Mema Tanzania
Member
- Feb 23, 2020
- 66
- 65
Ikiwa leo ni Siku ya ufahamu kuhusu usonji duniani tutizame kwa uchache kuhusu suala hili
Usonji au tawahudi kwa kiingereza autism ni tatizo la nafsi na hisia linalowatokea watu angali watoto na kuathiri uwezo wa kuwasiliana na wengine. Wenye tatizo hawaonekani watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuangalia wengine pale wanapozungumza au kushirikiana na watu wengine katika mambo kadhaa.
Pia hawako vizuri kimawasiliano muda mwingine hawawezi kuongea au kuzungumza na watu wengine. Mtu mwenye tatizo hili mara nyingi hurudia matendo kadhaa na anaweza kuhofia vitu katika mazingira yake yasiyoeleweka, hujijibu wenyewe, wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine hafikirii kina umuhimu.
Tawahudi ni ugonjwa wa ukuaji wa neva unaojumuisha kudhoofishwa kwa uwezo wa mwingiliano wa kijamii na mawasiliano, na kwa tabia finyu na ya kujirudia. Dalili hizo huanza kabla ya mtoto kutimiza miaka mitatu. Ugonjwa wa akili kwa watoto huathiri uchakataji wa habari katika ubongo kwa kubadili seli za neva na sinepsi zake zinavyounganika na kujipanga.
Usonji ni moja ya matatizo matatu yanayotambulika kama ugonjwa wa akili wa watoto (ASDs), mengine yakiwa maradhi ya Aspaja, ambayo hayacheleweshi ukuaji wa kiutambuzi na lugha na tatizo la ukuaji Ulioenea (PDD-NOS) ambao hutambuliwa kikamilifu wakati vigezo vyote au Aspaja havijatimizwa.
#WorldAutismAwarenessDay