Kama na wewe ulikuwa hujui, ngoja nikujuze!
Katika kumsindikiza rafiki yangu mgeni; mfanya biashara toka Dubai, Ambaye anataka kuweka duka moja la vifaa na simu kariakoo; Tulibahatika kupita sehemu kadhaa tukitafta fremu kupitia kwa madalali, Fremu za biashara ziko juu sana hadi ($3000-$6000) kwa mwezi na lazima malipo huwa ni kwa mwaka au miezi sita, na wenye nyumba/majengo wanapangisha kwa kuringa vibaya!
Na kuna baadhi ya mmiliki mmoja jirani ambaye tayari yeye anabiashara pale alisema hizo bei huwa zinapanda kila mara na pengine watu wengine hufanya fitina kwa wenzao ili wafukuzwe; Cha ajabu baadhi ya wamiliki hata kama hakudai ikitokea katikati akiomba umkopeshe pesa ni sharti umpatie vinginevyo utakuwa hatarini kutokupangishwa tena mkataba wako unapoisha.
Kusema ukweli hatukufanikiwa ikabidi tughairi tukatafte sehemu nyingine mbali na kariakoo, maana gharama ni kubwa sana halafu isitoshe Biashara ya simu ni ngumu sana kariakoo kwa mujibu wa maelezo ya wenyeji kwa kuwa fremu nyingi sasa wengi zinawashinda wanazirudisha.
Kwa akili yangu mwenzenu mwanzo nilijuwa labda ni Tsh milion moja na nusu kwa mwezi, au milion ama laki nane kwa mwezi, kumbe hizo ni bei za mwezi mmoja tu ndani ya fremu husika.