Siku ya mwisho kwa tanzania-hii hapa

peacebm

Member
Jan 31, 2010
57
9
Kwa Takwimu zilizotolewa jana zinaonyesha kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza AFRICA, na ni nchi ya kumi DUNIANI inayotegemea misaada toka kwa wahisani,
na kasi ya kutegemea wahisani inazidi, wakati Kenya ikipunguza kasi hiyo kwa kupanda kwa uchumi na kusimamia vyanzo vya mapato.

kwa mtaji huu, nchi yetu haijawahi
1. Kupatwa na SUNAMI(any natural disaster)
2. Kupatwa na VITA vya wenyewe kwa wenyewe
ambvyo vyote hapo juu hudidimiza uchumi wa nchi kwa zaidi ya 75%

mtazamo wangu finyu
1. Madini tuliyowapa idhini wawekezaji
(a) Almasi ambayo 1gram=?
(b) Dhahabu ambayo 1gram=100,000
(c) Tanzanite ambayo 1gram=>1,000,000
(d) Uranium ambayo 1gram=?
(e),,,,,,
(f),,,,,,,.....
................endelezeni hapo by filling the blanks

Madini yote haya yalipoanza kuchimbwa na wawekezaji ndio yaliyofanya uchumi wetu kuwa tegemezi zaidi huku yakiliingizia taifa hasara za uharibifu wa mazingira na kuwanufaisha tu magamba

Enzi za Nyerere ilikuwa vipi tulilima
(1) Mkonge
(2) Pamba
(3) Kahawa
(4) Pareto
(5) Zabibu
(6)...........
(7) ........endelezeni hapo
na kwa kutumia vyote hivi hapa juu Hayati Babu Nyerere aliweza kuendesha uchumi na kujenga nchi kadiri ya uwezo wake wote na kuhakikisha kwamba:
(1) Anakopa pesa kwa wahisani ambazo anajua atarudisha siku akija kununua mitambo ya kuchimbia madini bila kuwapa wahisani sekta hiyo
(2) Anajenga viwanda vya kutosha kuchakachua malighafi zinazozalishwa.

(3) Anajenga mahitaji ya huduma za jamii(shule, hospitali, barabara....)

(4) Anadumisha heshima,amani, upendo, mshikamano, usawa.......

(5) Analinda kwa nguvu zote sehemu zenye madini ambayo anajua yataliletea taifa mapinduzi ya 100% kimaendeleo pindi tutakapokuja kuyachimba sisi wenyewe kwa mitambo yetu wenyewe

Sasa sijui nchi yetu inaelekea wapi kama madini yote yanakaribia kuisha ardhini bila faida yoyote, viwanda vyote tumeviua, mashamba yote tumeyatelekeza na kusitisha kilimo cha kisasa huku tukijidanganya kilimo kwanza,

NAWAKILISHA HOJA NIKIOMBA MAONI YENU
 
Inahuzunisha! Kama Serikali yetu inaliona hili iangalie ni wapi inaweza kubadili hali ya upepo inavyokwenda. Kwa kuanza, miradi mipya ya upande wa madini iwe 50% kwa 50% kusiwe na mjadala! Kwenye kilimo kuwepo na hatua za makusudi kabisa kuhamasisha kilimo kwa kuangalia upya bei za mazao yetu. Ziboreshwe ziwe ndiyo kichocheo cha kuwafanya wakulima wahamasike zaidi kulima kilimo bora! Serikali isiwasikilize wahisani wenye maneno ya kijinga eti msitoe ruzuku kwenye maswala ya kilimo! Chakula tunakokwenda ni kama ilivyo kwa mafuta ilivyo sasa duniani! Watu lazima wale.(hapa namaanisha mazao ya vyakula) Tujenge viwanda vya kutumia mali ghafi zetu tutakazolima wenyewe. Nawasilisha
 
Mi nasema hivi? bora mkoloni arejee tujue moja! Huu ni ujuha kwa kweli.
Ungependekeza mkoloni ambaye unafikiri atatufaa. mreno? Mspaniola? Mjerumani? Mwingereza?
Mmarekani? Mfaransa?Mwisrael? Kaburu? Mwarabu, mchina? Au Mseveni na Kagame?
 
Ungependekeza mkoloni ambaye unafikiri atatufaa. mreno? Mspaniola? Mjerumani? Mwingereza?
Mmarekani? Mfaransa?Mwisrael? Kaburu? Mwarabu, mchina? Au Mseveni na Kagame?

Mjeremani should do the trick, hawana longolongo, wako serious na kazi.

Watatunyonya lakini powa tu kuliko hali ya sasa.
 
Back
Top Bottom