Silinde ajifunze ''busara'' za Lijualikali

Silinde ajifunze ''busara'' za Lijualikali

Kuna mengi tusiyoyajua mimi na wewe yanayoendelea ndani ya CDM. Silinde si mkaidi ki-hivyo na anakipenda sana Chama chake. Kama imefikia hatua anatoka hadharan na kuzungumza tujiulize kwa nini?
Naamini Silinde ni miongoni mwa wanasiasa wachache wazuri hapa Tanzania.
Hapana mkuu ninafahamu mengi sana kuhusu CHADEMA na kuna mazito sana yameshatokea huko nyuma ila kuna watu walivumilia mnoo sio kuja kuropoka.

Mnyika amewahi hadi megewa mpenzi wake rasmi kabisa na kiongozi wake mkubwa ila kesho yake tu baada ya fumanizi alipotezea utadhani hamna kilichotokea!! Na amekua mtiifu mnoo kwa huyo kiongozi mpaka leo.

Huo ukomavu ndio naoongelea, changamoto zipo vyama vyote na kila taasisi duniani muhimu ni uvumilivu na utulivu kabla ya kutafuta suluhu.

Sio kejeli kwa chama kilichokubeba ukiwa huna hata mia mfukoni
 
Islamic brotherhood ni extremists huwezi linganisha na CHADEMA, hao kina Silinde wangeshapigwa bomu kitambo tu so mfano wako ni irrelevant.

Bungeni hauingii kma mgombea binafsi bali kma chama na ndio maana hta viti vyenu mnakaa kichama hamchanganywi

Hata viti maalum wanapatikana kwa kura za kichama tu sio vingine, na hawakuingizwa na wananchi pale bali chama.

Kiufupi ukiwa mbunge lazima ubalance kati ya chama na bunge. Sasa ukiona hukubaliani na maamuzi ya wenzio kuna platform ndani ya chama kupeleka malalamiko sio kwenda kuropoka kwa public.

Na ndio maana mnavyosema kuna udikteta, hamjiulizi kwanini Kina Jaffar wameachwa tu hawakutumbuliwa ila ni Komu na wenzie?

Hvi udikteta huwa una limitation? Kwamba kosa moja ila unatumia wachache unasamehe wengi?

Sikubaliani na hoja yako mkuu
Kwani hujui kuwa jamaa amefanya maamuzi ya kuwakomoa wachache. Wote walikuwa wanakosa la kutotii amri ya mkulu wao. Mambo ya kuongea na media ni kisingizio tu.
 
Kwani hujui kuwa jamaa amefanya maamuzi ya kuwakomoa wachache. Wote walikuwa wanakosa la kutotii amri ya mkulu wao. Mambo ya kuongea na media ni kisingizio tu.
Awakomoe kwa faida ya nani sasa? Unajua gharama waliotumia kushinda jimbo la Momba baada ya kugawanywa kutoka Tunduma? Silinde manusura aporwe jimbo kma sio nguvu ya wanachama. Kumtimua ni kuliweka jimbo rehani.

Lakini message inayotumwa hapo ni kwamba insubordination haiwezi kuwa tolerated popote pale. Na unaweza ona hta Lijualikali kaongea kwa adabu sana.

Ukilea huu upuuzi unajenga precedence mbaya sana, toka zitto atimuliwe kuna nidhamu ilikuwepo maana the message was clear hakuna mkubwa kuliko chama.
 
Mkuu zitto junior,kama kuna mtu ataendelea kubisha kuhusu hoja yako hapo juu,huyo atakuwa na ama ana tatizo la akili,au ni mbishi wa kulipwa.
Kongole na ubarikiwe.
Awakomoe kwa faida ya nani sasa? Unajua gharama waliotumia kushinda jimbo la Momba baada ya kugawanywa kutoka Tunduma? Silinde manusura aporwe jimbo kma sio nguvu ya wanachama. Kumtimua ni kuliweka jimbo rehani.

Lakini message inayotumwa hapo ni kwamba insubordination haiwezi kuwa tolerated popote pale. Na unaweza ona hta Lijualikali kaongea kwa adabu sana.

Ukilea huu upuuzi unajenga precedence mbaya sana, toka zitto atimuliwe kuna nidhamu ilikuwepo maana the message was clear hakuna mkubwa kuliko chama.
 
zitto junior,
Uko sawa kabisa, hasa kwa haya - 'hata ukiwa na haki bila kutumia njia sahihi utajiharibia. - "Vijana tujifunze kuweka akiba ya maneno na kutumia njia sahihi kudai haki zetu.'

