Mwanamke: Unatoka mtoko wa kwanza halafu unakutana na karaha hizi….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke: Unatoka mtoko wa kwanza halafu unakutana na karaha hizi….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 18, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mtoko wa kwanza huwa unawaweka wanawake katika wakati mgumu ukilinganisha na wanaume. Wakati wanaume kwao sio tatizo kubwa la kuwaumiza vichwa, kwa wanawake huwa wanajiuliza maswali mengi sana kuhusiana na huyo mtu anayekwenda kuonana naye.Hebu tuchulie mwanamke ametoka na mwanaume kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufahamiana na kuangalia kama anaweza kuwa na muafaka na mwanaume huyo kwa matarajio ya kujenga familia bora. Lakini kinyume chake anakutana na karaha hizi zifuatazo. Je kama ni wewe mwanamke unakabiliana na hali hii utafanyaje?

  1. Unagundua kwamba mwanaume uliyetoka naye ana mke au ana mpenzi wake..

  Baada ya kufika kwenye mgahawa kwa ajili ya kupata mlo wa usiku pamoja, katikati ya maongezi yenu mwanaume huyu anakushika mkono kama ishara ya upendo wakati mkiwa mmekaa mezani. Unapochunguza vidole vyake unagundua kwamba ana alama ya pete ya ndoa, unapomdadisi anakanusha, lakini baada ya kumbana sana anakiri kwamba anaye mke lakini ndoa yake ina vurugu na inalegalegakiasi kwamba siku oyote itavunjika. Au wakati wa maongezi yenu anakiri kwamba anaye mchumba wake, lakini hadhani kama atamfaa ingawa bado wako pamoja. Je utafanya nini?

  2. Anakunywa kupindukia mpaka anashindwa kumudu mazungumzo…

  Baada ya kupata mlo mnahamia kwenye baa ili kupata vinywaji kidogo kabla ya kuachana, mkiwa hapo baa, mwanaume huyo anakunywa pombe kupita kiasi mpaka anaashindwa kumudu mazungumzo na kuongea pumba tupu.

  3. Anatumia muda wake mwingi kumzungumzia mpenzi wake waliyeachana..

  Inawezekana katika mazungumzo yenu unamuuliza sababu ya kuachana na mpenzi wake wa zamani.. mwanaume huyo anatumia muda mwingi kumzungumzia mpenzi wake huyo na anaonyesha dalili za dhahiri kwamba ana m-miss

  4. Baada ya kupata mlo, tumbo lako linaleta kisirani Labda chakula ambacho umekula hapo mgahawani hakikupatana na tumbo lako, ghafla unapatwa na tumbo la kuhara kiasi cha kujikuta ukipiga trip kadhaa kwenda maliwatoni, mpaka mwanaume huyo anakuuliza kama una tatizo. Je ungejibu nini?

  5. Marafiki zake wanajiunga nanyi..
  Wakati mnapata chakula na kuongea kwa bashasha, mwanaume huyo anapigiwa simu na marafiki zake ambapo anawaelekeza mlipo. Ghafla marafiki hao wanakuja na kujiunga nanyi kwa ajili ya kupata mlo mkiwa pamoja. Je ungefanyaje?

  6. Anakuwa na shauku kubwa na mwili wako.

  Wakati mkiendelea kupata vinywaji baada a kumaliza kula, mwanaume huyo anaanza kukushika shika mwili wako mara kwa mara hususan sehemu zako za faragha huku akikupiga mabusu motomoto kiasi cha kukukera. Je utafanya nini?

  7. Unagundua kwamba siye uliyemtegemea..
  Mlipokutana kwa mara ya kwanza ulimuona alikuwa ni mwanaume mzuri wa sura na umbo, mpole kiasi, mcheshi, mwenye utani mwingi na mwenye uelewa mpana. Na hizo sifa ndizo zilizokuvutia kwa jicho la kwanza na ndio ikawa ni sababu kwako kukubali kutoka naye ili mpate kufahamiana zaidi. Lakini mkiwa hapo kwenye mghahawa unagundua kitu tofauti. Wakati wa mazungumzo yenu unagundua kwamba si lolole wala chochote. Jamaa ni mweupe hajui kujieleza ana ubishi usio na maana na anayependa kujikweza tofauti na hali aliyo nayo. Lakini pia unagundua kwamba ni mwongo na asiyepima uzito wa kauli zake. Kwa kifupi ni mropokaji…. Je ungefanyaje?

