Silinde na wenzake kuwa wameonewa na kwamba CHADEMA ni madikteta. Well and good!

Lakini lazima tujiulize kama kosa wamefanya watu zaidi ya 15 kwanini wanne tu ndio wafukuzwe ila wengine wapewe nafasi ya kujieleza kamati kuu?

Kiukweli hao wanne wameonyesha ''insubordination'' kubwa sana kwa chama, Mhe Silinde kama katibu wa wabunge anafahamu kuna njia rasmi ndani ya chama za kupinga maagizo au maazimio ya kichama na hyo sio mara ya kwanza.

Lakini kilichoharibu anakaidi maagizo alafu anaenda kudhihaki chama kwenye media. Kwani alishindwa nini kuandika barua kupinga na kuomba marejeo ya maamuzi kwa kamati kuu, alafu sasa akikosa suluhisho ndio aingie bungeni?

Sasa hapa chini Mhe Lijualikali pamoja na ubabe wake wote ila kaonyesha ''maturity''/ukomavu mkubwa sana wa kiakili. Kaepuka huo mtego wa kupinga maelekezo kwenye public ilihali kuna vyombo rasmi ndani ya chama.

​


Kiufupi amegoma kabisa kutoa maoni yake mpaka pale atakapofikisha maelezo yake kwa chama. So hapa utaona wazi kabisa Mhe Silinde alipotoka, hata ukiwa na haki bila kutumia njia sahihi utajiharibia.

Hata Mhe Lwakatare nimesikiliza maelezo yake yote, ila siku anayodai hakuingia bungeni alifanya consultation na wadau wengine wote ila sikusikia ndani ya chama. Hivi Lwakatare na uzoefu wote wa kuwa KUB alishindwa jua balance ya maamuzi ya wabunge na chama? Mkisigana suluhisho mnalipata wapi? Je ni mitandaoni? Alishindwa kuandika barua rasmi kwa chama?

Vijana tujifunze kuweka akiba ya maneno na kutumia njia sahihi kudai haki zetu. Unakuta mtu ndoa yake inashida ila anaropoka kwenye page ya IG utadhani kuna suluhu huko!!

Nafahamu Mhe Mbowe anaweza kuwa na madhaifu mengi ila katika hili tunamlaumu bure tu kma ni udikteta angesomba wote hao hadi Lijualikali.
 
Izo busara jifunze wewe kwanza kabla hujamnyoshea mtu mwingine kidole.
 
Silinde watu walishafika bei siku nyingi. Visafari alivyopewa kwenda kule bunge la Afrika. Kusifiwa na jiwe alipowekwa kwenye kamati ya tanzanite watu tukajua tayari. Zitto naye alilaghaiwa hivi hivi na JK leo haaminiki upinzani.
 
Mkuu niamini mimi huu ndio mwanzo wa mwisho wa Lijualikali na wenzie wote waliopinga kutohudhuria bungeni na kasamehewa na chama.

Hii ni kama mtindo wa Marekani na Saddam Hussein au na Ghadaf. Jamaa hawasamei ila wanakusubiria wakati muafaka, kwanza kuanzia sasa hawata aminika tena ndani ya chama. Utaishi vipi na kushirikiana na watu ambao hawana imani na wewe?

Nimekumbuka clip flani ya audio ya anayedaiwa kuwa Jasusi wa kimarekani, ile clip aliyorusha juzi Mwanaharakati huru aliye tingisha wazee wa CCM.

Alisikika akisema kwa lafudhi ya kikongoman "Mimi asili yetu Africa, nimefanya kazi ya Intelligence nchi kadhaa za Africa na kutuma taarifa kule Marekani, hawa jamaa wanatudharau wanatujua sisi waafrika tuko na akili ya kijinga, tuna zile tabia za kusahau kipumbavu, Muzungu hana ile kitu kusamehe, anasubiri usahau akushughulikie, tuache tabia ya kusahau na hii ujinga ya kusamehe.."

Mara hii tumesha sahau kama kuku, kuna watu walidanganywa kusamehewa ndani ya CHADEMA na baadae wakashughulikiwa wakati muafaka ulipowadia.

Kawaulizeni akina Shonsa, Zitto na Mwigamba au Prof. Kitila, kawaulizeni madiwani walio shughulikiwa na chama baada ya migogoro flani.
 
Mkuu Titicomb kupewa chance ya kusikilizwa na kutimuliwa instantly ipi ni hatua mbaya zaidi?

Mhe. Silinde anacholalamika ni kutosikilizwa na ndio maana nmetoa analysis mpaka hatua ya sasa kwamba changamoto ni kukosa akiba ya maneno.

Hayo ya kushughulikiwa ni mambo mengine, mbona Mhe Mnyika alipinga kabisa kuondoka kwa Dr Slaa na Kuteuliwa Mashinji ila hakuropoka mitandaoni mpaka leo hakuwahi eleza ukimya wake.

Leo hii katibu Mkuu, hata Lissu ni mengi tu anamkosoa Mbowe ila anayamaliza ndani ila hashughulikiwi tu na zaidi kapewa umakamu mwenyekiti.

Unyenyekevu na maturity ndio msingi wa kufika mbali, hata kitabu cha 48 laws of power ile sheria ya kwanza kabisa inasema never outshine the master!!

Insubordination ni kwenda kinyume na hyo sheria kabisa mwishowe ndio unavurugwa kabla hujafika malengo yako.
 
zitto junior,
Mngelikuwa na busara mgelitengeza Islamic brotherhood of Tanzania? Wakina Silinde kutekeleza majukumu yao bungeni na kutumia haki yao ya kimsingi ya kikatiba kujieleza imekuwa kosa!
 
zitto junior,
Uko sawa kabisa, hasa kwa haya - 'hata ukiwa na haki bila kutumia njia sahihi utajiharibia. - "Vijana tujifunze kuweka akiba ya maneno na kutumia njia sahihi kudai haki zetu.'

Rejea kesi za Tundu Lissu uwe mfano mzuri wa kuwapa hao vijana - mdomo wake umemkosesha mengi na amechukiwa na wengi! Na masikini, huenda alikuwa na haki! Lakini anavyo idai hawezi akaipata.
 
tuumegee kidogo, maana kuna ukakasi hapo
Hakuna binadamu hakosi madhaifu mkuu so tukisema Mbowe ni perfect tutakuwa tunakosea.

Ila muhim Strength zake ni kubwa kuliko madhaifu na ndio maana CHADEMA imefika hapa ilipo.
 
Mngelikuwa na busara mgelitengeza Islamic brotherhood of Tanzania? Wakina Silinde kutekeleza majukumu yao bungeni na kutumia haki yao ya kimsingi ya kikatiba kujieleza imekuwa kosa!
Islamic brotherhood ni extremists huwezi linganisha na CHADEMA, hao kina Silinde wangeshapigwa bomu kitambo tu so mfano wako ni irrelevant.

Bungeni hauingii kma mgombea binafsi bali kma chama na ndio maana hta viti vyenu mnakaa kichama hamchanganywi

Hata viti maalum wanapatikana kwa kura za kichama tu sio vingine, na hawakuingizwa na wananchi pale bali chama.

Kiufupi ukiwa mbunge lazima ubalance kati ya chama na bunge. Sasa ukiona hukubaliani na maamuzi ya wenzio kuna platform ndani ya chama kupeleka malalamiko sio kwenda kuropoka kwa public.

Na ndio maana mnavyosema kuna udikteta, hamjiulizi kwanini Kina Jaffar wameachwa tu hawakutumbuliwa ila ni Komu na wenzie?

Hvi udikteta huwa una limitation? Kwamba kosa moja ila unatumia wachache unasamehe wengi?

Sikubaliani na hoja yako mkuu
 
amefuata nyayo za rafiki yenu Membe. #NiguseNinuke. #ChakulaKizurHoteli Isiyojulika.
Membe alikua nje ya mfumo na mapovu yake aliyafikisha ndani ya chama. Ila wao walimtumbua kwa sababu zao wenyewe.

Ila Silinde ni katibu wa wabunge yaani anauwezo wa kuitisha kikao kabisa na kufikisha mada ya huo mpasuko ujadiliwe.

Ssa hafanyi hivyo anaamkia tu kwenye media na bunge hku anakashifu? Kwani angeita kikao angekosa nini? Angeandika barua kutafuta suluhu angekosa nini?

Membe ilikua udikteta wa wazi msilinganishe na huu upuuzi wa huyu Silinde.
 
Yaani waandike barua rasmi kwenda kwenye chama, wakati chama kimewafukuza bila kuwasikiliza? Yaani hukumu imetoka bila mtuhumiwa kujitetea. Huo sio udikteta? Unamfukuza mtu kisa kahudhuria bunge? Alitumwa na wananchi akatalii Dodoma?

Mwenyekiti akumbuke hakuna marefu yasio ncha.. apumzike, chadema so mama yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe alikua nje ya mfumo na mapovu yake aliyafikisha ndani ya chama. Ila wao walimtumbua kwa sababu zao wenyewe.

Ila Silinde ni katibu wa wabunge yaani anauwezo wa kuitisha kikao kabisa na kufikisha mada ya huo mpasuko ujadiliwe.

Ssa hafanyi hivyo anaamkia tu kwenye media na bunge hku anakashifu? Kwani angeita kikao angekosa nini? Angeandika barua kutafuta suluhu angekosa nini?

Membe ilikua udikteta wa wazi msilinganishe na huu upuuzi wa huyu Silinde.
Kuna mengi tusiyoyajua mimi na wewe yanayoendelea ndani ya CDM. Silinde si mkaidi ki-hivyo na anakipenda sana Chama chake. Kama imefikia hatua anatoka hadharan na kuzungumza tujiulize kwa nini? Naamini Silinde ni miongoni mwa wanasiasa wachache wazuri hapa Tanzania.
 
Yaani waandike barua rasmi kwenda kwenye chama, wakati chama kimewafukuza bila kuwasikiliza? Yaani hukumu imetoka bila mtuhumiwa kujitetea... Huo sio udikteta? Unamfukuza mtu kisa kahudhuria bunge? Alitumwa na wananchi akatalii dodoma?

Mwenyekiti akumbuke hakuna marefu yasio ncha.. apumzike, chadema so mama yake

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Kuandika barua kupinga maelekezo ya mwenyekiti na aombe lijadiliwe upya kamati kuu.

2.waliofanya kosa ni 16 ila waliotimuliwa ni 4 tu so huo udikteta ni kutimua wachache na kusamehe wengi?

3.Bungeni unaingia Kwa udhamini wa chama na ndio maana mnakaa kwa mfumo wa chama sio mchanganyiko

4. Hao viti maalum takriban 10 wameingia kwa jimbo gani? Si wamefika pale sababu ya teuzi ya chama sio direct votes za majimboni ssa wanatakiwa wawe submissive kwa chama au wananchi ?

5. Kosa la Silinde na wenzie ni kupinga maelekezo ya chama publicly ilihali kulikua na mfumo mzuri ndani ya chama!!

6. CUF waliwahi fanya hivi kwa wale viti maalum mwisho wa siku spika akabariki ila nashangaa kwa CHADEMA imekua nongwa!! Ni lini Ndugai ametetea wapinzani kubaki bungeni?

Dah silinde brother hukushauriwa vyema
 
Back
Top Bottom