Siku 100 za Rais John Pombe Magufuli

Siku 100 za Rais John Pombe Magufuli




Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.



Waandishi wa habari na Madaktari wakifuatilia mkutano huo leo.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Museru akisisitiza jambo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali hiyo.



Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo.

………………………………………………………………………………………………………………….

Wagonjwa anaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi sasa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa yaliopo hospitali hapa.

Mafanikio hayo yamekuja baada ya uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa Tehama katika utoaji na uagizaji dawa.

“Wagonjwa wanaokosa dawa kwenye maduka yetu, hospitali inanunua haraka ili mgonjwa apate dawa kwa wakati. Kwa sasa ukosekanaji wa dawa hospitalini umepungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kuimarisha utendaji ndani ya hospitali,” amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.

Hayo yamesemwa leo na Profesa Museru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Profesa Museru amesema kwamba Katika muda wa kipindi cha miezi miwili Disemba 2015 na Januari 2016, hospitali imefanikiwa kulipa wafanyakazi malimbikizo ya madai yao ambayo walikuwa wakiidai hospitali hiyo kwa kipindi kirefu.

Malipo hayo ni malipo ya on call, malipo ya wauguzi ya usiku, malipo ya posho mbalimbali hasa kwa madaktari pamoja na kada nyingine za afya ambazo zinashughulika moja kwa moja na wagonjwa.

Amesema kwamba kutolipwa kwa malipo hayo kulishusha morali ya wafanyakazi kwa kiwango kikubwa na kupunguza kasi ya ufanyaji kazi na hivyo kusababisha kukosekana kwa tija katika utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.

Katika hatua nyingine, Profesa Museru amesema kwamba mapato kwenye hospitali hiyo yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 baada ya Disemba hospitali hiyo kuzalisha Shilingi bilioni 3.3 kutoka wastani wa shilingi 2.7 zilizokusanywa miezi mitano (Julai 2015 hadi Novemba 2015)

“Mwezi Disemba mwaka jana tulizalisha shilingi bilioni 3.3 na Januari 2016 tulizalisha shilingi bilioni 4.3,” amesema mkurugenzi huyo.

Akizungumzia mashine za CT-Scan na MRI, Profesa Museru amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli ilinunulia Hospitali hiyo mashine mpya ya CT-Scan yenye uwezo wa 126 slices.

“Uwapo wa mashine hii mpya umeongeza uwezo kwa kiwango kikubwa wa kupima wagonjwa wengi kwa wakati mmoja. Sasa tunaweza kumpima mgonjwa mmoja tumbo na kifua kwa sekunde sita. Awali tulikuwa tunapima wastani wa wagonjwa 20, lakini sasa tunapima wagonjwa wastani wa 50 ndani ya saa 24.

“Baada ya kuwapo kwa mashine hizi mbili za CT-Scan, Hospitali haitegemei tena kukosekana kwa vipimo vinavyohitaji mashine hizi. Aidha mashine hii mpya ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye nguvu kubwa imewezesha kufanya vipimo vya kiutalaamu zaidi hasa kwa upande wa viungo vya ndani kama moyo, utumbo, ubongo na hivyo kupata majibu sahihi ya chunguzi na uhakika zaidi. Mashine hii mpya tangu ilipofungwa Novemba 26, 2015 hadi Februari 9, 2016 imepima wagonjwa 863,” amesema Profesa Museru.

Amesema kwamba baada ya mashine ya MRI kutengenezwa wagonjwa zaidi ya 2,200 wamepimwa na kwamba baada ya mashine ya CT-SCAN kutengenezwa wagonjwa zaidi 1,000 wamepatiwa vipimo.
 
Nafikiri tukiendelea hivi matatizo ya wagonjwa yatapungua na huduma za matibabu zitaboreka zaidi
 
Habari wana JF,

Naomba kuchukua fursa hii kwa unyenyekevu na uaminifu kuwashirikisha katika kuzihesabu pamoja siku 100 za Rais Dkt John Pombe Magufuli madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kuapishwa kwake. Aliapishwa Alhamisi Novemba 5, 2015 hivyo uhesabuji wa siku mia utakoma Jumapili Februari 14, 2016 kisha tutafanya analysis ya changamoto/matatizo na mafanikio yake ndani ya siku hizi kama inavyofuatiliwagwa kwa marais wote Duniani huku ikijumuisha matukio yote muhimu yaliyotokea/kujili wakati huo.


