Naamini kuwa wanawake wanahitaji kuwa na haki sawa na wanaume ila si kwa jinsi ninavyoona mimi hii ni vita
kati ya wanaume walio kimya na wanawake wanaotumia majukwaa kupambana nasi.
Mimi nadhani wanawake wanatakiwa kufanya kwa vitendo na si kutumia majukwaa wakati wakifika majumbani wananywea na kutenda tofauti. Moja ya mambo wanayotakiwa kuyafanya ni:
kukataa VITI MAALUM maana wao sio waremavu au watu wenye mahitaji maalum
kukataa aina yoyote ya upendeleo
kufanya kazi kwa bidii
kuwa wajasili kwa kutii sheria na kuwajibisha yeyote anayewaadhalilisha
kupunguza majukwaa na kuwa na mikakati
kufika vijijini
kukataa kuwa mboga za viongozi waserikali na kutumiwa