Siku sita za Ushindi wa Kishindo-31/10/2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku sita za Ushindi wa Kishindo-31/10/2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mp Kalix2, Oct 24, 2010.

 1. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,212
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  Nashauri Meneja wa kampeni wa Chadema na timu mzima ya mapambano ya kukomboa Tz, kufanya jitihada kubwa ya kusambaza haraka iwezekanavyo ndani ya hizi siku sita zilizobaki CD/video ya mahojianao ya Dr Slaa kwnye ITV kwa Nchi mzima hasa kwa mawakala ,wajumbe wa nyumba kumi wa chadema,madiwani watarajiwa,wabunge watarajiwa na pia kuziuza kwenye kampeni zinazoendelea ilikufikisha ujumbe wa ukombozi kwa haraka na ufasaha mkubwa kwa wale ambao hawakufanikiwa kuona live.
  Ieleweke kuwa si-maeneo mengi ya Nchi yetu ujumbe kuwa DR angekuwa ITV live umepata kufika na pia maeneo mengine ITV haishiki hasa Vijijini na hakuna Umeme.Katika maeneo haya watu huonyesha Video tu kwa kutumia jenereta, hivyo wajumbe wanaweza kupata frusa ya kuonyesha mahajiano hayo ili kusaidia kupanua uelewa wa watu ili 31/10/2010 kufanya uamuzi mzuri na sahihi.

  Na yasema haya kwa sababu ya darasa kubwa aliyotoa Rais wangu mtarajiwa pale Moven Pink na ambayo ni muhimu kwa watanzania wengine kuipata kabla ya 31/10/10.

  Mungu Ibariki Tz
  Mungu wa bariki waTz
  Mungu Ibariki Africa.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  swadata
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ujumbe huu apelekewe BAREGU
  ni muhimu kuwa na last minute taticks za kulinda yale tuliyoyajenga for loong time since tulivyoweka nia ya kuikomboa tanzania kutoka kwa mkoloni CCM
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ziuzwe bei nafuu ili watu wengi wanufaike. waweke kwenye cds za kawaida za shs miatano kisha ziuzwe kwenye kila kampeni ya mbunge au diwani wa ccm anavyokampeni. Pia kama inawezekana sisi tulioko online tusaidie kutuma links za vids kwenye bulk emails kwa kuforward
   
 5. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe 100%. CHADEMA (Campaign meneja) toeni nakala za audio CD, video CD, DVD, VHS, na kuzisambaza haraka iwezekanavyo kwa wadau wote. Wasianeni na wagombea wenu kujua namna wanavyoweza kufikisha ujumbe. Kwa kipindi kilichobaki mnaweza kuongea na local TV/radio stations ktk baadhi ya mikoa ili kurusha matangazo. Vile vile magari ya matangazo yaweza kutumika. Nashauri zipatikane nakala za mahojiano ili tuziambaze kwa njia ya mtandao kwa wenye mapenzi mema na nchi hii.

  Kwa wote wanoitakia mema nchi hii mahojiano ya jana yalikuwa kiwango cha juu sana kwa viwango vyovyote vya kimataifa. Hakukuwa na shopping list ya consumer items.... Oh tutajenga barabara, visima, kupandisha hadhi hospitali, etc. Yale yote ambayo ni majukumu ya msingi ya serikali hayakutumiwa kama agenda ya kujinadi. :thumb:
   
 6. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  asante maana ushauri wako ni wa ukombozi,nadhani hilo suala litafanyiwa kazi maana timu ya ukombozi inafanya kazi kubwa kuhakikisha tanzania iko katika mikono salama ya dk slaa
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  kwa nyongeza, mimi nilidhani katika muda wa wiki mbili kabla ya kampeni, CHADEMA wangeongeza idadi ya mabango ya mgombea urais nchi nzima. Bado kuna vijiji ambavyo watu wanamsikia tu Slaa lakini hawajawahi kuiona hata picha yake. Ili kupunguza usumbufu wakati wa kupiga kura, ni vizuri watu wangeona picha za Mheshimiwa Slaa mapema ili iwawie rahisi siku ya uchaguzi.
   
 8. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr hongera kwa kusema sana jana,natka kukuhakikishia kuwa hauwezi kuwa raisi wa nchi kwa kuwa unaonesha kuwa na udini na visasi,pia hauna mtaadao wa kutosha hata kama mikutano yako inajaa ni kwa kuwa watu wanahamu ya kusikia maneno yako.
   
