Kuna mambo mengi yanayoweza kufanya mtu aheshimiwe au apuuzwe, uzi ulioweka hapa sidhani kama kuna sababu ya kutoupuuza. Moja ya sifa ya watanzania wengi ni kushabikia mambo ya kuambiwa ambayo hayana maana au ukweli. Hakuna dhambi kubwa kama kumsingizia mtu, kumchukia mwenzako au kumnenea mabaya. Sidhani kama ni sahihi kumzushia mtu kuwa ni fisadi au vyovyote vile bila kuwa na ushahidi kwa kutosha, hii ni dhambi kubwa. Kwa serikali iliyopo sasa sidhani kama ingemvumilia hata siku moja mtu fisadi, tena mtu kama Lowasa nafikiri angekuwa wa kwanza kupelekwa mahakamani kama serikali ingekuwa inaushahidi wa kutosha.
Sio sawa wala haikubariki kwa mtu yeyote kuongea hoja za kizushi na uongo, tuhuma zozote zinathibitishwa mahakamani sio kwenye vijiwe vya kahawa, kama mtu yupo uraiani huyo mtu ni safi. Ni dhambi na aibu sana kwa mtu mwenye akili timamu kuongea mambo ya kusadikika wakati nafasi ipo ya kuthibitisha. Siasa nyingi za Africa zinaendeshwa kwa fitina. Huwezi kusema nyarandu ni fisadi sasa kwa kuwa ametoka CCM, vyama ni vyama lakini wote ni watanzania, ieleweke wazi kuwa CCM itaongoza nchi muda mrefu lakini sio milele, ipo siku upepo utabadirika na chama kingine kitaongoza. Hivyo hakuna sababu ya kuchukiana au kuzushiana mambo ya uongo yasiyo na usibitisho. Haki ndiyo inaweza kuliinua taifa na watu wake sio kusingiziana na kuoneana.