Siku nyingi tutaungwa mkono na wana CCM kutokea ndani ya chama chao

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Kwa hali ya mambo ilivyo ndani ya ccm , ni wazi kabisa kwamba wanachama wake wengi hawaridhishi na wanaburuzwa tu kama hawajielewi .

Siku zote binadamu hawezi kutendewa ubaya na akakaa tu kama zuzu , ni lazima uvumilivu utamshinda tu , zipo taarifa kwamba mbinu ya sasa si kuhama , bali ni kuhakikisha kwamba fito zinagombaniwa ndani kwa ndani , kwamba wasioridhika na yanayotendwa w...atatuunga mkono wakiwa humohumo .

Tulishasema tangu mapema , KUMPA UENYEKITI MTU AMBAYE HAKUWAHI HATA KUWA MJUMBE WA NYUMBA 10 ACHILIA MBALI KATIBU KATA , ni matatizo makubwa sana .

Sijawahi kuona kiongozi anayempuuza kila mtu akafanikiwa , huyu atakuwa wa kwanza
.
Mabadiliko namba 9 yaliyofanywa juzi Dodoma ndio kitanzi chenyewe .

Ni suala la muda tu .
 
Chama kina Nguvu sana, kina namna yake ya kumshughulikia Rais anaeziba Masikio

2005 baada ya Mtandao kutikisa na kuwa na nguvu kuliko CCM Hali iliyofikia Comred Kinana alionekana Takaraka japo ndie Mwnylt wa Kampeni yalifanyika yaliyofanyika Lowassa na Rostam wakawa hawapikiki Chungu kimoja na Rais na hatimae Chama kikarudi kushika hatamu

1984 Abdu Jumbe yalimkuta yaliyomkuta

1985 Nyerere alikuja na Mgombea wake Kawawa akaangukia Pua

Jakaya 2015 alikuwa na Mgombea wake akaangukia Pua

2005 Mzee Mkapa alikuwa kawaanda Sumaye na Dr. Kigoda akaangukia Pua

Dr. Salmeen alitaka kuongeza Muda akaangukia Pua

Magu Hana Ubavu wala akili za kuwazidi kina Nyerere na Jk lakin waliyfyata kwa Chama
 
Kama majority of CCM wataiunga mkono Chadema against JPM then utegemee Tanzania mpya? Kwa akili hizi CCM hawaondoki leo wala kesho ....
 
Kama majority of CCM wataiunga mkono Chadema against JPM then utegemee Tanzania mpya? Kwa akili hizi CCM hawaondoki leo wala kesho ....
Nanuku toka kwa Godbless Lema ( Haya tunayofanyiwa sisi kama mkafikiri yanaishia kwa Wabunge tu kweli Mekosea sana yatakuja tu na Kwenu) Nukuu ya Pili Kutoka kwa Baba wa Taifa Mtu akizoea kula nyama ya binadamu hataka aache
 
Ninaupenda udikteta wa kutuletea maeneleo kuliko uungwana wa kutufanya mikia miaka nenda miaka rudi. Rais Wangu chapa kazi, tunataka kuiona Tanzania yenye neema na heshima haraka iwezekanavyo. Nasema tena chapa kazi, you have my full support.
 
Nanuku toka kwa Godbless Lema ( Haya tunayofanyiwa sisi kama mkafikiri yanaishia kwa Wabunge tu kweli Mekosea sana yatakuja tu na Kwenu) Nukuu ya Pili Kutoka kwa Baba wa Taifa Mtu akizoea kula nyama ya binadamu hataka aache
Hilo ndio tatizo lenu kila mwaka.Huwezi kutegemea mabadiliko kwa kuungwa mkono na CCM.
2015 mliwasubiri CCM wawasaidie haikuwa.
Juzi mliwatumia waraka wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wakatae mabadiliko ya katiba wakapitisha kwa 100%.
Chadema mnaonekana mmechoka,hakuna akili mbadala inayoweza kuibua hoja mpya.Mtasubiri sana mpate wana CCM wa kuwaunga mkono,wenzenu wana itikadi,sio bendera fuata upepo
 
Back
Top Bottom