Silaha bora ya kutungulia Ndege/Makombora S-400 ya Russia

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
S-400 ni silaha bora sana ya Kutungulia ndege duniani na makombora hayo yanatengenezwa na Urusi. Leo Urusi imeyaweka makombora hayo tayari kwa vita katika jiji la Moscow. Nchi ya Syria imepewa makombora hayo hivi majuzi kufuatia mashambulizi ya Marekani kwenye kambi ya jeshi la anga ya nchi hiyo ya Syria. Kombora hilo linauwezo wa kuuangusha ndege yeyote inayoruka katika anga ya Israel, Uturuki na Iraq.

Jeshi la anga la Marekani limeshtushwa sana kwa nchi ya Syria kupewa makombora hayo, unit moja ya kombora hii ni dola milioni 400 za kimarekani na kombora hii inauwezo wa kutungua ndege iliyoko umbali wa kilomita 400 kwa speed kali sana.
Rais Putin wa Urusi ameonyesha amedhamiria kuleta balance of power mashariki ya kati.
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 
Maneno miiiiingi!!!
Wenzao wanafanya kwa vitendo.
F-35 stealth bomber zinafanya mazoezi UK tayari kuungana na madege mengine huko pwani ya korea.

Warusi wakacheze Judo na wachina wakacheze taekwando au kung-fu

Mambo ya kibabe wawaachie wenye mbavu ie USA.
 
Hamna ni uwong mtupu Mrusi anacho fanya ni kuisoma gain media Ili kuwa nae ana Nuclear. Angetungua Tomawack syria tuone tech yake anaficha Nini kwenye uwanja wa show Za kibabe? Kama US na NATO alisambalatisha USSR basi kazi Za NUK za Mrus kiwango chake ni Israel tu. Show za kibabe awachie US
 
Maneno miiiiingi!!!
Wenzao wanafanya kwa vitendo.
F-35 stealth bomber zinafanya mazoezi UK tayari kuungana na madege mengine huko pwani ya korea.

Warusi wakacheze Judo na wachina wakacheze taekwando au kung-fu

Mambo ya kibabe wawaachie wenye mbavu ie USA.
Tatizo lenu nyinyi mnataka kuleta mabishano ya ki Bavicha kwenye hii forum.
Nendeni mkasome kuhusu Cold War kati ya Russia na USA hapo ndipo mtaelewa historia ya dunia hii.
 
Tatizo lenu nyinyi mnataka kuleta mabishano ya ki Bavicha kwenye hii forum.
Nendeni mkasome kuhusu Cold War kati ya Russia na USA hapo ndipo mtaelewa historia ya dunia hii.
Hii sio cold war mkuu, hii ni kitu ingine kabisa.

Kama ni historia hata binadamu alikuwa anatumia mawe kuwindia wanyama!!!!!! Sasa sijui mawe unaweza kuyatamka mbele za viumbe kuwa ni silaha inayoogopewa leo!!!?
 
Sasa haya madude yalikuwa kitambo hapo Syria mbona ile midude ya US haikuzuiliwa.
Kulikuwa na MoU kati ya Urusi na US ya kutoingiliana katika mashambulizi ya Anga na ardhini huko Syria. Baada ya US kushambulia kambi ya jeshi la Syria Urusi imevunja MoU hiyo na kuongeza coverage ya ulizi wa miundombinu yote muhimu ya kijeshi na raia nchini Syria. Sasa subiri uone kama US atajitoa akili na kushambulia Syria.
 
Naomba nimsaidie mleta mada kudadavua kwa kina juu ya S 400 TRIUMF (NATO REPORTING NAME SA-21 GROWLER).
Mnamo mwaka 1945 wakati wa vita kuu ya pili ya dunia,dunia ilishuhudia mapinduzi makubwa sana katika teknolojia ya upande wa vita kwa USA kutengeneza bomu la kipekee kabisa la NYUKLIA ( fat boy and litle boy) na kuyatupa HIROSHIMA NA NAGASAKI( kuna nadharia inasema kuwa maneno hayo mawili yana asili ya lugha ya kikanani ambayo ni miongoni mwa lugha zinazounda kiswahili,lugha hiyo ya kikanani kwa sasa inaongelewa sana na wapare/kipare.kama kuna mtu anayejua kipare anaweza pata maana ya maneno NAGA_SAKI NA HIRO_ SHIMA kwa kipare na moja kwa moja atajua tukio lililotokea huko kuwa lina maana sawa na maneno hayo kwa kipare.Mfano mwingine ni jina la kiongozi wa mapinduzi china MAO ZEDONG,jina hilo linafanana na neno la kipare MAWAAAA_SETONGAAA likiwa na maana ya kuwa mtu asiyeenda kwenye sherehe/asiyependa anasa na inafamika ya kuwa kiongozi huyo uchina hakuwai kunywa pombe au kuhudhuria sherehe zenye lengo la burudani.Mifano ipo mingi ila wacha niludi kwenye mada.)

