Siku za CCM kuitwa wapinzani zakaribia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku za CCM kuitwa wapinzani zakaribia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gabraison jr, Oct 11, 2011.

 1. G

  Gabraison jr Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha magamba kimepoteza mvuto wake mbele ya watanzania waliowengi kutokana na sera yake ya kukumbatia mafisad na kutotekeleza waliyoahid wengi wautabiri mwaka 2015 ccm haitakuwa tena chama tawala bali ni chama cha upinzani
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hakina hadhi ya kuwa chama cha upinzani kitabaki tu kwenye historia.
  chama cha upinzani lazma kiwe na changamoto kwa chama tawala.
   
 3. m

  mharakati JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tuache ushabiki CCM itang'ang'ania kiti cha urais mwaka 2015 labda waweke mtu ambaye hawezi kabisa kupigiwa kura na kuiba hiyo ni mlima wa kilimanjaro, la sivyo watashinda kwa nguvu yao ya dola..cha muhimu tujitokeze vijana kugombea hivi viti vya ubunge majimboni mwetu tuwape upinzani viti vya kutosha na kazi yetu ionekane kwa wananchi bungeni. hii italeta ushindi 2020
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,984
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Mambo hubadilika kila wakati,2015 inawezekana kabisa.
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,984
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Na wao wanalijua hilo.
   
 6. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Watatumia faida ya kuwa na dola mkononi kuendelea kutawala!Hata hivyo wajue kwamba mweleka wao upo karibu mno!
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  CCM itakufa hata kabla ya 2015
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Sasa ni mwisho wa kuchakachua wajue hilo
   
 9. G

  Gabraison jr Member

  #9
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yah hilo halina tatzo kama CDM wakiwaelimisha na kuwahamasisha watanzania wa mikoa ya pembezon hususan Ruvuma ccm itafika kikomo
   
 10. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakipita magamba tutajikuta tunajuta mara 100 ya hapa tulipo..........
   
 11. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  CCM imekufa na mbaya zaidi Viongozi wake akina Mukamasi na Nepi Bongo zao zina kansa.

  Wao wanafikiri CDM ndo inasababisha wachukiwe na wananchi, CCM hawajui tatizo la kukosa mvuto.Hawa Viongozi wa ccm wanapambana na CDM akili zao zote zinaiwaza CDM. Badala ya kuelekeza mawazo jinsi ya kutatua kero za wananchi. Migogoro ya ardhi, madini na mengine mengi.

  Kazi ya CCM ni kukumbatia wawekezaji tu ili wapate 10%. CCM ni wabinafsi, wanajali tumbo zao

  CCM wanasahau kuwa Serikali ya CCM inatakiwa itoe huduma bora kwa wananchi (Afya, Elimu), kuboresha uchumi (thamani ya shiliingi), Kutoa ajira kwa wananchi hasa vijana.

  CCM imekumbatia ufisadi na CCM inategemea hela za wafanyabiashara na dili za ufisadi kama Dowans.

  Sasa NEPI anaeza CCM kwa watu wenye njaaa.

  CCM acheni hizo, mtakufa na uroho wenu wa mali, acheni ufisadi.

  Let CCM die
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  NAHISI shetani ni mwanachama wa CCM!
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tu tuone kwenye uchaguzi wa CCM mwaka 2012.
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Tudai tume huru ya uchaguzi...hizi "stori" nyengine zitajishughulikia zenyewe.

  Bila tume huru ya uchaguzi na elimu ya uraia kwa wapiga kura....kiondoa CCM madarakani ni lazima watu wengi watatoka mhanga.

  Kikwete kama ni msomaji wa wakati basi angehakikisha kabla ya kumaliza muhula wake kuwa anahakikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umejadiliwa kwa uwazi...hili litapelekea kuandika katiba ambayo itafaa kupewa jina la Katiba ya Tanzania....pia kuhakikisha Tz inapata Tume huru ya uchaguzi kama anapendelea kuona TZ inabaki kisiwa cha "amani na utulivu".

  Haya yasipofanyika uwezekano wa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa wataka uhuru zitaibuliwa na itapelekea kupata NTC hapa TZ na vifo kuongezeka. Hivi vifo vya ajali za barabarani na ukosefu wa huduma za afya vinatutosha..hatustahiki kupata vifo vya ziada kwa kulinda kikundi cha siasa au wanasiasa kuendelea kutawala TZ bila ya tija kwa wananchi.

  Ni vyema vyama vya upinzani kupanga mkakati wa pamoja ili kudai tume huru . Time waits for no one..2015 hiyo hapo imefika!!!

  Tusitegemee matokeo tofauti ya uchaguzi chini ya tume hii iliyopo. Tusijidanganye!
   
 15. KIDESELA

  KIDESELA Senior Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Kila siku naomba mungu hawa magamba wafe kabisa,halafu tunaanza na mkapa na mawaziri wake kuwaburuza mahakamani na kuwafunga kwa wizi walioufanya,halafu aje vasco dagama na mawaziri na marafiki zake wte na mwanae riz tunawafunga na kuwafilisi hapo ntakuwa na raha ambayo sijawahi kuhisi!mungu ibariki nchi yetu ya asili waangamize wote walioifikisha hapa
   
 16. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Tatizo viongozi wa juu waCCM wameshindwa kubainni adui wao.

  Kwa mawazo yao wanafikiri adui yao mkubwa ni CDM.

  Adui yao mkubwa ni kushindwa kushughurikia matatizo sugu ya wananchi kama vile:

  1.Rushwa
  2.Ufisadi
  3.Kuongezeka kwa ufa kati ya maskini na matajiri na mengine mengi.

  "CCM will die on its own success"
   
 17. s

  salustian Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wameshajinyonga wenyewe, wanafahamu fika kuwa kaburi li karibu mno, ndo maana wanaita mizuka (Mkapa) toka makaburini kuja kuwafufua.
  Mkapa kuitwa na magamba kwenda Igunga kufanya kampeni naye anakubali bila haya kuandamana na Rostam aliyeitukana ccm siku si nyingi kwamba wana siasa uchwara, siasa za maji taka ni ishara tosha kuwa wameshakufa tayari, kilichobaki kuzika.
  Sasa utamtofautisha vipi Mkapa na mkulima wa Lingusenguse Songea anayeshabikia ssm kwa vile tu kapewa fulana ya njano?
   
 18. T

  Tata JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Kama katiba hii haitabadilika na uchaguzi ukasimamiwa na Tume hii hii ya uchaguzi kwa taratibu hizihizi na wasimamizi walewale - yaani wakurugenzi wa halmashauri za miji walahi wapinzani watausikia uraisi kwenye runinga kama ambavyo wamekuwa wakiusikia. Hivi hamjajifunza tu kuwa Igunga wapinzani mmeshinda kura ila ametangazwa mbunge wa CCM na ndicho kitakachotokea mwaka 2015?
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Nonda nakubaliana na mtazamo wako. Ni jambo jema kwa wapinzani kuwa na matumaini kwenye siasa ila inabidi matumaini hayo yawe na msingi unaoeleweka. Ni dhahiri kuwa CCM hawako tayari kuandika katiba mpya kabla ya uchaguzi ujao wa 2015. Na hili wanalifanya kwa makusudi kama mkakati wao wa kubakia madarakani kwa sababu ukweli ni kuwa kitakachowabakisha madarakani CCM ni mfumo wa kikatiba na kiutawala uliopo unaotoa mwanya kwa CCM kutumia vyombo vya dola, tume ya uchaguzi na pesa za walipa kodi ili kushinda uchaguzi.

  Mimi ninapendekeza wapinzani wawe na Plan B ikiwa CCM watachelewesha kwa makusudi mchakato wa kuandika katiba mpya kabla ya 2015 jambo ambalo ninaamini lina uwezekano mkubwa wa kutokea. Inabidi wapinzani wadai mabadiliko ya katiba ya sasa ili iundwe tume mpya huru ya uchaguzi itakayosimamia uchaguzi wa 2015 bila kukipendelea chama tawala. Wadai pia kuandikwa upya kwa daftari la wapiga kura chini ya usimamizi wa chombo huru siyo lazima ile tume ya uchaguzi ili tuwe na uhakika wa idadi halali ya wapiga kura. Mwisho wadai mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kuongeza udhibiti kwenye mchakato wa kipiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo.

  Mabadiliko haya yakifanyika kabla ya mwaka 2015 uwezekano wa kuiondoa CCM utaongezeka hata kama katiba mpya haitakuwa imeandikwa. Vinginevyo hizi juhudi za wapinzani kushiriki chaguzi chini ya mfumo uliopo zitaendelea kuwa sawa na kufukuza upepo tu.
   
 20. T

  Tata JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Unachoongea ni sahihi kuwa adui mkubwa wa CCM ni wao wenyewe kushindwa kushughulikia matatizo ya wananchi. Na hata watu wa CCM ambao bado wanaweza kutafakari kwa kutumia akili zao wanalijua hilo.

  CCM wanajua pia kuwa hatari ya karibu zaidi kwao kwa sasa hivi - immediate threat - ni CDM kwa sababu ndicho chama kinachoonekana kutoa mbadala wa uongozi nchini hasa baada ya CUF kuamua kujiunga na CCM kwenye uongozi wa Zanzibar. Kwa hiyo kimkakati CCM wako sahihi kuelekeza mashambulizi yao kwa CDM kwani kwa kufanya hivyo wanashughulika na hatari ya karibu na kujipa nafasi ya kupambana na kiini cha tatizo. Kwa bahati mbaya sioni juhudi za makusudi ndani ya CCM za kupambana na kiini cha tatizo la kupoteza umaarufu na uungwaji mkono.
   
Loading...