 9. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  I agree with you all ule mdahalo ulikuwa kwenye viwango vya juu sana,kijiji nilichotoka jamazangu walijitahidi kuwa karibu na runinga yao, lakini ITV hawakuipata. Nakubaliana na MP KaliX2 kuwa CDs zipatikane kwa haraka tupeleke kwa wale ambao hawakufikiwa, mm ningepeleka kijijini kwangu kwenye kata yangu haraka, wenye kufahamu namna ya kuwasiliana na Baregu watusaidie jamani.
   
 10. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MP Kalix2...my brother i had the same concept in my mind, kwamba kuna haja ya kurecord na kutuma hizo CD VHF kwa wananchi ambao kwa hakika wanaweza kuwa hawakupata taarifa za kuwepo kwa mdahalo wa huyu Shujaa wetu Dr. wa Ukweli Slaa. Personally i wish i could have supported this through my personal money atleast to send them to my homeland, huko kijijini jirani kabisa na Zitto Kabwe. The thing nimetoka shule recently na imagine pamoja na uzoefu wangu kazini wa 4 years eti kila nikiomba job nafuatilia nagungua kumbe ule mfumo wa ananijua nani unaendelea tena kwa kasi kubwa sana " Hivyo kwa kifupi ni majeruhi wa utawala mbovu kabisa kuwahi kutokea hapa nchini". Lakini all in all CHADEMA should do this soon as possible ili ujumbe ufike haraka iwezekanavyo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema, Mungu mbariki rais wetu mtarajiwa Dr. Wilbroad Peter Slaa.
   
 11. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Majimbo 70 moto Send to a friend Sunday, 24 October 2010 08:49 0diggsdigg


  [​IMG] Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Mrisho Kikwete

  Waandishi wetu, Dar na mikoani
  WAKATI kampeni za urais na ubunge zikielekea ukingoni, mvutano mkubwa umeibuka katika baadhi ya majimbo nchini kiasi cha kutoa ishara kuwa sura ya Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano inaweza kubadilika.
  Bunge la Tisa lililovunjwa mwishoni mwa mwezi Julai lilikuwa na wabunge 205 kutoka chama tawala cha CCM, huku CUF ikifuatia kwa kuwa na wabunge 19, Chadema watano, UDP mmoja na TLP mmoja ambaye hata hivyo hakumaliza kipindi chake baada ya kufariki ajalini.
  Lakini baada ya takriban siku zaidi ya 60 za kampeni na kujinadi, hali inaonekana kuwa itabadilisha muundo wa Bunge hilo kutokana na kuwepo dalili kuwa vyama vya upinzani vinaweza kuingiza idadi kubwa zaidi.
  Hali hiyo ilishatabiriwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alisema kuna uwezekano Bunge lijalo likawa na wabunge takriban 100 kutoka vyama vya upinzani, utabiri ambao ulienda sawa na matokeo ya tafiti za Redet na Synovate, ambayo ilieleza bayana kuwa wabunge 132 hawachaguliki na wengi wao ni kutoka chama hicho tawala na hivyo kuna uwezekano wa kutorudi kwenye chombo hicho cha kutunga sheria.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa Chadema ndiyo inayoongoza kwa kuibana CCM kwenye majimbo mengi ya Tanzania Bara ikifuatiwa na CUF, ambayo ngome yake kubwa ni visiwani Zanzibar na kwenye baadhi ya mikoa ya Bara, na kufuatiwa na NCCR-Mageuzi na TLP.
  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili unaonyesha kuwa kwenye majimbo yapatayo 50 ya Bara, CCM imebanwa vikali na vyama hivyo vitano, ukiachilia majimbo ambayo yalishikiliwa na upinzani kwenye Bunge la Tisa.
  Ukijumlisha na majimbo ambayo CUF ina uhakika nayo kisiwani Pemba, uwezekano wa wapinzani kuwa na idadi kubwa ya wabunge unaonekana kuwa mkubwa.

  Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa upinzani huo umesababisha wagombea urais wa vyama hivyo kulazimika kutembelea baadhi ya majimbo mara mbili ili kuweka sawa mambo, huku CCM ikiathiriwa kwa kiasi kikubwa na makundi yaliyozalishwa wakati wa kura za maoni na maamuzi ya halmashauri kuu kubatilisha ushindi kwenye baadhi ya majimbo.
  Tayari mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete na wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wameshatembelea mkoa wa Mwanza mara tatu kuweka mambo sawa kutokana na upinzani mkali. Kikwete anatarajiwa kutua Geita leo ikiwa ni mara yake ya tatu. Mkoani Kigoma, majimbo yanayoonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM ni Kigoma Kusini ambako David Kafulila ambaye alijiondoa Chadema baada ya kuachishwa kazi makao makuu, anaonekana kutoa upinzani mkali kwa wagombea wa CCM na Chadema.

  Hali haionekani kubadilika kwenye Jimbo la Kigoma Kaskazini ambako Zitto Kabwe wa Chadema anaonekana kuteka nyoyo za wananchi baada ya kulitumikia Bunge kwa mafanikio miaka mitano iliyopita. Zitto anaonekana kuwaacha kwa mbali wagombea wa CUF na CCM ambao wanawania kumuondoa mwanasiasa huyo kijana.
  NCCR-Mageuzi ina nguvu kubwa kwenye Jimbo la Muhambwe ambako mgombea wake, Felix Mkosamali anapewa nafasi kubwa dhidi ya waziri wa zamani, Arcado Ntagazwa wa Chadema na Jamal Abdallah wa CCM.

  NCCR ambayo imeshawahi kushika Jimbo la Kigoma Mjini, pia inaonekana kuwa na mizizi Kasulu Vijijini ambako mgombea wake, Zaituni Buyogela anaonekana kutoa upinzani mkali dhidi ya Chadema na CCM, huku Kasulu Mjini, Moses Machali wa NCCR akipeleka upinzani mkali dhidi ya mgombea wa CCM, Neka Raphaeli Neka.
  Mkoa wa Kagera Majimbo yanayoonekana kuwa na upinzani mkali ni Bukoba Mjini, Biharamulo, Karagwe na Ngara ambako wagombea wa NCCR na Chadema wameweka upinzani mkali dhidi ya CCM.

  Wagombea wa upinzani katika majimbo haya na vyama vyao kwenye mabano ni Sam Ruhuza (Ngara), NCCR Mageuzi, Alfred Lwakatare (Bukoba Mjini, Chadema), wakati Jimbo la Karagwe, wagombea wa NCCR, Peterson Mshenyera na Deus Kahangwa wa Chadema wanaonekana kuwa na upinzani mkali.
  Mkoa wa Rukwa Mkoani Rukwa tayari Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshapita bila ya kupingwa, lakini wagombea wenzake wa CCM wana kazi kubwa kwenye majimbo ya Mpanda Kati na Nkasi Kaskazini na Sumbawanga Mjini ambako wagombea wa Chadema wanapewa nafasi kubwa ya kushinda. Wagombea wa Chadema kwenye majimbo hayo ni Said Alfi wa Jimbo la Mpanda Kati, Kessy Sidi (Nkasi Kaskazini) na Norbet Yamsebo (Sumbawanga Mjini).
  Mkoani Mwanza
  Licha ya CCM kuita viongozi wake wa kitaifa, akiwemo mgombea urais Jakaya Kikwete ambaye leo anategemewa kutua tena Geita kutuliza upepo baada ya Dk Slaa kumaliza ziara ya tatu wiki iliyopita, hali bado si shwari. Ziara hizo za wagombea hao wa urais zinatokana na ukweli kuwa mkoa huo una watu wengi wengi, huku ushindani ukiwa ni mkubwa. Majimbo yenye mvutano mkali ambayo wagombea urais hao wamekuwa wakiyazungukia kila mara ni Nyamagana ambako mbunge wa CCM, Lawrence Masha amekaliwa kooni Ezekiel Wenje wa Chadema.
  Changamoto aliyoiweka Wenje iliongezeka baada ya kupita kikwazo cha uraia ambacho mpinzani wake, Masha alikiweka kwa Tume ya Uchaguzi akitaka aenguliwe.

