Siku 100 za Rais Samia naiona dhamira njema aliyonayo kwa nchi yetu

Mtumishi wangu Nebukardezari, huyu alikuwa ni Mfalme wa Babeli. Na bado Mungu alimwita mtumishi wake sembuse JPM.
Kama JPM alikuwa mtumishi wa Mungu aliyehai kama Nebukadreza anashindwaje Mama Samia kuwa mtumishi wa Mungu?

Mungu hana double standard ndio maana Israeli alipokosea alichapwa kama wengine.

Mungu ai mwanadamu hata aseme uongo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mara hii ushasahau jinsi gani Corona ilivyomchukuwa rafiki yako wa Chato?
Hivi watu mbona muna akili fupi kama za kuku na mtama?

Mungu alijitukuza kwenye kumchukua jua hilo kama hukujua hivyo. Ndio maana twawaonea huruma hawa wanao fanya maaumzi ambayo wengi wa Watanzania wanayashangaa ingawa wakiwa kimya. Na kutoa ujumbe kwa kuukata wito wa kuvaa barako huku kitaa.
 
Kw hiyo unamaanisha Majaliwa siyo mkali? Majaliwa kasoma mchezo wa mama kwa hiyo anacheza ndani ya key.

Anataka nafasi ya Majaliwa ila kachelewa. Kila Mtanzania wangazi zote anaye jielewa anajua Majaliwa ni kiongozi na alikuwa mdau wa mafanikio ya JPM. Walio kuwa wanaenda kinafiki nafiki na JPM ndani ya miezi hii wamejidhihirisha.
 
Mungu alijitukuza kwenye kumchukua jua hilo kama hukujua hivyo. Ndio maana twawaonea huruma hawa wanao fanya maaumzi ambayo wengi wa Watanzania wanayashangaa ingawa wakiwa kimya. Na kutoa ujumbe kwa kuukata wito wa kuvaa barako huku kitaa.
Mungu hana sababu yoyote ya "Kujitukuza", hivi nyinyi binaadam akili zenu zipo wapi?
 
Dhamira njema ya kutuletea chanjo ya corona? Mungu kamletea ujumbe kupitia kupokelewa kuvaa barakoa huku kitaa. Mfalme Nebukardezari aliletewa kwa kiganja kilicho uaandika ukuta. Kutaka kuonesha approach ya kumtegemea Mungu haikuwa sahihi!!! Mungu atajidhihirisha tu.
Wewe ni taahira kweli, kwa hiyo ulikuwa unataka uletewe chanjo ya pepopunda au? Ninyi misukule jiwe alifanikiwa kuwa brainwash sana.
 
Mungu hana sababu yoyote ya "Kujitukuza", hivi nyinyi binaadam akili zenu zipo wapi?

Ni kiswahili tu Mkuu basi katukuzwa kupitia tendo hilo. Yesu alimuomba Mungu Utukufu wake Baba yake 'Mungu' na kwa kupitia utukufu huo amtukuze Baba yake 'Mungu wa Mbinguni' Tafuta hiyo Yohana Mt 10:
 
Kilio cha wakulima wa Tanzania ni soko, pembejeo na bei. Msimu ujao wa kilimo sera ya awamu ya sita itakuwa wazi kwa wakulima. Na ameanza kwa kurudisha bodi ya korosho.

Tofauti na awamu iliyopita ambapo bei za mazao zilishuka na wakulima kupata hasara ikiwa pamoja na kudhulumiwa hela za korosho.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Ana kazi kubwa mno kuliko hiyo unayotaja hapo ya kuwahudumia masikni wa nchi hii. Siku mia moja umati wa asilimia 65 na zaidi ndio ungekuwa umeshamtambua kwamba anasimama nao bega kwa bega.
 
Wewe ni taahira kweli, kwa hiyo ulikuwa unataka uletewe chanjo ya pepopunda au? Ninyi misukule jiwe alifanikiwa kuwa brainwash sana.

Tahira ni wewe unayefikiria kutumia tumbo na kuacha akili ulizokirimiwa bure na Mungu wa Mbinguni. Huwezi kujiuliza kwa nini iwe ni chanjo tu hii ya corona iliyoleta kilio ulimwenguni cha kutiliwa mashaka kote? Unaweza kuwa Rais wa Taifa lenye roho 60M na ushee halafu ushindwe kufikiri kwa mrengo huo?
 
Ni kiswahili tu Mkuu basi katukuzwa kupitia tendo hilo. Yesu alimuomba Mungu Utukufu wske na kwa kupitia utukufu huo amtukuze Baba. Tafuta hiyo Yohana 10:
Unajua mkuu 'Shehullohi' (onga!); ngoja nikuache, kwa maana hizi kazi zenu ni ngumu kwelikweli kwa watu vichwangumu kama sisi tunaoamini kwamba nyinyi binaadam mnamfanya Mungu aonekane kama jambazi fulani hivi ambalo huvizia watu na kuwaumiza kwa njia mbalimbali.
Asiyetaka kamwe viumbe wake wajione huru na kufurahia maisha yao aliyowajalia ili wayaishi na kuyafurahia kadri ya uwezo aliowajalia yeye mwenyewe.

Mungu ni mwenye huruma isiyokuwa na kiwango wala mwisho, na wala hawezi kumvizia mtu yeyote anayeishi maisha yake bila kuathiri maisha ya mwingine. Mungu hahitaji kusifiwa, kutukuzwa na kupewa kila aina ya majina na sifa, kwa maana yote haya ni yake. Kutambuwa uwepo wake tu, na kuishi katika misingi ya kibinaadam, inatosha kumfurahisha.

Kazi njema (mgoshi)!
 
Tahira ni wewe unayefikiria kutumia tumbo na kuacha akili ulizokirimiwa bure na Mungu wa Mbinguni. Huwezi kujiuliza kwa nini iwe ni chanjo tu hii ya corona iliyoleta kilio ulimwenguni cha kutiliwa mashaka kote? Unaweza kuwa Rais wa Taifa lenye roho 60M na ushee halafu ushindwe kufikiri kwa mrengo huo?
Imenibidi nirudi haraka baada ya kuaga.

Kwa mawazo haya, unakosea sana, na yote ni sababu hujui unachoongelea hapa. Chanjo inafanya kazi vizuri sana hadi sasa, huko inakopatikana. Hakikisha, itakapopatikana tu hapa nyumbani usikose kwenda kupata chanjo.
Mungu hazuii kutumia akili. Sayansi ni kutumia akili.
 
Kabisa Mungu ajazuia kutumia akili alichokataa ni kutegemea akili zetu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom