Siku ya kumwambia mungu asante

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,855
Ndugu wana jamii,
naomba leo iwe ni siku ya kila mmoja wetu kwa imani yake na kwa mungu anayemuabudu na kumtumikia,
amwambie asante kwa wema na ukuu wote..
Kwa neema, baraka, na miujiza ambayo mungu wake amemfanyia.
Kumbuka fadhila na ukuu wa mungu wako,
kumbuka alivyokuvusha kwenye magumu mbalimbali..
Tumia muda huu mfupi kusema asante mungu wangu.
Nawatakia ijumaa njema na wikendi njema.
 
God bless you - umefanya vema kutukumbusha ila this has to be done EVERYDAY - ukiamka asubuhi - mshukuru Mungu - ukilala usiku mshukuru Mungu kwa wema wake, ukuu wake, uweza wake, rehema zake.

Tuko pamoja
 
Asante sana kutukumbusha. Naungana na waliotangulia kuwa hili la kumshukuru Mungu tunapaswa kulifanya kila siku.

Kumbuka ni kwa neema yake tunaishi na kuwa na nguvu za kufanya shughuli zetu halali za kila siku. Tunapaswa kumwambia asante Mungu ni wewe tu unayestahili KUABUDIWA.
 
Ee Mungu unibariki mimi na uwabariki wazazi wangu wawe na maisha marefu na afya njema siku zote........................amen
 
kesheni mkiomba kwani hamjui siku wala saa ...
anytime ukipata chance hata 1 min unasali
be blessed bujibuji
 
Asante sana kutukumbusha. Naungana na waliotangulia kuwa hili la kumshukuru Mungu tunapaswa kulifanya kila siku.

Kumbuka ni kwa neema yake tunaishi na kuwa na nguvu za kufanya shughuli zetu halali za kila siku. Tunapaswa kumwambia asante Mungu ni wewe tu unayestahili KUABUDIWA.

Join Date: Fri Dec 2009
Posts: 4
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0

Bishop,
Karibu sana JF, naona ujiunga leo na ukakutana na neno la Bwana wa Majeshi, Ubarikiwe sana. Basi usiishie huku tu kwenye neno, kuna Jukwaa la siasa n.k. unakaribishwa sana.
 
kesheni mkiomba kwani hamjui siku wala saa ...
Anytime ukipata chance hata 1 min unasali
be blessed bujibuji

Jiwe walikokataa waashi ndilo limekuwa jiwe kuu la pembeni jiwe lenye kukwaza, litakae mwangukia litamsagasaga nae atakaejikwaa kwalo atavunjika vipande vipande neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu machoni petu
 
Jiwe walikokataa waashi ndilo limekuwa jiwe kuu la pembeni jiwe lenye kukwaza, litakae mwangukia litamsagasaga nae atakaejikwaa kwalo atavunjika vipande vipande neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu machoni petu


thanks Pwida be blessed kwa neno lako
 
Kama si wewe, Israel na aseme sasa, hapo adui zetu walipotaka kutumeza hai Israel na aseme sasa, hapo tulipokuwa tukikabili bahari ya shamu na huku askari wa Misri Israel na aseme sasa. Mshukuruni bwana kwa kuwa fadhili zake ni za milele, yeye aliyewangusha wafalme wakuu kwa maana fadhili zake ni za milele, Ogu mfalme wa Bashani, kwa maana fadhili zake ni za milele.

Mlango wa Suleimani na waseme sasa fadhili zako ni za milele.

Mshukuruni Bwana kwa maana fadhili zake ni za milele.

Bwana ametutendea mambo makuu, Bwana kwa mkono wake wakuume,
Hakika bwana ni nguvu yetu nani atatuzui, hata wakianguka makumi elfu kushoto kwangu na kulia kwangu hapo bado sitaogopa, maana najua mtetezi wangu yu hai, nami nitauona wokovu wa Bwana katika nchi ya walio hai. Sitakufa bali nitaishi niyasimulie mambo makuu aliyonitendea. mshukuruni Bwana wote wenye pumzi kwa maana fadhili zake ni za milele.

Bwana ametutendea mambo makuu, tunafurahi. Eeh Mungu fadhili zako ni za milele. furaha yangu kubwa ni hii. Mungu wetu anatawala.

Bwana amejivika nguvu na adhama, bwana ametamalaki na kujikaza nguvu ili ulimwengu usitikisike, kiti chake kimekuwa thabiti, tokea zamani.
 
Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,
Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua,
Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,
Shida yangu nitaitangaza mbele zake.
Zab. 142
 
Ee Mungu Baba, Muumba wa kila kitu
Baba asante kwa mema yote uliyonitendea, asante kwa kunipa uhai, asante kwa kunipa kazi.
asante Baba Mungu kwa ajili yangu, kwa ajili ya wazazi wangu, kwa ajili ya ndugu zangu na majirani zangu.
nasimama mbele yako mimi mkosefu, najuta makosa yangu yote niliyatenda,
naahidi sitarudia tena, Ee Mungu nihurumie.
nawaombea wazazi wangu, ndugu zangu, mpenzi wangu, majirani zangu na wanaJF wenzangu Ee Mungu uwarehemu.
Baba bariki kazi za mikono yetu, bariki kila tufanyalo ikiwa ni njia ya kukupendeza wewe.
tujalie tuishi kama vile upendavyo.
Amina.
 
Back
Top Bottom