Sikubaliani na dr.slaa ktk hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikubaliani na dr.slaa ktk hili!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jile79, Apr 27, 2011.

 1. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  Akihojiwa na ch.10 jana usiku dr.slaa aliulizwa na kujibu kwa ufasaha mambo mengi sana mpaka mwongozaji(makwaiya) akamsifia sana na kumuuliza iwapo yeye(dr.slaa) anafanya sana utafiti kwa jinsi alivyo makini ktk kujibu kwa ufasaha maswali ya mtego.
  Ninapotaka kutofautiana na Mh.Dr.Slaa ni pale alioulizwa kwa pamoja kuhusu chadema kuwa chama cha kikanda/ukabila/udini......kuhusu udini dr.slaaa alieleza sana lakini ktk hitimisho alisema "chadema wameona Waislamu wanamadai mengi ambayo wameyakosa kutokana na historia hivyo chadema watajitahidi kuyatatua...."Sio siri mimi ni chadema piwa na mtu ninayemkubali sana dr. wa ukweli lakini kauli hii ilinikera sana kwa sababu kwa kauli hiyo chadema watataka kuijiingiza ktk matatizo ya kidini km ccm na cuf wanavyowadanganya waislamu kuyatatua matatizo yao ya kidini badala ya kuwaachia waislamu wenyewe na dini yao
  -chadema wajue ni chama cha watz wote kwani wametetea maslahi ya watz wote kwa vitendo na tusingependa kuenda nje ya maslahi hayo muhimu na hii imekijengea chama hadhi hii iliyopo sasa
  -wawaachie ccm na ccm-b kuhusu mambo ya dini kuhusu kuwatetea watu wa dini fulani,sisi tunataka tuone namna gani mtalikomboa taifa hili kutoka ktk lindi la umasikini uliokithiri na wa kujitakia
  -chadema wametaja list of shame bila kujali uislamu/ukristo na katika list zote wakristo ndio wanatajwa zaidi km cdm ingekuwa na udini kamwe isingethubutu kuwataja ndugu zao

  OMBI: epukeni propaganda za ccm na mafisadi na maswali na mtego ambayo yatakuwazimisha mjibu ili kufurahisha kikundi/vikundi fulani kwani mtaharibu taswira ya chama mbele ya jamii.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi nafikiri yupo sawa, kutatua matatizo yanayo ikabili jamii wakiwa kama kikundi iwe kikundi chakijamii au kidini itakuwa ni vem a na ndiyo sifa ya kuwa kiongozi kuliko kukaa kimya huku ukijua matatizo yao,
  Kama unakumbuka awamu ya Mwinyi kulikuwa vugu vugu kubwa la waislam kudai mambo mbalimbali alichokifanya Mzee Mwinyi aliunda tume iliyoshirika watu wa dini na wanasiasa pamoja na taasisi za serikali tunakumbuka mapendekezo yaliletwa na tume hiyo ilisaidia sana kipindi chake cha utawala mpaka alipoingia huyu jamaa wa magamba na kuleta chokochoko za kidini kama mtaji wao.
   
 3. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe Jile,

  Mkutano wa Tabora Prof Safari hotuba yake ilikuwa imejaa mambo ya kidini na propaganda zile zile. Prof anadai waislamu wameonewa sana na ccm hivo anawataka wajiunge CDM kitakachowapa haki zao na kuwaondolea matatizo yao. Nilimshangaa Prof huyu make WaTZ wenye matatizo si waislamu tu ni wote. Ni vema kujiepusha na hii mitego, waislamu wanatumia sana janja hii ya kulalamika ili kujenga mazingira ya kupendelewa.
  Msisitizo iwe ni kuwakomboa waTZ na kuwatendea haki wote na si kidini.
  Mungu ibariki TZ isiingiliwe na udini.
   
 4. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa upo sahihi na anaonyesha ni jinsi gani anatupenda! Waislamu wanaonekana kupinga mambo ya CHADEMA na kusema yanatetea wakristo peke yao! Wakati chadema ni chama cha wote! Waislam wanaendesha kampen mbalimbali kukipinga chama hiki wakidai kinatetea wakristo peke yao na kuacha waislam nyuma, na wakristo kuwa mbele! Kwa hiyo Dr slaa anatumia busara kusema anayafanyia kazi malalamiko hayo na kuyaweka sawa ili chadema kionekane ni chama cha WATANZANIA WOTE na si wakristo peke yao.. Kwahiyo mwache afanye kazi yake mkuu.
   
 5. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa yupo sahihi na anaonyesha ni jinsi gani anatupenda! Waislamu wanaonekana kupinga mambo ya CHADEMA na kusema yanatetea wakristo peke yao! Wakati chadema ni chama cha wote! Waislam wanaendesha kampen mbalimbali kukipinga chama hiki wakidai kinatetea wakristo peke yao na kuacha waislam nyuma, na wakristo kuwa mbele! Kwa hiyo Dr slaa anatumia busara kusema anayafanyia kazi malalamiko hayo na kuyaweka sawa ili chadema kionekane ni chama cha WATANZANIA WOTE na si wakristo peke yao.. Kwahiyo mwache afanye kazi yake mkuu.
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Naungana Mkono na wewe, sura iwe matatizo ya watanzania na si dini fulani! Kwani sidhani kama kuna mtu au watu walizuiwa kusoma, kufanya kazi au biashara kwa kuwa wanaabudu katika dini fulani! Ni hatari kuanza kutoa upendeleo kwa watu ambao kwa mapenzi yao waliamua kufuata au kutofuata mfumo fulani; au dini fulani kutilia mkazo swala fulani na kudharau swala lingine!

  CDM ingeachana na 'udini' na kushughulikia matatizo ya watanzania kwa ujumla wake! Tujifunze kwa wengine!
  Waislamu walikazania ilimu ahera na kwa mtazamo wangu ndio maana wana msimamo thabiti yanapokuja maswala ya imani yao!

  Kwa upande mwingine wakristu walijikita katika elimu dunia na ndio maana hawana misimamo kwenye imani yao; sioni kama wakristu wanatafuta mtu wa kumlaumu kwa utengano wao (no of madhehebu as kielelezo cha utengano wao)!

  Vivyo hivyo; waislam hawana haki ya kulaumu serikali, kwa chaguo lao la kujali ilimu akhera!
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  ni mahali gani na wakati gani chadema wamependelea wakristo mpaka kujitosa kwenye mitego ya mafisadi na ccm na cuf ya kujihusisha na udinibadala ya maisha ya watz....................

   
Loading...