Sikudhani JF ina wanawake 'wakali' hivi

TheSpam

Senior Member
Aug 15, 2019
180
257
Ilikua miaka ya 2015 kama sikosei hivi, niliamua kujitosa JF baada yakuchoka kutumia social networks za mbelembele ambazo wabongo wengi hawazijui. Networks kama mocospace, mopilot na zinginezo zilivuma sana tokea miaka ya 2005 hivi kuendelea.

Enzi hizo tupo sekondari lakini wajanja kama sisi tulikuwa tunauwezo wakumiliki simu nzuri kuliko anayomiliki headmaster wa shule. Na kwa sisi tulosoma maisha ya boarding basi unakuwa maarufu shule nzima. Walimu wenyewe wataanza vipi kukufukuza kisa kukukuta na simu!?

Basi miaka ya 2015 nilipoanza kabisa kutumia JF hasa jukwaa hili la malavidafi. Mtu mzima na ugeni wangu jukwaani nikaanza na mbinu zangu niweze kujaribu kuona kama kweli JF ina watu wa maana! au ni loosers tu walioshindwa ku-face reality katika maisha ya kawaida huko mtaani au la!? maana mimi kwa kuwa ninajijua ni classic hivyo sikutaka kuamini kuwa watu hasa mademu wa JF sio loosers kutakuwa na ambao wako classic kama mimi.

Basi ikatokea nikaanzisha maongezi inbobo ( PM) na manzi moja hivi Id yake siikumbuki, ila kwa bahati ikawa kama wote tunatoka kaskazini ingawa alikua anasoma chuo Dar. Ikumbukwe na mimi kipindi hicho nilikuwa nimetoka chuo kwa elimu ya ziada huko Glasgow. Basi bi dada ikatokea tunachat wee kama mwezi kisha tukaamia kwenye mawasiliano ya simu nk.

Yaani nilimuweka mtoto sawa kiasi akawa kama ameshanizoea kama tumeonana vile na mimi nikawa kama naona ni manzi ninayemjua. Simu za hapa na pale kwa siku. Jokes nk. Ikafika kipindi mpaka tunatumia miamala kwa njia ya simu yeye yuko Chuo Dar mimi niko mikoani Kaskaziniiii!.

Basi Bana! Bi dada akanitumia picha zake. Aloo sikuamini kama kuna watoto au mtoto mtamu mzuri na laini kama huyo ndani ya JF. Kwanza nilimkatalia nikamwambia umetumia picha za uongo. Basi alisisitiza ni yeye na siku tunaonana si nitamuona tu. Atleast hiyo ikanipa moyo ila uzuri wake ulinitisha maana hiyo sura baba...macho woooii na hiyo figure sio ya nchi hii.

Kijana nikajipa moyo. Siku zikayoyoma miezi kadhaa mara ikawa siku kanipigia kaniambia anataka kunisuprise! Duh mimi huwa sipendi suprise ila kwa kuwa mtoto wa JF alisema na kwa kiwango chake sikuweza kumkatalia. Nikasema no sweat nisuprise. Akaniambia niko hapa A town njoo tukutane eneo flani. Aloo kichwa iliwaka moto nikaenda mezani faster kuchukua ufunguo wa gari huku nimevaa pensi tu na tshirt nyepesi chini ndala. Maana ilikua ni jumamosi na nimechili ndani na mimi hujiweka simple watu huwa wananiita mzungu mweusi maana tabia zangu kama za hao jamaa wa ulimwengu wa kwanza.

Nikawasha ndinga huku geti ikifunguliwa na gateman fasta mpaka eneo la tukio. Ikumbukwe mimi nilimdanganya nimevaa jeans blue na shirt nyeupe ndo atanitambua hivo maana nilitaka mimi ndo niwe wa kwanza kumtambua na kumfanyia tathmini. Nikafika huku nimekaa kwenye gari tinted nilichukua ka sport car mana lingine kubwa lilikua linaoshwa. Nikamuona mtoto.

Aisee mtoto alikua 100% yeye yeye kama picha alizokua ananitumia. Yaani alikua ametupia nyuzi na pamba za viwango vya juu. Watu waliokuwa around that place macho yote kwa mtoto. Nikasema doh JF kumbe mambo ni real hivi..kifaa kama hiki ni bahati. Basi nikajitathmini mimi badala ya yeye sasa je atanikubali maana ndo mara ya kwanza ataniona.

Mentali nikajipa moyo nikasema kwani shi ngap huku nashuka nikaenda moja kwa moja aliposimama nikamshika bega nikamtaja jina nanii!!? akageuka oh ndo wewe nanii!? huku anatabasamu!. Nikamjibu ndio mimi huku nampa kumbato matata nikamalizia welcome and it is so nice to meet you. Akajibu pleasure is mine!.

Basi ikawa nimepata kibali kwa bi dada, alionekana kunielewa na kunikubali sana. Ofcourse sishangai maana itamchukua kazi sana mwanamke yeyote kunikataa! Sikataliki kirahisi labda mwanamke awe na mahusiano na mtu na si sababu ingine. Yaani alikua anacheka nakufurahi sana maana kama nilivosema awali tulishazoeana sana kwa simu. Kwa jinsi mtoto alivyokuwa classic sikuamini kama nilomvua kutoka JF ..

Mapenzi yetu yalichipukia hapo na kudumu kwa miaka miwili na hivi mpaka niliposafiri kwenda ughaibuni ikumbukwe nilifika mpaka kwao kujitambulisha nasikitika tu sikuweza kufikia kutimiza ahadi ya ndoa. Zaidi niwaambie mabaharia kama ilivo waweza kutana na mtu popote pale huku duniani iwe barabarani..mtoto wa kitaani geti la jirani, kanisani au shuleni chuo nk hata jukwaa hili la malavidafi unaweza ng'oa mashine balaa nakuweka ndani kabisa.
 
Hahaha anaza kiduku Lilo, ila mzee kama umekutana na visu ni wewe lakini kuna specie mbovu humu halafu zinajipa majina ya instagram,ukiona cute..... ujue hamna kitu hapo.
hakika ..ni kweli usemalo...kuna sampuli mbovu ila sijawahi kutana nazo..hii ni true story mm huwa situngi...JF kuna mapisi ila uwe makini kuchagua
 
Jamani mimi sio Kidukulilo! Mimi naandika real life stories na experience katika maisha ya kwangu pekee. Kweli 100%. Ndo maana nyuzi zangu zote ni za hali juu na kiwango.
 
Tayari nimeshazama PM 20 hivi nasubiri response... Nami nipate kisu cha kumenyea mihogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom