Siku ya Mapinduzi Rais Magufuli atakuwa Shinyanga

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,519
6,516
Katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano hatakuwepo Zanzibar na anatarajiwa kuwepo Shinyanga kwa shughuli maalum ambapo atahutubia Taifa.

Sio vibaya kutoa udhuru wa sherehe ya Mapinduzi, lakini najiuliza hivi viongozi wa mwanzo kabla ya Rais Magufuli walishawahi kufanya hivyo, yaani Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete wakiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano?
 
kwanini umeliza?
Ni mara yangu ya kwanza kusikia Rais wa Jamhuri ya Muungano amekosekana kwenye Sherehe za Mapinduzi akiwa ndani ya nchi. Mimi nauliza kama iwapo ilishawahi kufanyika kwa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete.
 
Kwa hiyo amekosea kwa yeye kuwa wa kwanza kukosekana? What are trying to say
 
Sina mamlaka ya kusema amekosea au amepatia kwa kuwa wa kwanza kukosekana. Hizi sherehe huwa zinafanyika sehemu moja. Sidhani kama Rais Zanzibar weshawahi kufanya hivyo, yaani siku ya sherehe za uhuru wa Tanganyika wahutubu kule Zanzibar.
 
Katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano hatakuwepo Zanzibar na anatarajiwa kuwepo Shinyanga kwa shughuli maalum ambapo atahutubia Taifa.

Sio vibaya kutoa udhuru wa sherehe ya Mapinduzi, lakini najiuliza hivi viongozi wa mwanzo kabla ya Rais Magufuli walishawahi kufanya hivyo, yaani Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete wakiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano?
Hongera kwa kutambua wajibu wa Rais hadi kukosoa ratiba za Rais aliyeko madarakani.

Unastahili kupewa cheo Ikulu uweze kupanga nakusimamia ratiba za Rais.
 
Mkuu;
Usiogope Muungano wetu mtukufu ndio umekuwa imara zaidi kuliko tulipotoka. Nenda kamsikilize hotuba yake kwani ameahidi kulihutubia taifa kutokea Shy. Huenda ana mzigo anataka kuutumbulia pale pale Shy. Zee la majipu limejiweka tiyari kutumbua jipu kuubwa this time. Kila aliye chini yake kwisha shusha kaptura aache wazi jipu lilipo ili Dr asipate taabu na wembe wake.
 
Hivi raisi akiwa Zenji ni raisi wa bara na visiwani au wa bara tu, maana nasikia ana-salute kwa Sheni. Nashauri asiwe anaenda huko kwani ni kujishusha
 
Mkuu;
Usiogope Muungano wetu mtukufu ndio umekuwa imara zaidi kuliko tulipotoka. Nenda kamsikilize hotuba yake kwani ameahidi kulihutubia taifa kutokea Shy. Huenda ana mzigo anataka kuutumbulia pale pale Shy. Zee la majipu limejiweka tiyari kutumbua jipu kuubwa this time. Kila aliye chini yake kwisha shusha kaptura aache wazi jipu lilipo ili Dr asipate taabu na wembe wake.
Mhh, asije kuutumbua Muungano! Manake atawauliza Wanazengo niutumbue au nisiutumbue?
 
Hongera kwa kutambua wajibu wa Rais hadi kukosoa ratiba za Rais aliyeko madarakani.

Unastahili kupewa cheo Ikulu uweze kupanga nakusimamia ratiba za Rais.
Cheo nikipate mimi mkulima nisiejua itifaki? Nafwaaaa
 
Mhh, asije kuutumbua Muungano! Manake atawauliza Wanazengo niutumbue au nisiutumbue?

Mkuu;
Nakuhakikishia Muungano wetu upo imara zaidi kuliko tulipotoka. Ila aweza hata kumtumbua Maalim na Kaf yake amweke Profesa msomi mwenzie
 
Mhh, ngoja tumsikie. Manake tangu achimbe biti Zanzibar hajarejea tena!
 
Anaogopa protocol itakaaje huko kwani yeye ataonekana kama rais wa Tanganyika
 
Katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano hatakuwepo Zanzibar na anatarajiwa kuwepo Shinyanga kwa shughuli maalum ambapo atahutubia Taifa.

Sio vibaya kutoa udhuru wa sherehe ya Mapinduzi, lakini najiuliza hivi viongozi wa mwanzo kabla ya Rais Magufuli walishawahi kufanya hivyo, yaani Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete wakiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano?
Kila mtu anajiuliza ila tuliambiwa tusiiishi kwa mazoea.
 
Amekataa kudharaulika kwani akienda kule anonekana kama Makonda

Huu ni muungano hewa Rais wa jamuhuri lakini hawezi kuchagua hata mkuu wa wilaya katika sehemu ya jamuhuri yake

Akiwa Znz anakuwa nyoka lá kibisa afadhali hata hajaenda

Ngoja tusikie singo mpya huko shinyanga toka chato modeni Taarabu
 
yote yanayo fanyika ni kwa ustawi wa nchi yetu, Mh. anachapa kazi kwa ajiri ya taifa letu, na pia hata,zanzibar ni kwa ajilri ya taifa, kwahiyo wewe unae uliza imekuwaje,wote wapo kazini,na ni kwaajili yako wewe na mimi.si vyema kukalili, wakati mwingine uone ni kwaida tu kwasababu hakuna kilicho haribika.
 
Back
Top Bottom