DENLSON
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 944
- 1,253
Ndani ya siku 100 Mh Rais ameonesha dhamira njema.
1. Uhuru wa kutoa maoni- Kwa kadili yake mwenyewe alituambia yuko tayari kukosolewa na kweli watu wanakosoa na anasikkliza mfano siku ambayo aliteua wakuu wa taasisi na watu wakasema mtu flani hafai asubuhi akatengua uteuzi. Hii inajumuisha na kuingia twitter bila VPN.
2. Demokrasia - Ameonesha dhamira njema ya kusikiliza maoni mbadala, kabla ya hapo Mbowe asingepata hata nafasi ya kuzindua ujenzi wa ofisi za chama
3. Sekta binafsi - Ameweka wazi anataka kufanya kazi na sekta binafsi na ameshakuta na wafanyabiashara na wawekezaji kuhusu hili.
4. Uhuru wa Mihimili ya Serikali - Hatujasikia kuna mhimili uliojichimbia chini sana. Mahakama inatoa hukumu angalau bila kulalia upande wowote.
5. Kodi - ameweka wazi hataki mapato ya dhulma.
6. Ajira na Mishahara - amesema ataongeza mishahara mwakani huku akijitahidi kuongeza ajira kwa kadri ya uwezo wa Selikari kwa sasa.
7. Uhusiano wa kimataifa - amefanya mabadiliko makubwa kwenye wizara pamoja na kurudisha uhusiano na mataifa jirani.
9. COVID-19 ameweka wazi msimamo wake ingawa haupendwi na wafuasi wa chama chake ila ndio ukweli wenyewe. Sisi sio kisiwa.
10. Uendelezaji wa miradi - anajitahidi kwa kadri awezavyo miradi ambayo tayari hela imetumika ikamilike ili fedha za Watanzania zisipotee.
Kwa kweli naiona DHAMIRA NJEMA ya Mh Rais na mimi kama mlinzi wa zamu sitanyamaza kumkumbusha Mungu kuhusu wewe mpaka atakapoifanya imara nchi hii ili kupitia yeye tupate KATIBA MPYA na kupitia yeye ule mshikamano na umoja wa Watanzania uonekane tena.