Sikuamini kama ni yeye………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikuamini kama ni yeye………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jun 28, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Alikuwa ni zaidi ya mama..........

  Sikumbuki umri wangu kamili wakati ule, lakini bila shaka nilikuwa na umri wa miaka kama sita hivi.
  Nakumbuka sisi nyumbani tulikuwa miongoni mwa familia za awali kupata simu nyumbani pale Tabora. Hata hivyo, nilikuwa tu nasikiliza baba au mama akizungumza na simu, kwani ilikuwa ikikaa juu kwenye meza fulani ndefu. Hata hivyo siku moja wakati nikicheza na nyundo, nilijigonga kidole na kuumia. Kwa sababu nilikuwa peke yangu, nilianza kulia kwa maumivu. Lakini, wazo lilinijia ambapo nilikumbuka kuhusu simu.

  Baba au mama, mara zote walipokuwa wakitaka kupiga simu, nilikuwa nikiwasikia wakisema, ‘opereta tafadhali.' Halafu baada ya hapo, wangeuliza au kuomba jambo, ikiwemo kusaidiwa wazungumze na watu fulani.
  Nilitafuta stuli na kupanda juu yake. Halafu niliinua simu na kusema, ‘opereta tafadhali.' Upande wa pili wa simu ulijibu, ilikuwa ni sauti ndogo ya kike. ‘Ehe nikusaidie nini mwanangu?' Nilianza kulia, labda kwa sababu, sasa nilisikia sauti ya mtu, yaani niliamua kudeka.

  ‘Nimeumia kwa nyundo, nataka mama aje.' Ile sauti ya upande wa pili iliniuliza, ‘unatoka damu?' nilijibu, ‘sitoki damu ila nimeumia,' Ile sauti ambayo wakati huo sikuwa najua kwamba ni ya operetta ilijibu. ‘kama kuna friji nyumbani, chukua barafu halafu weka kwenye kidole chako, kitapoa tu wala usilie.' Nilirudisha mkono wa simu na kufanya hivyo.
  Nilikuwa naijua vizuri friji kuliko simu, hivyo sikupata shida. Nilipata nafuu na kujiambia, ‘kumbe hawa maopereta wanajua vitu vingi.' Kwa hiyo mara kwa mara sasa wazazi wanapokuwa hawapo nyumbani, nikawa nainua mkono wa simu na kumwita opereta, ambapo nilikuwa naongea naye mambo mengi sana. Nilikuwa namuuliza maswali mbalimbali naye akawa anajibu.

  Basi tukazoeana angalau kwa sauti tu, bila kujuana.
  Nakumbuka kuna wakati kasuku wa jirani yetu mmoja mwarabu alikufa. Alikuwa ni kasuku ambaye tulimpenda sana. Alikuwa akijua kuiga sauti hata kuimba. Nilipojua kwamba, kasuku amekufa, niliinua simu na kumwambia opereta juu ya kifo cha kasuku yule. Opereta alisema, ‘kuna dunia nyingine ambapo watu huenda na kuendelea kuimba.' Nililipenda jibu lake, kwani lilinipa moyo kwamba, kasuku ataendela kuimba huko alikoenda.Nakumbuka nikiwa darasa la pili, siku moja nilimuuliza opereta maana ya ‘kabwela' Aliniambia kabwela ni mtu anayeamka akiwa hajui atakavyolala. Lakini usiku ukifika hulala. Sikulielewa vizuri jibu lake lakini nililipenda. Wakati huu nilishajua jina la operetta kuwa ni Marry na mimi alishajua jina langu, ingawa tulikuwa hatujawahi kuonana..Wakati huohuo nikiwa la pili, baba alipata uhamisho kwenda mkoani Tanga.

  Nilijua zikiwa zimebaki siku tatu tu kuondoka. Kwa kule kubabaika labda, nilisahau kumwita operetana kumwambia kuhusu kuhama.
  Usikuwa kuamkia siku ya safari ndipo nikakumbuka kuhusu opereta wangu. Kwa kuwa wazazi walikuwepo nyumbani nisingeweza kupiga simu. Niliamua kuchukua picha yangu ambayo nilipigwa shuleni na kuiweka kwenye bahasha. Juu ya bahasha niliandika opereta Marry. Kabla hatujaondoka nilikwenda nyumbani kwa rafiki yangu mmoja tuliyekuwa tukisoma naye darasa moja .Nilipofika nilimkabidhi ile bahasha na kumwomba ampe mama yake aipeleke kwa opereta. Tuliondoka Tabora nikiwa sijui kama operetta yule alipewa bahasha ile au hapana.Siku zikapita na nilisoma na kumaliza kidato cha nne ambapo nilipata kazi au ajira ya moja kwa moja {direct employment} kwenye shirika la reli {TRC} nilipangiwa Tabora kama kituo changu cha awali cha kazi.

  Kwa kweli hali haikuwa nzuri kwa sababu ajira ya moja kwa moja haikuwa nzuri kimaslahi hata kiheshima. Kwa vile pia ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuwa nje ya nyumbani, nilihuzunika sana.
  Wiki ya pili tu tangu kufika Tabora, nikawa ninataka kupiga simu kwa baba {mama alishafariki}, baada ya kuinua simu nilimuomba opereta. Ajabu ni kwamba, sauti ile niliyoisikia masikioni nilihisi kama sauti niliyowahi kuisikia miaka mingi iliyopita haikuwa ni ngeni kwangu. Kwanza sikuelewa hasa ni kitu gani, lakini baada ya muda nikakumbuka.‘Nini maana ya Kabwela' nilijikuta nauliza.

  ‘Kama hujaumiza kidole chako kwa nyundo na kasuku wa jirani hajafa , usiniambie uko Tabora,' ..........nilijihisi nikitetemeka. ‘Mama Marry' niliita nikiwa kama naota. ‘Ni wewe mwanangu Hussein……' yule opereta alisema. Ilinichukua muda kujibu.
  Sina haja ya kusema mengi sana, kwani yule mama alinielekeza kwake baada ya kumjulisha kwamba nilikuwa nimepangiwa kazi pale Tabora. Jioni ya siku ile nilikwenda kwake. Kwa mara ya kwanza nilimwona Marry. Hakuwa mtu mzima sana ingawa alionekana kuwa umri umeenda. Lakini kilichonishangaza ni kuona picha yangu ile niliyomtumia ikiwa kwenye fremu nzuri pale ukutani.

  Yeye ndiye aliyeniambia kwamba ilikuwa ni picha yangu, vingenevyo nisingeikumbuka. Lakini kwa nini aliiweka pale. Katika mazungumzo aliniambia kwamba hakuwahi kuwa na mtoto maishani mwake na hivyo kule kumsumbua kwangu kwa maswali kulikuwa kukimpa furaha na faraja sana. Alikuwa akijihisi kama vile nilikuwa mwanaye na alikuwa akifurahia sana hali ile. Kuondoka na kumwachia ile picha, anasema kwamba kulimfanya ahisi kwamba kapoteza mtoto, yaani kafa, hivyo akaamua kuiweka picha yangu kama kumbukumbu.

  Lakini ukweli ni kwamba, mama yule alikuwa amenivutia sana kwa namna alivyokuwa akijibu maswali yangu na kuvumilia usumbufu wangu. Mama yangu mzazi hakuwa na uwezo ule na wala hakuwa nyumbani muda mwingi. Kwa hiyo akawa zaidi ya mama yangu kwa sauti tu. Nilimpa picha yangu kama zawadi pekee ambayo ningeweza kumpa. Nilihamia pale nyumbani kwake nikawa nimepata mama mpya, naye akawa amepata mtoto. Niliamini na bado naamini kwamba, usije ukadhani lolote unalomtendea mtu ni dogo. Liwe ni zuri au baya, lolote unalomtendea mtu, jua linamgusa kwa njia ambayo wewe hujui.

  Kumgusa kwake huja kujirudia moja kwa moja au kupitia njia nyingine na ni lazima litakuumiza au kukusaidia, inategemea tu ulitenda nini. Leo hii hanidanganyi mtu kuhusu wema au ubaya tunaotenda unavyokuja kuturudia katika mazingira ambapo tunakuwa hatujui kabisa. Lakini, nimejifunza maana ya kuwavumilia wengine.
   
 2. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Hata mie nimejifunza kitu kwenye hadithi hii, asante!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Purple hii siyo hadithi bana, ni mkasa wa kweli........................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,032
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi hivi visa umevihifadhi wapi jamani? Ni zao tena la Jitambue? Kweli Munga Tehenan alikuwa kiboko. Namkumbuka sana katika gazeti la majira "Mzee wa nepi" Gazeti la Dunia na mwisho JItambue & Mshauri. Kama ulikuwa mdau hebu yarudisheni magezeti hayo.

  Kongosho
  Zinduna, gfsonwin FirstLady, MwanajamiiOne na wakinamama wengine wa JF mmeona umuhimu wa kukaa na watoto wenu na kuongea nao kwa upendo? Ni muhimu sana katika makuzi ya watoto.

  Bazazi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi asante sana kwa kisa hiki
  Kweli inapaswa kukaa na watoto karibu na kujua hisia zao na nini wanachohitaji
  Ni fundisho zuri sana mkuu
  Asante sana
   
 6. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  leo nimejifunza kitu hapa, sie ndo akina mama kila tunaporudi majumbani watoto wamelala
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mzee Mtambuzi barikiwa zawadi yako inakija by DHL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Kongosho muda wote yupo na konyagi watoto anaongea nao saa ngapi, Zinduna yuko bize na Talk show, FirstLady anaponya majeraha ya rafiki yake muda anautoa wapi kukaa na watoto, MwanajamiiOne yeye mawazo ya kuumizwa bado yanamsumbua muda haha, gfsonwin mmmh naogopa kusema.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Kisa kizuri sana, nimemkumbuka mama yangu (R.I.P) Alitupenda sana.....Nakumbuka katika zile nyakati baba hana kazi alivyokuwa anapanga bajeti sijapata kuona hata katika wizara zetu. Mpole japo mboko zake nilikula, baadaye anakubembeleza kula. Kwake watoto wake lilikuwa ni chaguo la kwanza.

  Nakukumbuka sana mama.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,985
  Likes Received: 1,909
  Trophy Points: 280
  Bazazi kaka yangu wa moyoni unalolisema ni kweli kabisa aisee. na hata Mtambuzi anatukumbusha mambo muhimu sana katika maisha yetu ya kila sku. Unajua wazazi wengi huwa tuna underestimate umuhimu wa kuongea na wanetu na kuwasikiliza kirafki ila ukitaka kujua gharama ya kutokumsikiliza mtoto wako uwe mzazi ama mlezi basi muulize mtu ambaye analea mtoto ambaye hakuwahi kusikilizwa hivyo walimwengu wakamsikilizisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,985
  Likes Received: 1,909
  Trophy Points: 280
   
 12. Candy kisses

  Candy kisses JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Dah kisa kizuri sana,
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160

  Wee acha tu, wakiona komputa wanaanza kulalamika, yaani mama anacheka na komputa tu lol
  Anyway, tutafika tu
  Yaani Bazazi, mama mwenyewe ni bazazi, hata ya kuwaambia watoto yapo?
  Anyway, wanakua kwa nguvu za Mwenyezi tu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160

  Wee acha tu, wakiona komputa wanaanza kulalamika, yaani mama anacheka na komputa tu lol
  Anyway, tutafika tu

  Yaani Bazazi, mama mwenyewe ni bazazi, hata ya kuwaambia watoto yapo?
  Anyway, wanakua kwa nguvu za Mwenyezi tu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,681
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Sina mengi ya kuongea; 'U made my day in learning-wise'
   
 16. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Thanks Mtambuzi kwa hadithi hii nzuri
   
 17. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  platozoom am a responsible mother, wife and a lady for my family aisee. Hata kama nitakuwa natoa mfyonzo but nahakikisha it is doens't cost my kids or anyone else at my family.

  my brother your family is the only priceless asset you have under the sky, and to me that is the only thing which gives me pleasure and joy.[/QUOTE]


  Mtu akisema hivi huwa namuona kama mzee!......vijana wa siku hizi mmh
   
 18. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi hapo penye bold pamenigusa sana. Laiti tungelikuwa na uwezo wa kuyasoma haya yote na kuyafanyia kazi naamini jamii yetu ingeishi kwa amani sana.
  Thanks kwa makala nzuri.
   
 19. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  NICE STUFF BABU Mtambuzi! nitakuwa nawasikiliza na kuwavumilia kwa utundu wao kha!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,682
  Trophy Points: 280
  Nimehisi uchungu sana hasa kwa mimi ambae sijalelewa na mama yangu mzazi!
   
Loading...