Siku Tanzania ikipata Rais mzalendo hakuna atakayepona

Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
468
486
Kwa namna ambavyo nchi yetu imekuwa ikiendeshwa kwa miaka ya hivi karibuni, hapana shaka yoyote kwamba bado tuna safari ndefu saana.

Na laiti kwamba Tanzania ikija pata raisi mzalendo basi tutegemee yale yaliyo wahi kutokea kwa jirani zetu wa zambia.

Nina imani kabisa ukifika wakati tukimpata raisi mzalendo atafanya yafuatayo.

1. Kwa kuamini katika uwajibikaji wa kitasisi na nguvu za kitaasisi, Raisi mzalendo asiye na chembe chembe za rushwa, atabadili katiba na kuzipa nguvu taasisi zote muhimu zinazo shikilia moyo wa nchi.

2. Kwa kuto kuhofia kuwajibishwa na yeye kwasababu ni mzalendo kwelikweli, basi hato sita kuwa chukulia hatua watangulizi wake wote walio onekana kuikanyaga katiba na kujinufaisha kupitia ofisi za uma.

3. Atajenga mifumo imara ya kidemokrasia itayo pelekea wananchi kuwa na nguvu za kuwachaguwa na kuwa kataa viongozi wao pindi watapo shindwa kutimiza matakwa ya dhamana za nafasi walizo pewa.

4. Atajenga bunge imara lenye uwezo wa kumuwajibisha hata yeye mwenyewe pindi atapo kiuka katiba ya nchi aliyo apa kulinda na kuitetea bila ya woga maana yeye huyo atakuwa mzalendo wa kweli.

5. Atakuwa ni mtu mwenye kuwa unganisha watu ili taifa liwe na watu wamoja wanao piginia maslahi ya taifa lao kwa vitendo.

6. Ata hakikisha wana nchi wote wanapata mgao sawa wa keki ya taifa bila kujali dini zao kabila rangi elimu na itikadi za vyama vyao. Kwa ama kutoa baadhi ya huduma za jamii bure kabisa maana kwa nchi yetu ni watawala pekee tena wenye mishahara mikubwa ndio huzipata huduma hizi bure kabisa kitu ambacho hakikubaliki.

7. Hato tumia kinywa chake kupandikiza chuki dhidi ya wanao mkosoa maana njia bora ya mwanadamu kujirekebisha ni kukosolewa na wengine wanapo ona umekosea.

8. Ataruhusu ukaguzi huru wa taasisi za serikali ikiwa ni pamoja na ofisi yake ili kuwajengea imani wasadizi wake katika majukumu yao kwa kuwa taswira huru ya kujifunzia uzalendo. Maana ni vigumu kuhubiri imani kama wewe siyo mwamini. Na hili litawezekana tu kama raisi mwenyewe ni mzalendo.

9. Atawasemehe wafungwa wote maana ameamua kuijenga tanzania huru mpya na yenye maono mkakati. Maana hato ruhusu matajiri wasamehewe kwa kurudisha fedha walizo iba na kuwaacha wezi wa kuku wafie gerezani wakati wanauwezo wa kurudisha kuku na mahindi waliyo iba. Hapa atawaacha tu wale walio fungwa kwa makosa ya mauwaji maana katu roho ya mtu hairudishwi.

10. Atazifanya mahakama kuwa huru ili yeyote awaye yote anapo pata tuhuma zozote basi ahukumiwe kwa makosa aliyo yatenda na si kwa amri ya mtu yeyote kutoka katika jamuhuri ya muungano wa tanzania. Maana kila mtu huwajibika kwa makosa yake na si ya mtu mwingine.

11. Atazipa uhuru taasisi za dini zote mahali ambapo watu hulelewa kiroho na kimwili ili kujenga taifa la watu waadirifu na si kuwazuiya viongozi wa dini kukemea maovu badala yake kuwa tia nguvu na kuwapa uhuru ili taifa la mungu libarikiwe na kufana katika yote.

12. Raisi mzalendo kwa makusudi atayapunguza majukumu yake ya uteuzi na kuandaa utaratibu bora wa kikatiba wa kuwapata viongozi wa tasisi za serikali kitu kitakacho wafanya viongozi hao wawajibike moja kwa moja kwa wana nchi na sio kwa raisi aliye wateua.

13. Hato ruhusu kwa hali yeyote ile watu wamwite mtukufu raisi maana utukufu unayeye aliye ziumba mbingu na nchi hivyo hapana mtakatifu wala mkamilifu duniani.

14. Atayeweza ipiga vita rushwa kwa vitendo na si kupunguza idadi ya wala rushwa kwa kuwaacha wachache wakinufaika kwa kaulimbiu rushwa ni adui wa haki.

15. Hato ruhusu raia yeyote kupotea ,kuteswa wala kukatishwa uhai wake kwa misingi yoyote maana atajenga jeshi imara lkwa ulinzi wa raia na mali zake. Maan mtu mmoja katika nchi anathamani kubwa kuliko tani kadhaa za madini ya tanzanite na damu yake ni ya thamani kwenye uso wa nchi na katika maskani ya mungu.

16. Atajenga taasisi huru za habari na vyombo vya habari zenye kuleta tija latika taifa ili watu wake wawe ni wenye kujuzwa na yeye kupata taarifa kwa wakati sahihi na za uhakika. Ata heshimu mawazo ya wana habari kama chombo muhimu kwa moyo na ustawi wa taifa letu.

Nawewe unaweza ongeza sifa za raisi mzalendo ataye kuja. Mungu atupe mri ili siku zijazo tukiwa hai wazee au vijana tumuone raisi mzalendo kwa mara ya kwanza katika nchi yetu.

14._______________________

15._______________________

16. _______________________

17. ________________________

18._________________________

Je tanzania imewahi kupata raisi mzalendo?

Chilemba wamela pamputi.
__________________________
 
Kwa namna ambavyo nchi yetu imekuwa ikiendeshwa kwa miaka ya hivi karibuni, hapana shaka yoyote kwamba bado tuna safari ndefu saana.

Na laiti kwamba Tanzania ikija pata raisi mzalendo basi tutegemee yale yaliyo wahi kutokea kwa jirani zetu wa zambia.

Nina imani kabisa ukifika wakati tukimpata raisi mzalendo atafanya yafuatayo.

1. Kwa kuamini katika uwajibikaji wa kitasisi na nguvu za kitaasisi, Raisi mzalendo asiye na chembe chembe za rushwa, atabadili katiba na kuzipa nguvu taasisi zote muhimu zinazo shikilia moyo wa nchi.

2. Kwa kuto kuhofia kuwajibishwa na yeye kwasababu ni mzalendo kwelikweli basi hato sita kuwa chukulia hatua watangulizi wake wote walio onekana kuikanyaga katiba na kujinufaisha kupitia ofisi za uma.

3. Atajenga mifumo imara ya kidemokrasia itayo pelekea wananchi kuwa na nguvu za kuwachaguwa na kuwa kataa viongozi wao pindi watapo shindwa kutimiza matakwa ya dhamana za nafasi walizo pewa.

4. Atajenga bunge imara lenye uwezo wa kumuwajipa hata yeye mwenyewe pindi atapo kiuka katiba ya nchi aliyo apa kulinda na kuitetea bila ya woga maana yeye huyo atakuwa mzalendo wa kweli.

5. Atakuwa ni mtu mwenye kuwa unganisha watu ili taifa liwe na watu wamoja wanao piginia maslahi ya taifa lao kwa vitendo.

6. Ata hakikisha wana nchi wote wanapata mgao sawa wa keki ya taifa bila kujali dini zao kabila rangi elimu na itikadi za vyama vyao. Kwa ama kutoa baadhi ya huduma za jamii bure kabisa maana kwa nchi yetu ni watawala pekee tena wenye mihahara mikubwa ndio huzipata huduma hizi bure kabisa kitu ambacho hakikubaliki.

7. Hato tumia kinywa chake kupandikiza chuki dhidi ya wanao mkosoa maana njia bora ya mwanadamu kujirekebisha ni kukosolewa na wengine wanapo ona umekosea.

8. Ataruhusu ukaguzi huru wa taasisi za serikali ikiwa ni pamoja na ofisi yake ili kuwajengea imani wasadizi wake katika majukumu yao kwa kuwa taswira huru ya kujifunzia uzalendo. Maana ni vigumu kuhubiri imani kama wewe siyo mwamini. Na hili litawezekana tu kama raisi mwenyewe ni mzalendo.

9. Atawasemehe wafungwa wote maana ameamua kuijenga tanzania huru mpya na yenye maono mkakati. Maana hato ruhusu matajiri wasamehewe kwa kurudisha fedha walizo iba na kuwaacha wezi wa kuku wafie gerezani wakati wanauwezo wa kurudisha kuku na mahindi waliyo iba. Hapa atawaacha tu wale walio fungwa kwa makosa ya mauwaji maana katu roho ya mtu hairudishwi.

10. Atazifanya mahakama kuwa huru ili yeyote awaye yote anapo pata tuhuma zozote basi ahukumiwe kwa makosa aliyo yatenda na si kwa amri ya mtu yeyote kutaka kati jamuhuri ya muungano wa tanzania. Maana kila mtu huwajibika kwa makosa yake na si ya mtu mwingine.

11. Atazipa uhuru taasisi za dini zote mahali ambapo watu hulelewa kiroho na kimwili ili kujenga taifa la watu waadirifu na si kuwazuiya viongozi wa dini kukemea maovu badala yake kuwa tia nguvu na kuwapa uhuru ili taifa la mungu libarikiwe na kufana katika yote.

12. Raisi mzalendo kwa makusudi atayapunguza majukumu yake ya uteuzi na kuandaa utaratibu bora wa kikatiba wa kuwapata viongozi wa tasisi za serikali kitu kitakacho wafanya viongozi hao wawajibike moja kwa moja kwa wana nchi na sio kwa raisi aliye wateua.

13. Hato ruhusu kwa hali yeyote ile watu wamwite mtukufu raisi maana utukufu unayeye aliye ziumba mbingu na nchi hivyo hapana mtakatifu wala mkamilifu duniani.

14. Atayeweza ipaiga vita rushwa kwa vitendo na si kupunguza idadi ya wala rushwa kwa kuwaacha wachache wakinufaika kwa kaulimbiu rushwa ni adui wa haki.

Nawewe unaweza ongeza sifa za raisi mzalendo ataye kuja. Mungu atupe mri ili siku zine tukiwa hai wazee au vijana tumuone raisi mzalendo kwa mara ya kwanza katika nchi yetu.

14._______________________

15._______________________

16. _______________________

17. ________________________

18._________________________

Je tanzania imewahi kupata raisi mzalendo?

Chilemba wamela pamputi.
__________________________
mzalendo zaidi ya Magufuli hajawahi na haji kutokea
 
Itachukua miaka 50 hadi 100 kuja kupata Rais bora kama Magufuli ni Mzalendo mwenye historia itakayokumbukwa vizazi hadi vizazi anaweka na ataacha alama kwenye Taifa hili alama isiyofutika atakumbukwa vizazi hadi vizazi uwezo wa akili zake ni mkubwa sana
 
naunga mkonyo mkojo hoja
 
Tumempata Mzalendo Magufuli

Mafisadi kila kona yanahaha sasa
Ufisadi upi umeisha? Awamu hii kuna ufisadi kuliko awamu zote hata Deni la Taifa limepaa mara Dufu kuliko Tawala za huko nyuma, mtukufu kamtoa CAG bora wa kiwango na sasa kapachika CAG wa kufunika ufisadi wao wote. Ununuzi wa Ndege kwa cash upo upigaji wa kutisha, ujenzi chatoa Airport, reli bwawa la umeme flyover kote huko wanapiga 10% na kampuni zao binafsi ndiyo zina supply’ vifaa vyote wanakula kwa njia kibao
 
Hakuna serikali ya hivyo duniani
Yaani hakuna Serikali kama hii ya kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani kwenye chaguzi mbalimbali? au hakuna kama Serikali kama hii Duniani inayobadilo CAG kienyeji? au hakuna Serikali kama hii Ndege zinanunuliwa kwa cash na hesabu zake haziruhusiwi kukaguliwa na CAG mwenye weledi mkubwa? au hakuna Serikali kama hii Duniani inayoingilia uhuru wa mahakama na kuzuia mikutano ya siasa kwa njia haramu.
 
Back
Top Bottom