MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA, UZEMBE, UBADHIRIFU NA UFISADI YANAENDELEA, UPINZANI UPO LAKINI SI WA KISIASA BALI WA WASOMI NA WACHUMI
Akiwa ndani ya Kombati kuelekea kambi ya Mafunzo kwa Maofisa wa Kijeshi Monduli, Magufuli alionekana kuwa mwenye nguvu, mchangamfu na msikivu kuliko kawaida. Amiri Jeshi Mkuu, Aliahidi kutumia nguvu kazi ya Majeshi katika kukuza Uchumi wa Taifa.
Ili kwenda na kasi ya Magufuli TAKUKURU wamefanya uchunguzi na kukamilisha uchunguzi wa tuhuma nzito 36 zinazohusu wizi, ukwepaji kodi na ubadhirifu wa mali za umma.
Miongoni mwa kesi hizo ni;
1. Lake Oil - Tuhuma za Ukwepaji wa ulipaji kodi
2. EGMA - Tuhuma za Ununuzi wa mabehewa chakavu
2. TRL - Tuhuma za Ukiukwaji wa kanuni wakati wa utafutaji wa makandarasi wa ujenzi wa reli ya kisasa.
Tuhuma hizi pamoja na zile zingine 33 zitaombewa kibali toka kwa DPP ili zipelekwe mahakamani.
Habari nzima ni kama ilivyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi la Tarehe 27/01/2016.
ODOMA: SIMBACHAWENE AMVUA KAZI MKURUGENZI WA MANISPAA.
Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma alivuliwa ukurugenzi baada ya kutuhumiwa kushindwa kusimamia zoezi la Elimu Bure Mkoani humo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida NIDA imetumia Bln180 kuandikisha si zaidi ya watu mln5 ile hali Tume ya Uchaguzi walitumia pesa hiyohiyo kuandikisha watu zaidi ya mln20.
Mkurugenzi wa NIDA pamoja na maofisa kadhaa wamefutwa kazi na Raisi ameagiza uchunguzi ufanyika mara moja na watakaobainika kuhusika wapelekwe mahakamani mara moja. Vyombo vya kiuchunguzi vilivyokabidhiwa dhamana hiyo ni CAG, TAKUKURU na PPRA.
Kisha Mabalozi wa Tanzania nchini Japani na Italia mikataba yao ya kazi imeisha na wamerudishwa nyumbani mara moja, huku balozi wa Uingereza na Italia wakirudishwa nyumbani kwa kushindwa kufanya kazi vizuri.
Siku hiyo hiyo Mhandisi Madeni Kipande alisitishwa kazi yake ya katibu tawala mkoa wa Simiyu baada ya kumaliza muda wake wa majaribio wa miezi 6, na kuonekana kwamba hawezi kumudu kasi ya Magufuli.
Habari kamili imeandikwa katika Gazeti la Mwananchi la Tarehe 26/01/2016.
UHAMIAJI NAO WAHAMISHWA:
Tarehe 21/01/2016 Gazeti la Mwananchi lilichapisha habari iliyokaririwa ya kwamba Balozi Ombeni Sefue ametoa taarifa juu ya utenguzi wa Kamishana wa Uhamiaji pamoja na Ofisa Wake wa fedha wa taasisi hizo. Ameagiza uchunguzi ufanywe mara moja na kama watagundulika kuhusika na tuhuma hizo basi wachukuliwe hatua stahiki za kisheria.
TANGA: Baadhi ya watoto wa darasa la kwanza walilipishwa kati Sh3,000 na Sh6,000 ili kuandikisha watoto darasa la kwanza. Hbari kamili ipo Gazeti la Mwananchi, hii inaenda kinyume na Tangazo la serikali la ELIMU BURE
MBOWE NA LISU: Kwa nyakati tofauti wamepinga ama baraza la mawaziri kufanya kazi bila miongozo na kufuata sheria za kazi, au kufanya kazi kama mawaziri (hawa ni wale mawaziri walioteuliwa na Rais) ile hali hawajaapishwa kuwa wabunge na pia kwa Rais kuongoza kwa amri au decree. Upinzani huu si mpya kuzingatia hawa ni wanasiasa
na mawaziri wa magufuli.
