Siku ya kwanza kukutana na mtoto wa kishua...

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,635
37,834
Basi bwana kwa vile nilikuwa na chat chat naye mtandaoni na kutumiana ma picha ya mahaba kwa muda mrefu basi nikaona itabidi nionane naye mtoto wa kishua, sikubali aiseee, toto rangi ya chungwa, ziwa saa sita unusu, toto slim fit, figure number 8, toto macho yanaitaa, kiuno cha nge nyuma kasusiwa, acha kabisa acha kabisa.

Sasa siku ya siku ikafika bwana, nikajitutumua vilivyo, nikajipanga nikapangika - mfukoni kwa mara ya kwanza maishani namiliki laki kadhaa hivi - natembea kwa umakini mkubwa vibaka wasije kunichomoa kuelekea meeting point mitaa ya posta posta pale kati kabisa kwenye Hotel moja kali saana.

Nafika pale bwaana sikukaa sana anaingia binti mrembo, kaumbwa kaumika sheikh - kavaa gauni refu limemchora number 8, viatu mchuchumio laah - watu wote midomo wazi pale hotelini... hata waliokuwa na wenza wao wanakodoa.. hapo hapo nikajua huyu mtoto ni pic kali...nikajua sasa leo Masanja nisirudie makosa yangu.... wahudumu nao mimacho yote kwake...walatino nao ndiyo usiseme.... nikasema hapa ndipo napopataka - Maganga leo dodo si ndo hili chini ya mfenesi

Hagi moja kali saana la kizungu nikampa, smile moja kali sana ya kiratino ...tukaenda kuketi..... kama kawaida mhudumu akaja tukaagiza vinywaji baridiii.....huku tukipeana mastory as if sisi ni wapenzi wa muda mrefuuu - zikaja bites bites, vyuku - meza ikachafuka kwa muda mfupi.... mimi ndiyo Maganga bwana ...sipendagi mautani kwenye mambo serious.

Baada ya mazagazaga yote bill ikaja mezani - mwanaume kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe nikamwaga mpunga mezani na keep change juu kuonyesha ushujaa wangu kwa mrembo... mrembo akashusha pumzi ndefu huku aliniangalia kwa jicho la mahaba--- Thanks Mag.....I really enjoyed... your nice person... thanks so much..... (Mag ndiyo kifupi cha jina langu Maganga) si unajua tena ukikutana na watoto wakali.. Na mimi nikakumbuka cha kuombea maji nikajibu - thanks too bby....huku na mimi nikimkata jicho na kuonyesha naomba kitu kwake.

Haya bwana, wakati ukafika wa kuagana, akaniambia lazima awahi nyumbani maana wazazi wake saa 12 kamili huwa wanarudi toka job, nikamwambia pouwa usijali "there is always next time baby" huku nikimwaga tabasalamu lingine la nguvu na yeye akinishushia la kwake....kwa mara nyingine nikaona jicho la mahaba... nikagundua mtoto kashasomeka, mwili wote huo kashanikabishi niutumie nitakavyo mimi - ni kiasi cha muda tu kuzungumza!!

Nilimpa hela iliyobakia yote atumie kwenye Ubber nikabakia na buku la nauli nililokuwa nimelificha kwenye mfuko mwingine - pia nikamweleza kwamba nitabakia kidogo maana dereva wangu alikuwa kaenda mbali kidogo nilimtuma kitu... akasema usijali mpenzi huku akinigea tabasamu tena - tulisimama tukapiga ma hagi mazito ya kizungu na kiratino kisha akafunguliwa mlango na mhudumu akasepa.... huku nikimsikindiza kwa macho kucheki umbo lake kwa nyuma, ama kweli mtoto kaumbika vilivyo...nilitamani nimwite tena yaani....

Niligeuka kurudi hotelini kuzuka kidogo kisha niondoke zangu, nikakutanisha macho na wahudumu wawili wa kike na kiume waliokuwa wanatuhudumia...wakatabasamu kuashiria wamenikubali... nikarudi kuketi huku nikiwa sina mawazo kabisa kuhusu pesa nilizotumia - yaani zimekwenda kihalaki kabisa...wale wahudumu waliniomba number yangu ya simu nikawapa...

Mzee mzima nilisubiri kama dakika tano sita hivi zipite ili mrembo atokomee, baada ya hapo na mimi nikaondoka kusogea kwenye kituo cha basi pale posta mpya ili nisepe zangu home kabla ya muda wa kugombea siti na msongamano haujafika...mfukoni nina buku langu.. nikachoma ndani ya daladala...

Guess what? yaani nina maana unajua kilichoendelea baada ya hapo??? stay turned.
 
2770320_2754471_JamiiForums-1361292337.gif
 
Chai zingine muwe mnaangali na nyakati jamani ..now jua kali sana hii chai haipandi hata kwa viboko
 
Back
Top Bottom