Sasa kitendo cha USA kumiliki silaha hizo mwaka 1945 kilikuwa cha kimapinduzi sana katika medani ya vita.Miaka tisa baadae USSR chini ya JOSEPH STALIN nayo ilifanikiwa kutengenez bomu lake la kwanza la nyuklia lakini hilo likikuwa linatumia HYDROGEN badala ya URANIUM ( USA). Bomu hilo la USSR lilikuwa na nguvu mara 15 ya bomu la USA.
Hivyo basi mabomuya nyuklia yakawa sio kitu tena kwani nchi nyingi tu zikaanza kutengeneza.

Mnamo mwaka 1979 USSR kwa mara ya kwanza ikabadilisha mfumo wa kivita duniani kwa kutengeneza MFUMO WA ULINZI WA ANGA DHIDI YA MAKOMBOLA.
Mfumo huo ulipewa jina la S 300.Ugunduzi wa mfumo huo ulibadilisha medani ya vita kwa sababu ishu haikuwa kushambulia tu bali kushambulia adui huku ukijikinga na mashanbulio ya adui yako( kushambulia na kujilinda).
USA nao hawakuwa nyuma kwani mnamo mwaka 1981 walifanikiwa kutengeneza mfumo wao wa ULINZI WA ANGA DHIDI YA MAKOMBOLA ambao wakaupa jina ya PATRIOT.
sasa kuanzia miaka hiyo hadi leo, mapinduzi makubwa yameendelea kufanyika katika mifumo hiyo ya ULINZI WA ANGA DHIDI YA MAKOMBOLA.

Kutokana na mada,mfumo unaozungunziwa ni S 400 TRIUMF, ambao nato wameupa aka ya SA 21 GROWLER.
Mfumu umepatikana kama mbadala wa S 300.
Katika mpangilio wa herufi,S ni herufi ya 19.sasa ukichukua 19 +4=23.
Namba 23 huwakilisha idadi ya mambo au tageti ambazo mfumo huu huweza kuzitungua kwa muda mmoja.
Mfumo huu uweza kutungua kitu chochote chenye ukubwa kuanzia saizi ya mkono na kuendelea.

S 400, 400 huwakilisha umbali ambao mfumo huu huweza kutungua kombora la aina yoyote, ambao ni km 400.licha ya kuwa na uwezo wa kutungua kombora ndani ya km 400,mfumo huu pia huweza kugundua kombora katika umbali wa km 600,pia kuua mfumo wa umeme au kuhack makombora hayo ndani ya km 600.
Hivyo basi km 400 ni kwa ajili ya kutungua tu,ila km 600 ni kwa ajili ya kuhack makombora( mfumo huu unatumia teknologia ya HOMING NA WALA SIO RADA)
Mfumo huu pia huweza kufanya kazi kwa km 250 kwa ajili ya makombora ya masafa ya kati na mafupi.
Ifahamike ya kuwa makombora yote nayotumiwa na mfumo huu yana spidi/mwendokasi wa HYPERSONIC ambao ni spidi kubwa zaidi ya SUPERSONIC au SONIC.


Kwa sasa mfumo huu sio bora zaidi kwani WARUSI washatengeneza mfumo mpya wa S 500.
Mfumo huu kwa sasa unatumiwa na CHINA,IRANI na baadhi ya nchi ambao wameuziwa na URUSI.
Licha ya kuwa mfumo huu sio bora zaidi kwa WARUSI,bado ni bora zaidi ya mifumo mingine duniani ya aina hiyo kama PATRIOT WA USA NA IRON DOME WA ISRAEL.

Mfumo huu ushawai kutumika SIRIA.Wakati URUSI walipofunga mfumo huu SIRIA, waliweza kutengeneza NO FLY ZONE katika nchi ya SIRIA na ndo kipindi hiki ambacho USA na washirika wake waliondoka SIRIA.
Mfumo huu ulipofingwa SIRIA, URUSI iliweza kuziweka ISRAEL,UTURUKI,LEBANON,IRAQ,JORDAN na SIRIA yenyewe chini ya himaya yake na hakukuwa na uwezo wa kombora lolote kurushwa kutoka nchi hizo ambalo lisingetunguliwa na URUSI ( ikumbukwe ya kuwa URUSI alifunga mfumo huu baada ya ndege yake kutunguliwa na UTURUKI)
Najua kuna watu watakuja na hoya ya kuwa kama mfumo huo ni bora kwa nini makombora ya USA juzi yametua SIRIA?
Jibu ni kwamba kwa sasa URUSI ishaondoa vifaa vyake vingi pamoja na wanajeshi wengi sana SIRIA kwani anaamini kazi iliyompeleka ishaisha,so hakuna S 400 tena SIRIA.

