Siku kanda ya Kaskazini wakiamua kujitenga kama Biafra

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
19,998
49,115
Miaka ya karibuni Sudan Kusini imepewa uhuru wake baada ya kujitenga na Sudan Kaskazini,huko nyuma mwishoni mwa miaka ya 60 eneo la Biafra nchini Nigeria liliwahi kutaka kujitenga na nyerere akawa upande wa Biafra hali iliyomletea kutoelewana na viongozi wa Nigeria wa wakati huo
miaka ya karibuni katika nchi yetu wazanzibar waliowengi wanatamani kujitenga na tanzania bara ili wajitawale wao kama wao,sasa pepo hilo la kujitenga limekwenda mpaka mikoa ya kaskazini,Tanga,Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Mara.kama sio leo kesho ipo siku mikoa hii itadai mamlaka yao kamili kama hali ikiendelea hivi,nadhani wanapata kiburi kwa kuwa wana bahari,maziwa(victoria,natron ,manyara)ardhi nzuri na asilimia 80 ya utalii kwa huku bara umejikita katika mikoa hiyo.serengeti,manyara na mt kilimanjaro.Sijui watajiita Tanzania Kaskazini kama wenzao wa Sudan au Korea kaskaini,kama si leo ni kesho mimi na wewe hatujui lakini hilo lipo,ila kujitenga kwa Zanzibar kutatokea kabla kizazi hiki kutoweka duniani
 
Last edited:
Si hata jeshua nasari alishaawahi kulisema hilo kuwa wanataka wajitenge
 
Hiyo nchi itakua geographia yake yenyewe tu kivutoa to cha utalii...maana itakua ni ndefu na nyembamba kama kamba.
 
Mi ni wa kaskazini ila siungi mkono hoja yako. Hakuna sababu ya kufanya eti mikoa ya kaskazini kujitenga. Hizi chuki za kikabila zinaenezwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi ionekane eti kwamba sisi watu wa kaskazini ni wakorofi kitu ambacho sio kweli. Yaani hapa hajitengi mtu tupo na nyie sambamba.

Yaani unafikiri wachaga wao ni wajinga kiasi hicho. Nchi ishakuwa na gas na Oil halafu tujitenge si itakuwa tumepishana na gari la pesa.???? Eboooo :eek:
 
Last edited:
Kwann watu wako obsessed sana na watu wa kaskazini? Nchi haitawaliwi na wakaskazini lakini kila siku kuna thread mpya kuhusu “hatari” ya watu wa kaskazini kwa Tanzania. Hamna vitu vya maana vya kufanya?
 
Mi ni wa kaskazini ila siungi mkono hoja yako. Hakuna sababu ya kufanya eti mikoa ya kaskazini kujitenga. Hizi chuki za kikabila zinaenezwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi ionekane eti kwamba sisi watu wa kaskazini ni wakorofi kitu ambacho sio kweli. Yaani hapa hajitengi mtu tupo na nyie sambamba.
Ni.mawazo yake tu na jinsi anavyoona hali inavyokwenda but utaratibu ukiendelea hivi wa kutenga na kudunisha maendeleo ya kaskazini mashariki,amini nakuambia hilo vuguvugu litaanza tena hata haitachukua muda saaana.
 
hakuna haja ya matengano , haki na umoja ni ngao , tushikilie hivyo tusifuate ubinafsi
 
Umeleta hoja ya kijinga kupita maelezo. Siasa za ukanda zilianzishwa na kikwete na familia yake wakiungwa mkono na Nape Nnauye kama silaha yao dhidi ya CDM. Kwa sasa hoja hii haina mashiko sana sana itakushushia hadhi yako mleta hoja.
 
Sawa mshajua kuwa watu wa kaskazini ni “wezi sana” jengeni “grili” kila sehemu sasa. Nadhani ukiona mtu anafatilia kitu kimya kimya ujue anakikubali.. Poleni na hiyo obsession yenu

Nyie wezi, acheni wizi. Nyie hamuoni aibu kila kwenye wizi mnajitokeza? Kwenye mazeti mnatangazwa nyie. Acheni hizo
 
Nyie wezi, acheni wizi. Nyie hamuoni aibu kila kwenye wizi mnajitokeza? Kwenye mazeti mnatangazwa nyie. Acheni hizo
Sioni kama una hoja ya msingi. Ni kama vile watu wanaona mtu flan ametoka wanaishia vijiweni kusema jamaa ameenda kwa mganga bagamoyo ndo maana.. Kama kweli kaenda kwa mganga kwann nawe usiende? Kama ni wezi hivyo mamlaka husika hazipo? Au kama vipi nawe jiunge katika “wizi” wa watu wa kaskazini
 
Kujitenga haitawezekana kwasababu wakaskazini wanaoishi nje ya kaskazini ni wengi sana kuliko walio ndani ya kaskazini.
 
Back
Top Bottom