Siku ya mtoko wa kwanza, mpenzi anakutana na yule uliyeachana naye…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya mtoko wa kwanza, mpenzi anakutana na yule uliyeachana naye…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 22, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Inaweza kutokea kama ajali tu, hujawahi kumwambia kuhusu mwanaume uliyeachana naye miezi kadhaa iliyopita baada ya kudumu naye kwa muda mfupi sana katika mapenzi yenu kutokana na kukumbwa na vurugu za mara kwa mara Kwa kifupi huyo mpenzi alikuwa ni mnyanyasaji sana. Hukuwahi kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kwa mpenzi mpya kwa sababu hamkuwahi kuzungumzia jambo hilo.

  Lakini kibaya zaidi watu hao wanafahamiana na baada ya kukutana kwao katika mghahawa huo mliokwenda wanasalimiana kwa bashasha na kuzungumza kidogo kuhusu biashara zao wanazofanya pamoja……………. Haiishii hapo huyu mpenzi mpya anatumia nafasi hiyo kukutambulisha kwa huyu mpenzi wako wa zamani kwamba wewe ndiye mtarajiwa wake kama mambo yatakwenda vizuri……………

  Hebu niambie mwanamke, unakutana na shiranga hili unafanyaje……………………..?
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi , ulishaambiwa wewe ni bias bado tu hujaacha. Back to the topic, introduction itaendelea kama kawaida lakini nitasitisha maongezi marefu wakati ule ili kila mtu achukue zake. Maelezo marefu nitampa baadae kuwa alikuwa ex, hii ni kuepusha uzushi utakao tokea hapo mbele.

  Si unajua kuna wanaume wengine wanatabia za kike, keshakuona umemove on lazima akufanyia vagi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  MadameX nimeshamalizana na mlalamikaji kwa PM, na sasa tunaenda sawa.
  :focus:
  Umejibu vizuri, lakini kumbuka wanaume wakiachwa huwa inakuwa nongwa, na hudhani kama anaweza kutumia nafasi hiyo kukumaliza kwa kumweleza mpenzi mpya uzushi mwingi...?
  Unadhani uhusiano wenu utakuwa salama kweli?
  tuseme mpenzi mpya amekuelewa lakini je itakuwaje pale mpenzi wa zamani atakapomtembelea huyo mpenzi mpya nyumbani kwake na kukukuta wewe ndani ya nyumba, utamwandalia soda, chai au kahawa? Kumbuka hamjafunga ndoa mna date tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. N

  Neylu JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Patamu hapo..! Kwanza lazima nitaishiwa pozi ghafla.! Kitakachofuata baada ya mazungumzo itabidi nimweleze mpenzi wangu ukweli woote tukiwa wawili..

  Ishawahi kunikuta ya namna hiyo.. Yule ex akaniambia nisimwambie mpenzi wangu kwani urafiki wao utaisha, tena aliniomba sanaaa.... I agreed.. Sasa unajua nini kilichotokea?? Yule ex yeye ndio akamwambia mpenzi wangu tena hakumwambia kama nilikuwa ex wake.. Alimweleza kwamba bado tunaendelea..! Mpenzi wangu hakuniuliza chochote, taratiiiibuu akakata kamba, nilikuja kugundua mchezo mzima baadae sana..!
   
 5. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hainihusu.......napita tu
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Kama ulivyosema kuwa hapatakuwa na usalama kwahiyo sidhani kama atakuwa mjinga kumleta nyumbani kwasababu tayari atakuwa inampa shida yeye. Pili, akiwa mwenye akili lazima ajue kuwa huyo bwana ni history kama nina story nae nisingemwambie ukweli.

  Ikiwa bado inaleta matatizo inabidi awepe ultimatum, mwanaume lazima awe wa kujiamini sioni kuishi kwa kushukushuku.
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hapa ndipo shida ilipo.. sijui kwa nini watu wengine huwa wanashindwa kukubaliana na ukweli kwamba 'it is over' na kwamba kila mtu anapaswa asonge kivyake..
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Ngoja nijifiche pembeni nione!
   
 9. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Anko! kama yule wa mwanzo tushamalizana wala sioni haya sababu yeye aliniona si wa mana,sasa huyu nilonae sasa anipendeza kwa mengi tena raha sanaaaaa anione ,akisema wa nini mwenzie anasema ananipata lini....
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo utamchunia kama hivi.......................

  [​IMG]
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Dah Baba yangu hii mitego mwe!! Afu jinsi ilivyo huweziamini jinsi dunia ilivyo ndogo aisee.

  Kuna rafiki yangu alijikuta kwenye situation kama hiyo. Boyfriend wake (ambaye walikuwa wanawasiliana tu kwa simu) alikuja Tanzania na wakakutana kwa mara ya kwanza. After some times za kuzoeana yule Boyfriend akawa comfortable na kuanza kumwuintroduce rafiki yangu kwa friends zake. Ndipo siku ya siku likamfika. Boyfriend alimweleza wazi kuwa kuna swahiba wake amerejea toka mikoani anataka aonane naye. Wakaenda, wakati boyfriend anamtafuta kwa simu huyo swahiba si akataja jina la Ex wa mdada! Ex - ambaye hakuwa really ex- wake kwa kuwa hakuwaga nae officially na hawakuachanaga kabisa - alikiri kuwa siku moja moja walikuwa wanakumbushia.

  Alichokifanya ni na yeye kumpigia simu swahiba wa boyfriend wake akamwambia...mimi ndo huyo girlfriend unayekujatambulishwa na flani................ hahah jamaa alikuwa mstaarabu akauchuna aisee!

  Kwa upande wangu dah.....nlivyo na kiherehere ningemwambia tu ukweli mara tu atakapoondoka huyo mjamaa na kisha nitampa muda wa kuasess the situation na kufanya maamuzi ambayo nitamuhakikishia kuwa sitomlaumu kwayo.
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hahahha Kaizer best, huyu Mtambuzi aisee anawatafuta watu aisee.
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu MwanajamiiOne unajua wakati mwingine nakuwa kama naota tu.................
  [​IMG]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Baba yangu naomba Mwenyezi MUNGU akupe maisha marefu yenye ndoto nyingi zaidi kwa sababu kupitia ndoto zako wengine tunajitambua na kujielewa na kujifunza mengi. Ubarikiwe sana Baba yangu.
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu MwanajamiiOne Wenzako humu wanasema mimi ni BIAS....................LOL
  Kutwa kunisengenya............

  [​IMG]
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Baba Yangu......wamesahau kuwa hakuna Expert wa kila kitu? Kila mtu anaspecialize kwenye eneo alipendalo. Wewe umechagua hili so una haki.

  unless waseme hata wale Magyno wako bias kwa kuchagua eneo hilo la mwili na wale wa watoto kuchagua watoto tu!.
   
 18. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mhhhhhh
   
 19. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Angalia mlivyo waongo we mtambuzi lini umeni PM,sina maana nahitaji ila nataka kuonyesha na we ni walewale
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  jeneneke, lakini sikutaja hata jina lako................ Je umejuaje kama nakuzungumzia wewe.................? LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...