Rejea kesi za Tundu Lissu uwe mfano mzuri wa kuwapa hao vijana - mdomo wake umemkosesha mengi na amechukiwa na wengi! Na masikini, huenda alikuwa na haki! Lakini anavyo idai hawezi akaipata.
Yaan hapo lumumba mkimchukia Tundu Lissu ndo una conclude eti wengi tunamchukia kwa taarifa yako Tundu Lissu anapendwa kuliko hata huyo mliomgeuza mungu wenu hapo lumumba
 
Kama huna cha kuchangia kuwa observer tu kma wengine.

JF ya 2009 huwezi kuta comment ya hvi.


Mkuu, JF ya sasa, hakuna KUSHAWISHIANA KWA HOJA. Mtu mwenye msimamo fulani, hata aeleweshwe kwa ujuzi wa kiasi gani, ATAJIFANYA HAKUELEWI ulichosema.

Ukifuatilia karibia wote wanaomuunga mkono Silinde, ni wale siku zote wakitakiacho mabaya chama chake.

Kwa ufupi, hizo adhabu walizopewa, wanastahili. Hivi Wabunge wa CCM, wangekubaliana makubaliano kama hayo, kuna mtu angekiuka?

Sina shaka inakumbukwa msukosuko walioupata wale wabunge wa CCM waliotaka kwenda kumtembelea Mheshimiwa Lema kule gerezani, tofauti na matakwa ya Mwenyekiti wao.

Kwa kifupi, anaponzwa na hayo maneno maneno kwenye vyombo vya habari, pamoja na Bungeni.

Alivyokuwa MJINGA, anadai alipelekwa na WAPIGA KURA huko Bungeni. Kama ingekuwa ni hivyo, JPM bila Chama kutumia nguvu, asingepata nafasi ya kuwa mgombea, bali angekuwa Lowassa, ambaye alikuwa na kundi kubwa lililokuwa linamuunga mkono.
 
Wasaalam JF, kwanza niweke wazi mimi ni mmoja ya shabiki wakutupwa wa siasa za Mhe.Silinde. Naonaga ni mstaarabu sana, ana maturity, hakurupuki, sio ''mropokaji'' bila data, hana jazba, anachangia kistaarabu na hana siasa za visasi ndio maana niliona anafaa sana kuwa Mwenyekiti huko mbeleni. Yes, alifaa sana yupo "composed" mno hivyo sina chuki wala ''bias'' na huyu mwamba.

Anyway, kumekuwa na kelele nyingi humu JF kuonyesha Mhe. Silinde na wenzake kuwa wameonewa na kwamba CHADEMA ni madikteta. Well and good!

Lakini lazima tujiulize kama kosa wamefanya watu zaidi ya 15 kwanini wanne tu ndio wafukuzwe ila wengine wapewe nafasi ya kujieleza kamati kuu?

Kiukweli hao wanne wameonyesha ''insubordination'' kubwa sana kwa chama, Mhe Silinde kama katibu wa wabunge anafahamu kuna njia rasmi ndani ya chama za kupinga maagizo au maazimio ya kichama na hyo sio mara ya kwanza.

Lakini kilichoharibu anakaidi maagizo alafu anaenda kudhihaki chama kwenye media. Kwani alishindwa nini kuandika barua kupinga na kuomba marejeo ya maamuzi kwa kamati kuu, alafu sasa akikosa suluhisho ndio aingie bungeni?

Sasa hapa chini Mhe Lijualikali pamoja na ubabe wake wote ila kaonyesha ''maturity''/ukomavu mkubwa sana wa kiakili. Kaepuka huo mtego wa kupinga maelekezo kwenye public ilihali kuna vyombo rasmi ndani ya chama.

​


Kiufupi amegoma kabisa kutoa maoni yake mpaka pale atakapofikisha maelezo yake kwa chama. So hapa utaona wazi kabisa Mhe Silinde alipotoka, hata ukiwa na haki bila kutumia njia sahihi utajiharibia.

Hata Mhe Lwakatare nimesikiliza maelezo yake yote, ila siku anayodai hakuingia bungeni alifanya consultation na wadau wengine wote ila sikusikia ndani ya chama. Hivi Lwakatare na uzoefu wote wa kuwa KUB alishindwa jua balance ya maamuzi ya wabunge na chama? Mkisigana suluhisho mnalipata wapi? Je ni mitandaoni? Alishindwa kuandika barua rasmi kwa chama?

Vijana tujifunze kuweka akiba ya maneno na kutumia njia sahihi kudai haki zetu. Unakuta mtu ndoa yake inashida ila anaropoka kwenye page ya IG utadhani kuna suluhu huko!!

Nafahamu Mhe Mbowe anaweza kuwa na madhaifu mengi ila katika hili tunamlaumu bure tu kma ni udikteta angesomba wote hao hadi Lijualikali.
Nini maoni yako kwa sasa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom