Siku 26 tangu kutangazwa kuwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. JOHN POMBE MAGUFULI, amefanya yafuatayo ikiwa ni mipango yake ya kubana matumizi ya serikali , kusimamia utendajikazi wa idara na taasisi za serikali, kuhakikisha huduma za kijamii zinaboreka n.k:
1. Amefanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya fedha.
2. Amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kumsimamisha kazi aliyekuwa mkugenzi wa Hopitali hiyo kwa kipindi hicho. Aidha kwenye ziara hiyo aliagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha Machine za MRi na CT-SCAN zinafanyakazi na katika kutekeleza agizo hilo, Wizara ya fedha ilitoa zaidi ya Bil.3 kulipa sehemu ya madeni ya matengenezo ya mashine hizo.
3. kufanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya Bandari Tanzania.
4. Amefuta matumizi ya zaidi ya shilingi mil 250. zilizokuwa zitumike kwa ajili sherehe za ufunguzi wa bunge la 11 na zikapelekwa Hospitali ya MUHIMBILI kununua vitanda, magodoro na mashuka kwa ajili ya Wagonjwa.
5. Amefuta safasi kwa watumishi zaidi ya 50 waliokuwa wahudhurie mkutano wa jumuiya ya Madola nje ya nchi, safari ambayo ingegharimu takribani shilingi mil.700
6. Amefuta sherehe za siku ya Uhuru zinazofanyika Desemba 9 ya kila mwaka na kuagiza Watanzania kutumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao ili kukabiliana na mpuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa sasa uko mikoa mingi nchini. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu kiongozi, Rais anafikiria pesa zitakazotokana na kufutwa kwa sherehe hizo zifanye kazi gani.
Nimeguswa sana na jitihada hizi binafsi(narudia, jitihada binafsi) za rais. Hivyo nimeamua kuanzisha mada mahsusi ambayo nitakuwa naihuisha kila wakati rais atapokuwa anaibuka na jambo jipya kabisa.
Mods, nawaomba sana mada hii ikae pale juu kabisa ili iwe inaonekana kirahisi kwa kila mmoja wetu ili kujionea mambo gani rais wetu yameapa uzito tangu aingie madarakani.
TUUNGE MKONO JUHUDI HIZI ZA MHE. RAIS KWA MAENDELEO YA TAIFA.