Siku Rais Magufuli alipokuwa MC wa Dr. Dau

Tarehe 19 April 2016 itakumbukwa kama tarehe ya kihistoria kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla.
Ni siku ambayo Mheshimiwa Rais Magufuli alipofungua rasmi daraja la Kigamboni.

Kwangu mimi siku hiyo sitaisahau kwani ni siku ambayo kulitokea muujiza mkubwa kwa wenye kufikiri.
Wageni waalikwa walikuwa wengi, mawaziri, mabalozi mbalimbali, wafanyabiashara na watu maarufu kadha wa kadha, walala hai na walala hoi (kwa sauti ya profesa Shivji) walikuwepo kuhudhuria uzinduzi huo wa daraja la kihistoria kwa nchi yetu.

Cha kushangaza, kati ya watu maarufu waliopoteza usingizi wao kufanikisha mradi huo ufanikiwe ni Rais Magufuli pekee, ambae wakati wa utekelezaji wa mradi huo alikuwa ni Waziri wa Ujenzi, ndiye alipewa fursa ya kuzungumza.

Dr. Ramadhan Dau ambae alikuwa ni kinara wa utekelezaji wa mradi huo adhimu na adimu alikuwa mualikwa lakini hakuwepo katika listi ya wazungumzaji siku hiyo (kwanini? Mimi sielewi).

Tunapanga yetu lakini Allah ni mbora wa wapangaji wote.

Ilipofika zamu ya Rais kuongea, basi naam yeye ndiye aligeuka MC na ghafla akamtangaza Dr. Ramadhan Dau asimame kuongea machache kuhusu ufanikishaji wa ujenzi wa daraja hilo.

Hakika huo ulikuwa ni muujiza mkubwa sana. Rais wa nchi ghafla kugeuka MC wa Dr. Ramadhan Dau, ambae siku hizo hizo alikuwa akijadiliwa nchi nzima kwa tuhuma za uongo na uzushi.
Hakika u MC huo wa Rais Magufuli siku hiyo ukakata mzizi wa fitina kwa Dr. Ramadhan Dau.

Hongera Rais, hongera Dr. Dau.

Haijapata kutokea.


Huo u mc mie sijauona aisee
 
Back
Top Bottom