Alhamisi Novemba 5, 2015 aliapishwa na kuwa Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo saa sita mpaka saba mchana,uapisho huo ulifanyika katika viwanja vya Uhuru, Jijini Dar es Salaam.


attachment.php


baada ya kuapishwa jioni hiyohiyo akitumia malaka aliyopewa kikatiba kama Rais, alimteua mtumishi wa kwanza katika serikali yake ya awamu ya tano. Mtumishi huyo alikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju.

attachment.php


Mapema Ijumaa ya Novemba 6, 2015 yapata majira ya saa nne asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam alimuapisha George Masaju na kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali.

attachment.php

Baadae siku hiyohiyo, Ijumaa ya tarehe 6 alifanya ziara ya kushutukiza Wizara ya fedha na kubaini changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na utoro wa watumishi. Rais Dkt John Magufuli hakuwakuta baadhi maofia wa Wizara hiyo pindi alipotembelea.


Jumamosi ya Novemba 7, 2015 Ikulu JIjini Dar es Salaam Rais Dkt John Pombe Magufuli alikutana na watumishi wa serikali ikiwa ni pamoja na Manaibu Katibu Wakuu, Manaibu Wakuu na Watendaji Wakuuu wa Serikali huku akiwaambia wajiandaa kufanya kazi kwa ufanisi katika serikali ya awamu ya tano chini yake. Mbali na hapo, aliwaambia dhamira yake ya kuendeleza sera yake ya "Hapa Kazi Tu" na kuongeza kuwa haikuwa ya kuombea kura tu bali ndio aina ya mtu (yeye) alivyo, kuagiza watumishi hao kutenda zaidi na kufika vijijini kubaini matatizo na changamoto zinazoikabili jamii, kufuta safari za Nje za watumishi mpaka pale atakapotoa tamko tena au kuwa rishaa yake, posho na vikao visivyo na lazima, kuwaasa watumishi wa serikali kutoongeza thamani za gharama katika matumizi ya serikali na pindi ikibainika wahusika watachukuliwa hatua papohapo ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, kushughulikia suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na mwisho aliagaiza uanzaji wa kutoa huduma bure za elimu kwa wanafunzi watakao anza shule mwaka wa masomo 2016 na kusema watumishi waanze andaa mpango mkakati wa kutekeleza yote yaliyoazimiwa katika kikao hicho.

attachment.php

attachment.php


Karibuni katika thread Maalum ya siku mia za Rais John Pombe Magufuli.

Jumatatu November 9, 2015 Rais Dkt John Pombe Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza kwa kutembelea Hostipali ya Taifa ya Muhimbili. Katika matembezi hayo, Rais Magufuli alipata nafasi ya kwenda kutembelea na kumjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha Hakiza Binadamu na Sheria (LHRC) Nchini Dkt Helen Kijo Bisimba aliyepata ajali ya gari yenye namba za usajiliT336 CTT siku ya jumapili.

attachment.php
attachment.php


Mungu ibariki Afrika,
MUngu ibariki Tanzania.
Msiache kutuwekea links za yale yaliyoandikwa nje ya mipaka ya Tanzania au Kimataifa hapa.
 
... Nikiwa kama mtanzania mpenda mageuzi endelevu (sio mabadiliko tafadhali) nimependa na kufurahia kasi ya Magufuri
Mkuu, mageuzi endelevu hayaletwi nna juhudi za mtu mmoja mmoja, bali mfumo kumlazimisha mtu yeyote atakayeshika madaraka ya urais
Kwa mfano, kama tukilazimika kikatiba kufanya uchaguzi wa rais mwaka huu huu, na tuliyemchagua hana utashi wa kupeleka mambo kwa kasi kama ya JPM, na mfumo (katiba) haimlazimishi kufuata style kama ya JPM, unadhani hayo mageuzi yanastahili kuitwa endelevu? Nani anayaendeleza hadi yaitwe endelevu?
 
Lowassa njoo tuambie siku mia za mhishimiwa zimekaaje
Adui yako si Lowasa eti kwa kuwa aligombea na JPM, adui yako ni yule aliyeshindwa kuyaleta mafanikio hayo kwa muda wa miaka 10 aliyokuwapo madarakani
 
Adui yako si Lowasa eti kwa kuwa aligombea na JPM, adui yako ni yule aliyeshindwa kuyaleta mafanikio hayo kwa muda wa miaka 10 aliyokuwapo madarakani
Lowassa alikuwa campaign manager wa yule aliyekaa madarakani kwa miaka 10. Kama huyo mheshimiwa alifanya madudu, maana yake ni kwamba Lowassa anahusika katika kutuletea madudu yaliyotutesa kwa miaka 10. Na pengine ni bahati kwa taifa kwa lowassa kushindwa kupata uongozi, kwani siioni tofauti kati yake na yule ambaye alihakikisha anaiongoza nchi kwa miaka 10.
 
Back
Top Bottom