  8. Mpenzi wako wa zamani mliyeachana kwa kisirani ni mjomba wake…!
  Wakati wa mazungmzo yenu hapo mghahawani unagundua kwamba ni mwanaume mwenye muafaka na anayefaa kuitwa mume. Ni mtu ambaye mnaendana kwa kila kitu, ni msikivu na mwenye subira na asiye na papara. Lakini katika mazungumzo yenu kuhusu familia zenu unagundua kuwa mpenzi wako wa zamani ambaye mliachana miaka kadhaa iliyopita kwa vurugu kubwa na kuwekeana visasi ni mjomba wake. Huyo mjomba wake anaishi mkoa mwingine na ulikutana naye wakati ulipokuwa ukifanya kazi katika mkoa huo kabla ya kuacha na kuhamia mkoa mwingine. Je utafanya nini?

  9. Kila kitu kinaenda kinyume na matarajio yenu…
  Kuna wakati huwa tunakutana na visirani mpaka tunajiuliza tulikanyaga mdudu gani siku hiyo… Inaweza kutokea mpenzi wako kafanya booking ya meza kwenye mghahawa kwa ajili ya dinner, lakini mnapofika mnaambiwa meza yenu wamepewa watu wengine, mnaona kuliko kulalamika itakuwa ni kupoteza muda bure kwa kuwa maji yameshamwagika. Mnaamua kwenda katika mghahawa mwingine, lakini kwa mshangao mnakuta napo pamejaa, manaanza kuingia mghahawa mmoja baada ya mwingine lakini kote mnakuta kumejaa. Je mtaahirisha au mtaamua kwenda nyumbani kwa mmoja kati yenu kwa ajili ya kuendelea na mtoko wenu?

  10. Unagundua kwamba pamoja na kuwa na mwili mkubwa kumbe jamaa ni mdogo sana kiumri ukilinganisha na umri wako…
  Kuna watu wamejaaliwa kuwa na miili mikubwa, ukilinganisha na umri wao. Hiyo iko kote kote, si kwa wanawake wala wanaume. Kwa mfano inatokea mwanaume uliyetoka naye wakati wa mazungumzo yenu unakuja kung'amua kwamba umri wake ni mdogo sana tofauti na muonekano wa mwili wako. Mwanaume huyu anazo sifa muafaka za kuweza kuitwa mume, lakini umri umemzidi sana kiasi cha miaka mitano. Je utaendelea kuwa na uhusiano naye au utajitoa mapema…?."

   
 2. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Namba 6 inahusika.
  Na ndio maana % kubwa ya Mitoko ya Wanaume ni kwenye Bar zenye Guest House au Hotel ambako wanaweza wakapata Chumba,wenyewe wanakwambia for Emergency Case,hasa mkiwa mnatumia kilevi...!!!
  Kumbe Wana sababu zao.
  Nimemaliza.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nice one mate!
   
 4. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Loh! Hapo kwenye number 3 inaboa saaanaa,maana mtoko wa siku hiyo ukishaisha ndIo mwisho wa kuonana mimi na yeye. Hachelewi katikati ya mchezo akakuita jina Ex wake.

  Hapo kwenye Number 7 ndo maana huwa tunaambiwa dont judge a book by its cover,unaweza kumkuta mkaka sexy body nn..sura soft kama ngozi ya kalio lakin mweupeee. Hajiamini,mlalamikaji,hawez kufanya maamuzi yake mwenyewe...ovyo kabisa!
   
 5. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Loh! Hapo kwenye number 3 inaboa saaanaa,maana mtoko wa siku hiyo ukishaisha ndIo mwisho wa kuonana mimi na yeye. Hachelewi katikati ya mchezo akakuita jina Ex wake.

  Hapo kwenye Number 7 ndo maana huwa tunaambiwa dont judge a book by its cover,unaweza kumkuta mkaka sexy body nn..sura soft kama ngozi ya kalio lakin mweupeee. Hajiamini,mlalamikaji,hawez kufanya maamuzi yake mwenyewe...ovyo kabisa!
   
