Siku Rais Magufuli alipokuwa MC wa Dr. Dau

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,521
2,000
Tarehe 19 April 2016 itakumbukwa kama tarehe ya kihistoria kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla.
Ni siku ambayo Mheshimiwa Rais Magufuli alipofungua rasmi daraja la Kigamboni.

Kwangu mimi siku hiyo sitaisahau kwani ni siku ambayo kulitokea muujiza mkubwa kwa wenye kufikiri.
Wageni waalikwa walikuwa wengi, mawaziri, mabalozi mbalimbali, wafanyabiashara na watu maarufu kadha wa kadha, walala hai na walala hoi (kwa sauti ya profesa Shivji) walikuwepo kuhudhuria uzinduzi huo wa daraja la kihistoria kwa nchi yetu.

Cha kushangaza, kati ya watu maarufu waliopoteza usingizi wao kufanikisha mradi huo ufanikiwe ni Rais Magufuli pekee, ambae wakati wa utekelezaji wa mradi huo alikuwa ni Waziri wa Ujenzi, ndiye alipewa fursa ya kuzungumza.

Dr. Ramadhan Dau ambae alikuwa ni kinara wa utekelezaji wa mradi huo adhimu na adimu alikuwa mualikwa lakini hakuwepo katika listi ya wazungumzaji siku hiyo (kwanini? Mimi sielewi).

Tunapanga yetu lakini Allah ni mbora wa wapangaji wote.

Ilipofika zamu ya Rais kuongea, basi naam yeye ndiye aligeuka MC na ghafla akamtangaza Dr. Ramadhan Dau asimame kuongea machache kuhusu ufanikishaji wa ujenzi wa daraja hilo.

Hakika huo ulikuwa ni muujiza mkubwa sana. Rais wa nchi ghafla kugeuka MC wa Dr. Ramadhan Dau, ambae siku hizo hizo alikuwa akijadiliwa nchi nzima kwa tuhuma za uongo na uzushi.
Hakika u MC huo wa Rais Magufuli siku hiyo ukakata mzizi wa fitina kwa Dr. Ramadhan Dau.

Hongera Rais, hongera Dr. Dau.

Haijapata kutokea.

mikeimani

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
3,037
2,000
Daraja ni muhimu sana. Lakini vitu vingi ni muhimu sana. Kama hakukuwa na ufisadi katika ujenzi wa daraja hilo hongera nyingi Dr Dau. Ni vipi kama unajenga hospitali ambayo kila mtu anaihitaji lakini gharama za ujenzi ni mara kadhaa ya bei halisi?

Daraja ni la muhimu kuliko magorofa ya nssf yaliyojengwa Kwa bei mbaya na yasiyo na wapangaji. Hela za watu zilitumika ovyo kwenye kujenga magorofa yale, likely ili wapate cha juu
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,729
2,000
Tarehe 19 April 2016 itakumbukwa kama tarehe ya kihistoria kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla.

Ni siku ambayo Mheshimiwa Rais Magufuli alipofungua rasmi daraja la Kigamboni.

Kwangu mimi siku hiyo sitaisahau kwani ni siku ambayo kulitokea muujiza mkubwa kwa wenye kufikiri.

Wageni waalikwa walikuwa wengi, mawaziri, mabalozi mbalimbali, wafanyabiashara na watu maarufu kadha wa kadha, walala hai na walala hoi (kwa sauti ya profesa Shivji) walikuwepo kuhudhuria uzinduzi huo wa daraja la kihistoria kwa nchi yetu.

Cha kushangaza kati ya watu maarufu waliopoteza usingizi wao kufanikisha mradi huo ufanikiwe ni Rais Magufuli pekee ambae wakati wa utekelezaji wa mradi huo alikuwa ni Waziri wa Ujenzi ndiye alipewa fursa ya kuzungumza.

Dr. Ramadhan Dau ambae alikuwa ni kinara wa utekelezaji wa mradi huo adhimu na adimu alikuwa mualikwa lakini hakuwepo katika listi ya wazungumzaji siku hiyo (kwanini? Mimi sielewi).

Tunapanga yetu lakini Allah ni mbora wa wapangaji wote.

Ilipofika zamu ya Rais kuongea, basi naam yeye ndiye aligeuka MC na ghafla akamtangaza Dr. Ramadhan Dau asimame kuongea machache kuhusu ufanikishaji wa ujenzi wa daraja hilo.

Hakika huo ulikuwa ni muujiza mkubwa sana. Rais wa nchi ghafla aligeuka MC wa Dr. Ramadhan Dau ambae siku hizo hizo alikuwa akijadiliwa nchi nzima kwa tuhuma za uongo na uzushi.

Hakika u MC huo wa Rais Magufuli siku hiyo ukakata mzizi wa fitina kwa Dr. Ramadhan Dau.

Haijapata kutokea.
Kweli kabisa, kwa kweli kazi hiyo ya u mc ilimpendeza sana, nashauri kusiwe na haja ya kukodi ma mc ili kupunguza gharama
 
LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,269
2,000
Tarehe 19 April 2016 itakumbukwa kama tarehe ya kihistoria kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla.

Ni siku ambayo Mheshimiwa Rais Magufuli alipofungua rasmi daraja la Kigamboni.

Kwangu mimi siku hiyo sitaisahau kwani ni siku ambayo kulitokea muujiza mkubwa kwa wenye kufikiri.

Wageni waalikwa walikuwa wengi, mawaziri, mabalozi mbalimbali, wafanyabiashara na watu maarufu kadha wa kadha, walala hai na walala hoi (kwa sauti ya profesa Shivji) walikuwepo kuhudhuria uzinduzi huo wa daraja la kihistoria kwa nchi yetu.

Cha kushangaza kati ya watu maarufu waliopoteza usingizi wao kufanikisha mradi huo ufanikiwe ni Rais Magufuli pekee ambae wakati wa utekelezaji wa mradi huo alikuwa ni Waziri wa Ujenzi ndiye alipewa fursa ya kuzungumza.

Dr. Ramadhan Dau ambae alikuwa ni kinara wa utekelezaji wa mradi huo adhimu na adimu alikuwa mualikwa lakini hakuwepo katika listi ya wazungumzaji siku hiyo (kwanini? Mimi sielewi).

Tunapanga yetu lakini Allah ni mbora wa wapangaji wote.

Ilipofika zamu ya Rais kuongea, basi naam yeye ndiye aligeuka MC na ghafla akamtangaza Dr. Ramadhan Dau asimame kuongea machache kuhusu ufanikishaji wa ujenzi wa daraja hilo.

Hakika huo ulikuwa ni muujiza mkubwa sana. Rais wa nchi ghafla aligeuka MC wa Dr. Ramadhan Dau ambae siku hizo hizo alikuwa akijadiliwa nchi nzima kwa tuhuma za uongo na uzushi.

Hakika u MC huo wa Rais Magufuli siku hiyo ukakata mzizi wa fitina kwa Dr. Ramadhan Dau.

Haijapata kutokea.
ulitaka kumaanisha nini mkuu,tunahisi kuna kitu cha msingi umetaka kukiongea ila haujafikia malengo tukaelewa,go on mkuu..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom