IFAC
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 3,641
- 9,217
- Thread starter
- #141
Aibu naona MimiAcha uongo!
Umeandika pumba.
Mpanda na Kaliua ni wilaya mbili tofauti zinajitegemea.
Ni sawa na mtu aseme "niliikuta Kinondoni Mkwajuni wilaya ya Tabata"
Hivi hii Tanzania unaijua kweli?
Umetembea? au umezaliwa kijinini kwenu, umeisoma hapo hapo na unatarajia ufe na uzikwe hapo hapo!
Mpanda Mlowoka ni Kijiji kilichopo karibia na Msitu wa hifadhi wa Usawima uliopo wilaya ya kaliua.
Ukiwa kwenye hicho Kijiji mto Maragasi unauona kwa kupanda mlima unaitwa Mawasiliano na ili upate Mawasiliano ya simu lazima upande huo mlima.
Idadi kubwa ya wakazi wake ni wafugaji, wakulima wa bange na wahalifu wa kutumia siraha, majangili na kila mtu wa hovyo.
Jinsi ya kufika huko unapitia njia kubwa ya gari ya kwenda Ulyankulu ambayo zamani ilikuwa Kambi ya wakimbizi wa Kirundi.
Ukifika njia panda ya Kijiji Cha Miti mirefu nenda Miti mirefu Center nyoosha na hiyo njia kwenda Mpanda Mlowoka.
Mpanda Mlowoka ni Kijiji na Mpanda ni makao makuu ya Mkoa wa Katavi.
Jifunze kabla hujabisha mtandaoni.