 6. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  1,6,7 aisee unatamani ungekuwa umevaa bomu ulipuke nae..
  1. Et nnae but sina future nae,huku anapigiwa simu unamuona anavyo-vibrate!
  6. Yan hachelewi kukukiss na kukuita bby,wkati hata hujamkubalia, mara akiongea na simu nipo na myheartbeat(aisee nilimkata jicho,nlitaman kumpgia ukunga wa mwizi)! Na hivi alishaniboa!
  7. Akaanza story oh mymom,blah blah mydad fyoko fyoko,mara mimi nlikuwa wamwisho darasani!.
  Nlipolegea, oh gari ya shemeji(mmewe dadake)ananiazimaga!
  Aisee wakat ukimuangalia unasema juan miguel,ver smart,kumbe kichwa kina popcorn!
  Wat i did, nlmtxt mtu anipigie kuna emergence,nkatimka kama Ambulance iliyobeba majeruhi!
   
 7. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Si bora hata hiyo... Mwingine anakunyamazisha kabisa,utasikia 'Nyamaza kidogo'...loh!! Na wakat alisema hawako katika good terms na uhusiano upo ukingoni..hapo stori imenogaaa kudadaadeki unakuwa mpole tu na hasira kibao!
   
 8. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Mtoko wa kwanza geto tu kuepusha karaha zote hizo, ukileta malavidavi ndo matokeo yake hayo. Unakula mzigo kwanza, kama inalipa ndo mnapelekana bar na restauant!
   
 9. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,026
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi! Sielewi hata kidogo uzi huu! Sina la Kuchangia

  Hata Hivyo,
  Bazazi hana eneo maalum la Kumpeleka BintAdamu!
  Kwake kila Kichaka ni Choo!
  Maongezi mara Zote BintAdam anakuwa "pace maker"!
  Anakuwa Pace maker ili asimtambue Bazazi na madhaifu yake!
  Pace maker ili aweze kumtambua uimara na udhaifu wake.
  Bazazi anataka amfahamu BintAdamu ili amtawale Kirahisi.
  Akimtawala kirahisi, atamfaidi kirahisi.


  Bazazi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. NyotaMalaika

  NyotaMalaika Senior Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Yaani 1,2 na 5 vilinitokea on the same date halafu mbaya zaidi akawa anakataa kulipa bill(eti mhudumu kamuongezea)...na hao marafiki alowaita wote wakaondoka kutuachia soo.....
   
 11. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mie no 1 na 6 hakuna mjadala, its the end of the date and everythng, Madame B mbona nasubiri ule mchapo mamii
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  asante sana Mtambuzi......lakini kuna kipengele kimoja ambacho kwa maoni yangu......nadhani kingetakiwa kiwe namba 11........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,952
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  do you know what is that? is a xter of an insecured man.
   
 14. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  message sent
   
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Mie namba 2 i can understand Smtimes wanaume wanakunywa sana on a 1st date kuondoa anxiety(spelling mnisamehe frm kayumba), na kugain comfidence haswaa kama Goma lenyewe limekaba hadi penalti hivo linahitaji kuvaa raisoni namba 2 ili ulicheze.

  Namba 3 hainitishi coz formula ya substitution iliwekwa maalumu kwa kazi hiyo. Nikiongezea integration baaaaaaaass!

  Namba 4 ni nomaaaaaaaaaa! Ndo maana on a first date nagoma kwenda sijui chinese resturant, sijui alabasha kwa walebanoni, sijui ethiopian, sijui thai cusines!!!!!!!!! Ni mwendo wa kuzitiririsha bier au wine mwanzo mwisho.
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kipi hicho jamani? Preta
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hivi nyie mna njama gani.....? Siwaelewi elewi wewe na Madame B
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo namba 7 yako ni kiboko ya mambo....................LOL
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Madame B sasa kama mwanamke yuko kwenye MP inakuwaje hapo.....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,266
  Likes Received: 1,197
  Trophy Points: 280
  Yaan ningeondoka namwacha hapo2,ndo angejua akili zangu
   
Loading...