Nasubiri kuiona siku Rais Samia akipigiwa mizinga Zanzibar kama ilivyo huku bara

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,209
31,847
Salaam, Shalom!!

Sisi wengine shule zetu ndogo, unakaa unajiuliza ikiwa tuna Nchi Moja Tanzania, na Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iweje akiwa Zanzibar Hana mamlaka kama huku bara?

Sasa huu Muungano mbona utata mtupu? Kwanini hawezi kugusa hata kisiwa kimoja kule Zanzibar awape wawekezaji ikiwa Zanzibar ni sehemu ya nchi Moja ya Tanzania?

Bado naisubiri siku hiyo adhimu , nimuone Rais Samia, Amiri Jeshi mkuu akipigiwa mizinga katika tukio lolote Zanzibar kama ambavyo nimekuwa nikiona huku Tanganyika.

Mungu Mbariki Mzee Warioba.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
 
Back
Top Bottom