Mfumo huu pia juzi umefungwa katika mpaka wa URUSI,CHINA NA KOREA KASKAZINI,ili kama itatokea vita basi kusiwe na uwezekano wa baadhi ya makombora kupita anga ya URUSI.
ifahamika ya kuwa kwenye mpaka huo,kuna makazi ya warusi 700 (km 17 kutoka mpakani)
Naambatanisha maelezo ya ziada ili watu waweze kuelewa zaidi kuhusu mpaka wa URUSI, CHINA na KOREA KASKAZINI.



URUSI ni nchi kubwa sana na imeanzia ulaya na kuishia ASIA.katika lugha nyingine naweza sema kuwa ni nchi moja ambayo ndani yake kuna mabara mawili,bala ya ULAYA na ASIA.
Mji wa URUSI ambao huigawa nchi iyo katika mabara hayo mawili ni YEKATERINBURG.
Miongoni mwa miji ya urusi iliyopo bara la ASIA ni VLADIVASTOK,TOMSK,SAHARINSKI YA KUSINI,,KHABAROVSK,YAKUTSK NK, ambayo kwa pamoja huitwa MASHARIKI YA MBALI YA URUSI( far eastern)

Sasa mji wa VLADIVASTOK ndo miongoni mwa miji ambayo ipo mipakani na umepakana na nchi nyingi tu.
Mji huu umepakana JAPAN ( kwa upande wa bahari),CHINA NA KOREA( kwa upande wa ardhi).

d70bd358f66b44eabdf91217272a6b83.jpg


5436ec7c9462170ae5959c44b1faf9c5.jpg


Hivyo basi kwa kuwa mji huu kwa upande wa ardhi umepakana na CHINA na KOREA KASKAZINI,ni wazi kuwa URUSI lazima aweke vifaa vyake vya kisasa katika mpaka huo ili kwamba ikitokea kuna vita kati ya nchi flani na KOREA KASKAZINI basi waweza kujihami na makombora ambayo yatalengwa kwenda upande wa URUSI kwani km 17 kutoka kwenye mpaka wa URUSI na KOREA KASKAZINI kuna makazi ya WARUSI wapatao 700 na kutoka kwenye mpaka mbaka mji wa VLADIVASTOK sio mbali sana.
Kumbuka ya kuwa VLADIVASTOK ni mji wa kijeshi wa urusi na kuna kambia kubwa sana ya
Majeshi ya URUSI, kwa vikosi vya Maji,pia mji huu ni muhimu sana kwa urusi kwani ndo anaotumia katika maswala ya kiulinzi dhidi ya JAPAN,CHINA NA KOREA.

VLADIVASTOK pia ni mji wa siri kwani ulikuwepo URUSI tangu zamani ila haukuwapo kwenye ramani ya nchi hiyo.kwa mara ya kwanza mji huu umeanza kuwekwa kwenye ramani mwaka 1991,so bado ni mji muhimu sana kwa URUSI.

Hivyo basi swala la MRUSI kuweka MITAMBO yake ya kukinga anga dhidi ya shambulio lolote( AIR DEFENCE MISSILE SYSTEM) halimaanishi kuwa yupo upande wa KOREA KASKAZINI bali ni kujilinda tu.
Nawasilisha.
 
Sasa haya madude yalikuwa kitambo hapo Syria mbona ile midude ya US haikuzuiliwa.
yapo kwenye kambi ya Jeshi la Urusi tu.

Halafu tambua kwamba Mfano Tanzania ikinunua S-400 Moja na ikawekwa Dar si kwamba adui atashindwa kushambulia mbeya au Arusha au Mara.
 
Hamna ni uwong mtupu Mrusi anacho fanya ni kuisoma gain media Ili kuwa nae ana Nuclear. Angetungua Tomawack syria tuone tech yake anaficha Nini kwenye uwanja wa show Za kibabe? Kama US na NATO alisambalatisha USSR basi kazi Za NUK za Mrus kiwango chake ni Israel tu. Show za kibabe awachie US
We mjinga kweli unajua kwa jiji la Mosscow pekee kuna S-400 ngapi?
Na syria S- 400 ilo wapi ana ina cover wapi? hilo ndo unatakiwa kulijua
 
Kuna Watu Wanauliza km S-300,S-400 na Pantisir air defence zipo Siria iweje US aliipiga Kambi ya Jeshi la Syria kwa Tomhwak missiles.....Ebu Tujiulize US Tomhawk missiles zilizo rushwa Syria zilikua 59 lakini Only 23 landed in Syria hizo nyingine 36 zilienda wapi nadhan jibu unalo! Hakuna Shaka kwa Sasa S-400 Triumph haina mpinzani japo Israel ana Arrow 3 System, US ana Agies na Patriot system,Iran ndo ana test Bavar System japo Sayad 2 is operational.....ChiNa ana HK system ambazo zinatumia analogy ya S-300 za Russia na Kuna joint project ya France/Italy nao wana system zao.....So S-500 Sijui itakuaje
 
Back
Top Bottom