kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 719
Leo ni siku ya mazoezi kitaifa kama ilivyoelekezwa na Mh. Samia Saluhu makamu wa rais....
Mkoani Arusha zoezi hili limezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mh Gambo.
Zoezi lilianza saa kumi na mbili asubuhi katika viwanja vya mkuu wa wilaya wa Arusha na kuhitimishwa katika uwanja wa sheikh Amri Abeid Kaluta.
Zoezi hili limefana sana na kupata mwitikio mkubwa wa makundi mbalimbali.Mh Gambo alipata fursa ya kuzungumzia vita ya madawa ya kulevya ambapo alisema kwa mkoa wa Arusha zoezi hili linaendelea kimyakimya ambapo watuhumiwa wanakamatwa na kuhojiwa kabla ya kuja kutangazwa baada ya kujiridhisha na tuhuma zake.
Vile vile mkuu wa mkoa aliwaasa wananchi wasitajane kwa chuki na husuda kwani ni jambo baya na linaleta mvurugano katika jamii...."mutaje watu wanaohusika kweli na sio mtu mmegombana kwenye mambo yenu huko unaamua kumkomoa,RPC anaendelea kupokea majina na task force inaendelea kufanya uchunguzi kabla ya kuja kwenye mediaup
alinukuliwa kiongozi huyo wa juu ngazi ya mkoa.
Mazoezi haya ni kwaajili ya kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kupambana na magonjwa hatari kama kisukari na mengineyo yasiyoambukiza.
Mh Gambo akimalizia push up ya mia moja...
Mkuu wa mkoa wa Arusha akizungumza na walemavu waliokuja mazoezini
RAS mkoa wa Arusha na RPC Charles Mkumbo wakipiga push up
Taasisi za umma zilishinda mchezo wa kuvuta kamba.