Siku ya kwanza jijini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya kwanza jijini Dar

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by katawa, Oct 7, 2012.

 1. k

  katawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 203
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 60
  Ilikuwa ni tar 17-12 1988 nilpopata taarifa kuwa siku tatu baadaye nitasafiri kuelekea 'dizim' Dar es salaam.Maandalizi ya nguvu yakaanza ikiwa ni pamoja na kuazima nguo bila kusahau chupi.Rafiki yangu mpendwa Asuvisye akaniazima chupi aina ya vipi.
  Siku ikawadia mimi na kiongozi wangu wa msafara tukapanda basi la Zainabu.Njian nilikuwa kero kwa abiria kwa kuwa nilishangaa mambo mengi na nilikuwa nauliza maswali bila kikomo ukizingatia ni mara ya kwanza kupanda basi ktk umri huo wa miaka kumi na nne.

  Siku inayofuata tukafika dar mchana.Tulipofika magomen kiongozi wangu akanitwisha kiroba cha mchele yeye mbele mimi nyuma,akajitokeza muungwana kunisaidia nikampa kiroba mwenyeji wangu akiwa mbele yangu.Alipofika nyumbani kugeuka anaona sina kipeto aliponiuliza kiko wapi nageuka nyuma sikumuona muungwana aliyenipokea.

  siku ya pili ilikuwa ijumaa ktk tembea yangu nikapita eneo ambalo watu wengi waliovaa nguo nyeupe na kofia walikuwa wanaingia na kutoka ilikuwa majira ya jioni.nikapata shauku ya kujua kuna nini huko ndani,nikaingia nikiwa nimevaa raba aina ya DH.Kumbe ni msikiti nimeingia na viatu na watu walikuwa kwenye swala kilichotokea unaweza ukakihisi.

  Siku nyingine nikapelekwa feri na watoto wenzangu.Nilipoulizwa iwapo najua kuogelea nikakubali ili nisionekane wakuja, nikajitosa kwenye maji kwa nguvu.Washukuriwe wavuvi waliokuwepo eneo lile.

  Ndani ya muda mfupi Dar niliyokuwa naiota na kuitamani ikanikifu nikamlazimisha mwenyeji wangu anirudishe kwetu Uyole Mbeya ambako utulivu ni kama Mbinguni.

  Je mwanajamii mwenzangu hebu nijulishe wewe ilikuwaje siku ya kwanza jijini DAR?
   
 2. AKILImuchknow

  AKILImuchknow JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 216
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sio wote wakuletwa wengine ni borntown!
   
 3. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Sisi tumepata akili tukiwa Dar na bado tupo sana tu
   
 4. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2017
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Msikitini uliingia na viatu raba DH
   
 5. m

  mliverpool JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2017
  Joined: Jan 6, 2015
  Messages: 415
  Likes Received: 838
  Trophy Points: 180
  Ndo mnaotusumbuaga nyie na maustaarabu yenu ya kujifunzia mjini,,ningekuwa makonda ningeweka utaratibu maalum kuingia mjini
   
 6. wambura marwa

  wambura marwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2017
  Joined: Mar 7, 2015
  Messages: 2,187
  Likes Received: 1,097
  Trophy Points: 280
  Mimi natamani sana kufika dar
   
 7. wambura marwa

  wambura marwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2017
  Joined: Mar 7, 2015
  Messages: 2,187
  Likes Received: 1,097
  Trophy Points: 280
  Ila mkuu umetisha sana hiyo ya kupokewa kipeto cha mchele hahahaha
   
 8. upupuwapwani

  upupuwapwani JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2017
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 1,387
  Trophy Points: 280
  Kumbe ukizaliwa Dar kuna vingi unavikosa eeh
   
 9. N

  Nali JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2017
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 60
  Mm mara ya kwanza nilipanda bus la kwenda Dar wakati huo tunaita Kooch, nilianza kuandika majina ya Maeneo yote na vituo vyote tulivyopitia kuanzia mianzini, ilboru, sanawari, mountmeru, philips, kimandolu, ngulelo, kwa mrefu, nduruma, Tengeru, USA, maji ya chai, king'ori , Kia, Boma, sadala, machame, kibosho, changmai, Moshi stand......nimefanya hivyo mpk Dar, huku nikiuliza bila aibu.

  Begi langu ilikua ni malboro mbili ya rangi ya blue na nyeusi...jamani tumetoka mbali, ni kwa neema tu tumefika hapa tulipo
   
 10. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2017
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Baada ya Maji ya Chai Kikatiti Mkuu Vepe Naona Vituo Vingi sana Umeviacha...Vikiwemo Kilala, Makumira na Danish Umeruka pia Machame nadhani ndio Machine Tools.

  Kiboroloni, and then Njia Panda himo, Mwanga,Same,Hedaru,Mnazi,Mazinde,Mombo,Korogwe,Segera,Handeni,Kwedukwazu,Mkata,Wami,Msata,Chalinze,Ruvu,Kongowe,Maili moja Kibaha,Mbezi,Kimara,Ubungo,Stand ya Mkoa. Zamani ilikuwa Manzese,Argentina,Magomeni Kagera,Magomeni Mwembechai,Magomeni Usalama,Magomeni Mapipa,Fire and then Stand ya Kisutu.
   
 11. Tater

  Tater JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2017
  Joined: Oct 16, 2015
  Messages: 3,167
  Likes Received: 7,882
  Trophy Points: 280
  Daaah... Vituo vyote unavyo...!? Shikamoo Utingo..!!
   
 12. bbc

  bbc JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2017
  Joined: Jan 18, 2016
  Messages: 2,128
  Likes Received: 2,331
  Trophy Points: 280
  Mbombo ngafu fijo kama ni kweli!!
   
 13. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2017
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Ngoja niitikie tu Shikamoo ya kwanza JF Siwezi ilazia damu Marahaba...Abiria ilikuwa Ukitaka Kupanda Bus unasema tu unataka lipi unapata tiketi... Ngorika,Dar Express,Masama Safaris,Fresh Ya Shamba,Njuweni,Sawaya,Mapande,Air Msae ,Yarabi Salama,Imamu Express, Shengena ,Relwe, Kamata,Kindokyakosembe,Kindokyakombe,Zafanana,Kimotco,Islam,Hood, Air Chalinze,Price Osaka,Real No Challenger,Simba Mtoto,Metro,Born City Midfielder ,Bazuu, Moro Kuna Sharuks na Aboud zipo. Hata Treni ukipenda ilikuwepo Dar Moshi.
   
Loading...