mkuu ina mgharimu kiasi gani kumaintain hiyo afya,je mtanzania wa kawaida atamudu!!!nadhani hii kitu bado ni tishio!!Baada ya kufuatilia kwa umakini maendeleo ya afya ya Magic Johnson kwa miaka 20 sasa, na kugundua kuwa mtu anaweza kupata watoto wasio na VVU wengi atakavyo..nimefikia hitimisho kuwa ukimwi si tishio tena
Baada ya kufuatilia kwa umakini maendeleo ya afya ya Magic Johnson kwa miaka 20 sasa, na kugundua kuwa mtu anaweza kupata watoto wasio na VVU wengi atakavyo..nimefikia hitimisho kuwa ukimwi si tishio tena
Ndugu zangu,
Nimeona si vibaya kuwakumbusha tunapoenda kwenye siku ya Ukimwi duniani hapo kesho tujaribu kuangalia kwa mapana baadhi ya mambo na kujitafakari kwa mapana kama tuko kwenye njia salama ama la.
Nafarijika kusikia na kutambua kwetu kuwa janga la UKIMWI linahitaji elimu kwa jamii yote ili kufanikisha mapambano dhidi yake. Na nafarijika pia kusikia aghalabu siku hizi vitendo vya unyanyapaa vinapungua kwa kiasi kikubwa. Ndugu zetu walioathirika wasitengwe au kunyanyaswa.
Ningependa sote tujiulize tena maswali magumu bila aibu na tuchukue hatua bila ajizi. Je, tangu mwaka huu uanze tumeshiriki kiasi gani kuzuia kuenea kwa UKIMWI? Je, wewe umekwisharekebisha mwenendo wako na kuacha tabia zinazochangia kuenea kwa UKIMWI? Je, kwenye mazingira unayoishi (sehemu ya kazi au vyuoni) pamekuwa na mwamko mpya wa kupambana na UKIMWI? Wewe unashiriki vipi?
Kila mmoja atafakari kwa dhati moyoni mwake na achukue hatua. Tusaidiane kwa kila hali kuweza kujikinga, na kwa walioathirika tayari kuwatendea haki bila ubaguzi. Kila sehemu iwe na utaratibu wa kukumbushana mara kwa mara juu ya UKIMWI, na mkakati mahususi wa kuzuia kuenea kwa virusi vya UKIMWI.
Nawatakia afya njema na mchango mwema kwenye jamii yetu inayotuzunguka ili tuutokomeze UKIMWI na kuifanya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla kua ni sehemu yenye mafanikio yanayotokana na afya njema.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika.
abdulnoor3@gmail.com
Matanagazo ya siku ya Ukimwi Duniani yanayoazimishwa tokea Mkoani Lindi kupitia TBC - 1 yamepooza kinoma, watangazaji wa TBC inaonekana hawakujipanga kabisa. BI Mwanahawa Lugongo ambae anaendesha matangazo hayo ni kama amekurupushwa...matukio yanaenda kiholela tu.. sauti zinakatika katika hovyoo..
Aibu MKURUGEZNI CLEMENT MSHANA.
CCM wengi ni waathirika...Katika Maazimisho ya siku ya ukimwi ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Lindi, wanaCCM wa Mkoa huo wamepamba maazimisho hayo kwa shughuli mbalimbali za Chama walizoziandaa katika kufanya Maazimisho hayo kufana, walijigawa katika Makundi kulingana na Jumuiya za Chama hicho ambapo jumuiya ya vijana walifanya maonyesho ya gwaride la chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Pia jumuiya zingine walijipanga vema katika maandamano ya kumpokea na kumsindikiza Mheshimiwa Rais kitendo ambacho Mheshimiwa Rais kilimvutia na kukisifia, lakini pia vikundi vya sanaa na uhamasishaji.
Pia katika matukio mengine vijana wa CUF ambao walijipanga kubeba mabango yenye ujumbe wa kukashfu viongozi wa CCM wa mkoa huo walishindwa kufanikiwa azma yao hiyo baada ya kujikuta kuwa miongoni mwao wanawaunga Mkono viongozi wa CCM na hivyo kufanya mabango hayo kutotumika.
Katika Maazimisho ya siku ya ukimwi ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Lindi, wanaCCM wa Mkoa huo wamepamba maazimisho hayo kwa shughuli mbalimbali za Chama walizoziandaa katika kufanya Maazimisho hayo kufana, walijigawa katika Makundi kulingana na Jumuiya za Chama hicho ambapo jumuiya ya vijana walifanya maonyesho ya gwaride la chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Pia jumuiya zingine walijipanga vema katika maandamano ya kumpokea na kumsindikiza Mheshimiwa Rais kitendo ambacho Mheshimiwa Rais kilimvutia na kukisifia, lakini pia vikundi vya sanaa na uhamasishaji.
Pia katika matukio mengine vijana wa CUF ambao walijipanga kubeba mabango yenye ujumbe wa kukashfu viongozi wa CCM wa mkoa huo walishindwa kufanikiwa azma yao hiyo baada ya kujikuta kuwa miongoni mwao wanawaunga Mkono viongozi wa CCM na hivyo kufanya mabango hayo kutotumika.