  Awali Wenje alienguliwa na Tume ya Uchaguzi wilayani lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilibatilisha maamuzi hayo na kumrejesha baada ya Wenje kukata rufani. Jimbo jingine ambalo limetajwa kuwa na mvutano mkali ni Kwimba ambapo mvutano upo kati ya Shanif Mansoor wa CCM na Leticia Nyerere wa Chadema. Katika jimbo la Buchosa, mvutano umeongezeka kati ya mgombea wa CCM, Dk Charles Tizeb na mgombea wa Chadema, Kaswahili Martin ambao wameonekana kuchuana vikali, kiasi cha mgombea wa CCM kukaririwa akilalamika kuwa chama chake kimeathiriwa na makundi yaliyotokana na kura za maoni.
  Hata hivyo, CCM inaonekana kuwa na mteremko kwenye majimbo ya Busanda na Geita Mjini ambako wagombea wake Donard Max na Lolencia Bukwimba wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kurejea Dodoma. Max anachuana na Rogath Joseph Ilengawa wa Chadema Jimbo la Geita Mjini wakati Bukwimba anapambana na Finias Magesa wa Chadema ambaye alimtoa jasho mwanachama huyo wa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka juzi.
  Kwenye Jimbo la Magu, hali imeelezwa kuwa ya mvutano mkubwa baina ya mgombea wa UPDP, Lugongoteke Julius na mgombea wa CCM, Dk Festus Limbu.
  Mkoa wa Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro mchuano mkali upo kati ya Chadema na CCM isipokuwa jimbo la Vunjo. Kwenye jimbo hilo, yeyote kati ya John Mrema (Chadema), Chrispin Meela (CCM) na mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema anaweza kuibuka na ushindi kutokana na wote kukaribiana kwa kukubalika.

  Wachambuzi wa masuala ya kisiasa mkoani humo wanasema kuwa ushindani huo unaweza kumpa mwanya mgombea wa CCM kushinda kirahisi kwa kuwa wagombea wa upinzani wanaweza kujikuta wakigawana kura zinazoipinga CCM.
  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa ukiondoa majimbo ya Mwanga, Moshi Vijijini na Same Magharibi, lolote linaweza kutokea katika majimbo mengine ambayo wagombea wa CCM na Chadema wanachuana vikali.
  Philemon Ndesamburo wa Chadema bado anaendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwenye Jimbo la Moshi Mjini, huku mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiibuka kama mgombea mwenye nguvu kubwa kwenye Jimbo la Hai. Kwenye majimbo hayo mawili, CCM imelazimika kufanya kampeni mbili kwa wakati mmoja, huku ikiwa na kazi kubwa ya kuvunja makundi yaliyotokana na mchakato wa kura za maoni za ndani ya chama hicho.
  Wagombea wa CCM kwenye Jimbo la Rombo, Basil Mramba na Aggrey Mwanry (Siha), Anne Kilango (Same Mashariki), wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea wa Chadema. Joseph Selasini kuchuana na Mramba (Rombo), Naghenjwa Kaboyoka kuchuana na Kilango (Same) huku Mwanry akichuana na Humprey Tuni.
  Mkoa wa Dar es Salaam Mkoa wa Dar es salaam una rekodi ya kuwa na wabunge wa upinzani kwenye majimbo ya Temeke, Kigamboni na Ubungo, lakini hali sasa inaonekana kubadilika kutokana na vyama hivyo kujiimarisha kwenye majimbo mengine ya Kawe, Segerea na Ukonga.

  John Mnyika, ambaye alipambana vikali na Charles Keenja kwenye jimbo la Ubungo mwaka 2005 na kushindwa kwa kura chache, sasa anaonekana kuwa na nguvu zaidi akimtoa jasho mgombea wa CCM, Hawa Nghumbi sambamba na mgombea wa CUF, Julius Itatiro.
  Kwenye Jimbo la Kawe, mgombea wa CCM, Angela Kiziga anachuana vikali na mgombea wa Chadema, Halima Mdee, ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum kwenye Bunge la Tisa, pamoja na mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ambaye aliamua kugombea ubunge.

  Jimbo jipya la Segerea ambalo limetenganishwa na Ukonga, mbunge wa zamani wa Kishapu ambaye sasa amehamia Chadema, Fred Mpendazoe anachuana vikali na Makongoro Mahanga wa CCM ambaye alikuwa mbunge wa Ukonga kwa vipindi viwili. Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa wa CCM anapambana na James Chacha wa Chadema. Dk Faustine Ndugulile, ambaye alishinda kiti cha Jimbo la Kigamboni mwaka 2005 akiiangusha CUF, mwaka huu anapambana vikali na Anna Komu wa Chadema. Mkoa wa Arusha Mkoa wa Arusha kuna majimbo manne ambayo yanaonekana kuwa na mchuano mkali. Uchunguzi unaonyesha kuwa kadiri uchaguzi unavyokaribia, nguvu za wagombea wa upinzani dhidi ya wale wa CCM inazidi kuongezeka.
  Lakini CCM ina uhakika wa kushinda kwenye majimbo mengi, ikiwa imeshaliweka kibindoni Jimbo la Simanjiro ambako mgombea wake, Christopher Ole Sendeka amepita bila ya kupingwa. Jimbo la Karatu ambalo lilikuwa chini ya Dk Slaa kwa vipindi viwili, linaonekana linaweza kuendelea kuwa chini ya Chadema ambayo imemsimamisha Mchungaji Israel Yohana kukabiliana na upinzani unaonekana kuwa mdogo kutoka kwa Wilbard Lory wa CCM.
  Hali ni ngumu kwenye Jimbo la Arusha Mjini, ambako wafuasi wa Chadema na CCM wamekuwa wakipambana mara kwa mara. Chadema imemsimamisha Godbless Lema wakati CCM imemsimamisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Batilda Burian. Siasa za makundi na ukabila ndani ya CCM, zinaelezwa kuwa zinamsumbua sana mgombea wa chama hicho Dk Burian.

  katika majimbo la Arumeru Mashariki na Magharibi, wagombea wa CCM, Naibu Waziri Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari na Godluck Medeye wamebanwa na wagombea wa Chadema.
  Katika jimbo la Arumeru Magharibi, mgombea wa Chadema, Mathias Ole Kisambo akimchuana vikali na Medeye.
  Mkoa wa Manyara Kwenye Jimbo la Kiteto, mchuano mkali upo kati ya mgombea wa CCM, Benedict Nanyaro na mgombea wa Chadema, Victor Kimesera.
  Jimbo la Mbulu, mgombea wa CCM ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Phillip Marmo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Chadema, Mustapha Akoonay. Marmo ni mbunge kwa miaka 25 sasa katika jimbo hilo. Jimbo la Babati Vijijini, Jitu Soni wa CCM, Francis Philipo wa Chadema, Babati Mjini yuko Kisyeri Chambili wa CCM na Paulina Jakuru wa Chadema.
  Jimbo la Hanang mchuano ni mkali kati ya Mary Nagu CCM na Rose Kamili wa Chadema.
  Mkoa wa Ruvuma Mkoani Ruvuma majimbo ambayo yana mchuano mkali ni Mbinga Mashariki ambako mgombea wa Chadema, Erenius Ngwatula anapambana vikali na Gaudence Kayombo wa CCM. Jimbo jingine ambalo lina ushindani mkali kutoka ni Tunduru Kaskazini ambako mgombea wa CCM, Mhandisi Ramo Makani anachauana vikali na Mazee Rajab wa CUF.
  Mkoa wa Mbeya
  Wapinzani nguvu yao inaonekana kuwa kubwa safari hii kutokana na Chadema na TLP kusimamisha wagombea wake.
  Kwenye Jimbo la Lupa, mgombea wa TLP, Sunday Sanga anaonekana kutumia mpasuko ndani ya CCM kushinda akinapambana vikali na mbunge wa sasa Victor Mwambalaswa.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr 2, anaonekana kupania kumaliza enzi za Benson Mpesya wa CCM ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi viwili. Mpesya alikuwa mwalimu wa MRTWO ambaye anawania kwa tiketi ya Chadema. Sambwee Shitambala wa Chadema ambaye aliondolewa kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini kutokana na makosa yaliyobainika kwenye kiapo chake, anaonekana kujizatiti kukabiliana na Mch Lackson Mwajali wa CCm ambaye alishinda kwenye uchaguzi huo.
  Kwenye jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) anapambana na Mtela Mwampamba wa Chadema wakati Mbozi Magharibia, Dk Luca Siayame (CCM) anapambana na mgombea wa Chadema, David Silinde. Kwenye jimbo la Mbarali ushindani unaonekana kuwa kati ya Idawaya Kazamoyo wa Chadema na Dickson Kirufi (CCM). Mkoa wa Tanga Mkoani Tanga, ushindani uko kwenye Jimbo la Mlalo ambako mgombea wa CCM, Brigedia mstaafu, Hassan Ngwilizi anapambana na Charles Kagonji wa Chadema huku mgombea wa CUF, Gogla Shechonge akitia changamoto.
  Jimbo la Pangani ushindani ni baina ya mgombea kwa tiketi ya CUF,Omari Ali Mohamed (Masomaso) na wa CCM Salehe Pamba, wakati kwenye jimbo la Korogwe Mjini ni baina ya Kalistus Shekibaha wa Chadema na Yussuph Nassir wa CCM. Jimbo la Tanga ni baina ya Omari Nundu wa CCM na Mussa Mbakouk wa CUF. Mkoa wa Shinyanga
  Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo anaonekana kuongoza harakati za kurejea bungeni kwa kutumia Jimbo la Bariadi Mashariki, wakati kwenye Jimbo la Bukombe ambako Prof Kulikoyela Kahigi wa Chadema anachuana vikali na Emmanuel Luhaula wa CCM.
  Katika jimbo hili mgombea wa urais wa CCM, Jakaya Kikwete alipata wakati mgumu hivi karibuni kumnadi mgombea wake baada ya wananchi kumkataa. Jimbo la Shinyanga Mjini, Philipo Shilembi wa Chadema amemkalia vibaya Steven Masele wa CCM huku jimbo la Maswa Magharibi John Shibuda wa Chadema anachuana vikali na Robert Kisena wa CCM. Ushindani wao umesababisha wafuasi wao kupambana mara kwa mara na kusababisha dereva wa Kisena kuuawa katika vurugu zilizotokea wiki iliyopita. Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbyi wa Chadema anachuana na vikali na Peter Bunyongoli wa CCM huku katika jimbo la Bariadi Mashariki, John Cheyo wa UDP anapambana na Martin Makondo wa CCM.
  Katika jimbo la Meatu Meshack Opurukwa wa Chadema na Salumu Khamis CCM wanapambana vikali. Lindi na Mtwara Majimboa mabayo yana ushindani mkubwa mkoani Lindi ni Kilwa Kusini ambako Suleimani Bungala wa CUF anachuana vikali na Ramadhan Madabida wa CCM, Lindi mjini Salumu Barwany wa CUF, Abdulaziz Mohamed wa CCM, Mtwara vijijini Chikamba Wanainuka wa CUF na Hawa Ghasia CCM,Newala Hakika Maarifa CUF na Kapt George Mkuchika wa CCM.
  Mkoa wa Mara

  Kattika jimbo la Musoma Mjini hali inaonyesha mtoto wa muasisi wa CCM Mwalimu Julius Nyerere, Vicent Nyerere anayegombea kupitia Chadema amekuwa akimuendesha puta mgombea wa CCM, Mathayo Mathayo hali ambayo imesababisha wafuasi wa vyama hivyo kukatana mapanga. Mvutano huu ni uliopo katika Jimbo la Serengeti, ambako wagombea wanaochuna ni Dk Steven Kebwe wa CCM ambaye anapambana na Marwa Rioba wa Chadema.
  Kivumbi kingine kipo katika jimbo la Tarime ambako CCM kupitia mgombea wao Nyambari Nyangwine wameamua kulirejesha jimbo hilo baada ya kulipoteza muda mrefu huku Chadema nao wakisaka kuendelea kulishikilia kwa kutumia mgombea wao, Mwita Waitara. Mkoa wa Iringa
  Jimbo la Iringa Mjini ndilo linaonekana kuwaka moto kwa Monica Mbega wa CCM akichuana vikali na Mchungaji Peter Msigwa Chadema na Mariamu Mwakingwe wa NCCRMageuzi akitoa chagamoto. Katika Jimbo la Njombe Kaskazini, mgombea wa CCM, Deo Sanga anapambana na Alatabga Nyagawa wa Chadema wakati jimbo la Njombe Magharibi Thomasi Nyimbo wa Chadema anaonyeshana kazi na Gerson Lwenge wa CCM.

  Imeandaliwa na Joyce Mmasi, Dar; Frederick Katulanda, Mwanza; Daniel Mjema, Moshi; Mussa Juma, Arusha; Joyce Joliga, Songea; Brandy Nelson , Mbeya; Burhan Yakub, Tanga na Tumiani Msuwoya, Iringa.
   
 12. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  We as Tanzanian '"together we can"" tukumbuke kutunza shahada zetu.
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Tunashukuru kwa uchambuzi makini. Iyo ndo kazi ya uandishi.
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tafuta matibabu ya kichwa nadhani si kizuri
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mungu atupe uhai
   
 16. K

  King kingo JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jamani tukiwaachia kila kitu Chadema mambo yanaweza kuwa magumu upande wetu, kama unajua kuna sehemu hawajafanikiwa kuona mdahalo na unafahamu unaweza leta mabadiliko basi fanya juhudi binafsi za kutafuta CD/Tape na kuwapelekea jamaa zako hivi ndivyo tunaweza kufanikiwa kwani tukumbuke sote tuko kwenye mapambano - PLAY YOUR PART
   
Loading...