WASOMI: Mpaka tarehe 13 January 2016 maofisa takribani 20 wa serikali walikuwa tayari ama wamefutwa kazi na mawaziri wa Magufuli au kuhamishwa kazi kama ilivyoripotiwa hapa na Gazeti la Mwananchi. Wasomi Tanzania wanasema hiyo siyo dawa kwa kuwa timuatimua hizo zimekuwa za KUKURUPUKA.
Waliokwisha kutoa maoni yao ni pamoja na Mohamed Bakari (UDSM), Lilian Liundi (TGNP), Harold Sungusia (LHRC) na Kitila Mkumbo (UDSM) wote wakilaumu ukosekanaji wa ufumuaji wa mifumo ya kijamii, kiuchumi na kitamaduni iliyotufikisha hapa kama Taifa. Huku wengine wakihusisha timuatimua ya zaidi ya Vigogo 70 (ambao Magufuli anawaita majipu) na mambo ya siasa na visasi. Pia wengi wanauliza je mbona hakuna mkakati wa kukuza uchumi?
ELIMU BURE YAIBUA MAPYA. Pesa ya walinzi, chakula, usafi, ukarabati wa majengo na vifaa vya kazi hazikuwekewa katika mahesabu ya Magufuli. Baadhi ya shule walinzi hawakuja kazini na vifaa kuibiwa. Baadhi ya shule za sekondari walioajiri walimu kama vibarua walimu hawakufika kazini. Ile hali wazazi wameleta watoto kwa wingi wakijua ELIMU NI BURE.
Baadhi ya watoto wanaenda shule bila daftari wala kalamu, huku shule zenye watoto wengi zikihitaji kushona nembo za majina ya watoto na hela za nembo haziko kwenye bajeti ya serikali. Bajeti ya serikali ni Sh10,000 kwa kila mtoto kwa mwaka. Hii ni kama tone la maji katika jangwa kwani watoto walikuwa wanalipa 10,000 kwa wiki hasa shule za mijini.
OFISI ZA SERIKALI ZIPO NYUMBA ZA KUKODISHWA: Serikali inadaiwa pango la ofisi zake mbalimbali nchini kwa kuwa imepanga kutokana na kukuosa kuwa na ofisi za kutosha Tanzania. Haijafahamika mara moja inadaiwa kiasi gani lakini dhahiri kuna hatari ya serikali nayo kutimuliwa na wenye nyumba. Habari hii ipo hapa. Imagine hadi NEC wanaishi nyumba ya kupanga.
WAHARIRI - MKAKATI WA KUBANA MATUMIZI UANGALIWE UPYA
Mhariri huyu analalamika sana kuhusu kufutwa safari za nje huku akiunganisha ufutwaji wa safari za nje na kushuka ama kupungua idadi ya watalii nchini na sekta mbalimbali zilizounganishwa katika mnyororo wa shughuli hizo za kitalii, ingawaje mhariri huyu anaweza kuwa na point swali na kujiuliza hapa ni kuwa je mawaziri wetu ndio walikuwa wanawalete watalii wakiwa wametoka nje ya nchi? Na je kwa nini watalii wasiendelee kujaza madenge hayo kama walikuwa hawalipiwi nauli? Hariri ya Mhariri wa Mwananchi ipo hapa.
MEMBE
Membe bado analia na safari za nje ya nchi kufutwa na pia kulalamika ya kwamba baraza la mawaziri si dogo, ile hali yeye mwenyewe akigombania Urais ndani ya chama chake hakuwa na agenda ya kubana matumizi wala kupunguza idadi ya wizara.
Na pia alienda mbali zaidi kwa kumtaka Rais kwa-handle vizuri wafanyabiashra. Yaani awabembeleze kulipa kodi isije wakaondoka na kwenda kuwekeza nchi zingine. Hoja za membe zimejibiwa na Husein Bashe kwa kumtaka Membe amwacha Magufuli afanye kazi yake.
habari kamili ipo hapa,
Price Watch Afrique: MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA, UZEMBE, UBADHIRIFU NA UFISADI: KUELEKEA SIKU 100 ZA UTAWALA WA RAIS WA TANZANIA DR JOHN POMBE MAGUFULI
na kazi alizofanya magufuli ndani ya siku 60 ipo hapa
Price Watch Afrique: SIKU 60 ZA UTAWALA WA MAGUFULI