Sikiliza kaka

Sikiliza kaka

BR Stationary

Member
Joined
Oct 7, 2026
Posts
10
Reaction score
18
MAN TO MAN

Umri wa miaka 25–35 na kuendelea unaweza kuwa kipindi kigumu sana katika maisha.

Unaanza kuona wazazi wako wakizeeka, marafiki wakipungua, msongo wa mawazo kuhusu kazi na maisha, huku ukipambana na mashaka juu ya uwezo wako mwenyewe.

Familia yako inatarajia uwe imara, uvumilie na uonyeshe kuwa unaweza kukabiliana na kila kitu.

Unaanza hata kupoteza hamu ya mambo ambayo zamani yalikuwa yakikupa furaha.

Lakini brother usikate tamaa, endelea kuwa imara. Hata kama mambo ni magumu kiasi gani, Huhitaji kuwa na majibu ya kila kitu leo.

Pambana hatua kwa hatua, jipe muda na usisahau kuwa hata mwanaume mwenye nguvu anahitaji kupumzika na kupata msaada. 🤝
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom