Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
1)naanza kuwasalimu,kwa jina lake manani.
Salamu kwetu muhimu,juu yenu iwe amani.
Mola wetu mkarimu,atupe nyingi imani.
Leo ni siku muhimu,wanawake duniani.
2)wanawake ndio nguzo,hilo ninawajuzeni.
Nyinyi ndie muongozo,kweli nawaambieni.
Hilo ni langu dokezo,sana nitaelezeni.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
3)nyinyi ndie mama zetu,mlitubeba tumboni.
Tena ndie taa yetu,imulikayo gizani.
Mama ni nuru ya kweli,ituwekapo mwangani.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
4)nyinyi mama wa taifa,walimu bora nyumbani.
Wanawake mnasifa,hiyo kweli ya moyoni.
Mmelizaa taifa,asie jua ni nani.
Leo ni siku adhimu,wanawake duniani.
5)wanawake mashujaa,toka tangu beijini.
Hadi huku wamejaa,wanena hadi mbuguni.
Hakuna tena zubaa,leo wote jukwaani.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
6)mbona nyinyi mnaweza,kuushika usukani.
Taifa kuliongoza,kama ilivyobungeni.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
7)wanawake msimame,mshikamane mikono.
Pole pole na mseme,wetu ni mshikamano.
Tukamate ufalume,yawe yenu mapambano.
Ni siku ya wanawake,yafanyika duniani.
Mtunzi=Idd ninga wa tengeru arusha
Salamu kwetu muhimu,juu yenu iwe amani.
Mola wetu mkarimu,atupe nyingi imani.
Leo ni siku muhimu,wanawake duniani.
2)wanawake ndio nguzo,hilo ninawajuzeni.
Nyinyi ndie muongozo,kweli nawaambieni.
Hilo ni langu dokezo,sana nitaelezeni.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
3)nyinyi ndie mama zetu,mlitubeba tumboni.
Tena ndie taa yetu,imulikayo gizani.
Mama ni nuru ya kweli,ituwekapo mwangani.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
4)nyinyi mama wa taifa,walimu bora nyumbani.
Wanawake mnasifa,hiyo kweli ya moyoni.
Mmelizaa taifa,asie jua ni nani.
Leo ni siku adhimu,wanawake duniani.
5)wanawake mashujaa,toka tangu beijini.
Hadi huku wamejaa,wanena hadi mbuguni.
Hakuna tena zubaa,leo wote jukwaani.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
6)mbona nyinyi mnaweza,kuushika usukani.
Taifa kuliongoza,kama ilivyobungeni.
Leo ni siku adhwimu,wanawake duniani.
7)wanawake msimame,mshikamane mikono.
Pole pole na mseme,wetu ni mshikamano.
Tukamate ufalume,yawe yenu mapambano.
Ni siku ya wanawake,yafanyika duniani.
Mtunzi=Idd ninga wa tengeru arusha